Nafasi ya kazi Halmashauri ya Wilaya ya Busega

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
2,083
2,000
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega amepokea kibali cha ajira mbadala cha tarehe 01 Februari, 2021 chenye Kumb. Na. FA.l701533/01,,B"l 34 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kutokana na hali hiyo, anawatan gazia Watanzania wote wenye Sifa na uwezo wa ktlaza nafasi moja (01) ya kazi kwa kada iliyoainishwa hapa chini:-

MTENDAJI WA KIJIJI III (Nafasi 01)-TGS B1

SIFA ZA MWOMBAJI

 • Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (lV) au Sita (Vl) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo; Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo-Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI
 • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijij
 • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezali wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji
 • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
 • Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE
 • Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
 • Waombaji wote waambatishe nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
 • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo binafsi (CV), nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika
 • Picha moja Passport Size iandikwe jina kwa nyuma
 • Hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (Statement of Results havitakubalika)
 • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma Wasiombe Kazi na wanapaswa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.451257l01lDl140 wa tarehe 30 Novemba ,2010
 • Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili na yatumwe kwa njia ya Posta kabla ya 25/02/2021 kwa anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya
s.L.P. 157
BUSEGA
 

Attachments

 • File size
  1.2 MB
  Views
  8

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom