DOKEZO Malalamiko kuhusu uongozi wa Afya – Halmashauri ya Mpimbwe (CHMT)

DOKEZO Malalamiko kuhusu uongozi wa Afya – Halmashauri ya Mpimbwe (CHMT)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naomba mamlaka husika ichunguze muundo na uteuzi wa viongozi wa CHMT katika Halmashauri ya Mpimbwe, kwa kuwa kuna baadhi ya nafasi za uratibu na uongozi zinazoshikiliwa na watumishi ambao sifa zao za kitaaluma hazilingani na majukumu wanayotekeleza, licha ya kuwepo kwa wataalamu wenye sifa stahiki.

Kwa mfano, nafasi za uratibu wa UKIMWI, chanjo, MTUHA pamoja na FFARS zinadaiwa kushikiliwa na watumishi ambao hawana sifa, taaluma au uwezo unaoendana na nafasi hizo. Hali hii inaweza kuathiri ufanisi wa huduma na ushauri wa kitaalamu katika uongozi wa Halmashauri.

Aidha, kuna madai kwamba baadhi ya viongozi hao hawahudhurii kazini mara kwa mara kutekeleza majukumu yao, huku wakidaiwa kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu uwepo wao kazini. Pamoja na hayo, wanaendelea kupokea mishahara na posho.

Baadhi ya watumishi wamewahi kuwasilisha malalamiko kuhusu suala hili kwa Mkurugenzi wa Halmashauri, lakini hadi sasa hakuna mabadiliko yanayoonekana.

Naomba mamlaka husika ifanye uchunguzi wa kina kuhusu sifa za watumishi walioteuliwa katika nafasi hizo, utekelezaji wa majukumu yao na utii wa taratibu za utumishi wa umma, ili kuhakikisha nafasi za uongozi zinashikiliwa na watu wenye sifa stahiki na wanaotekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
 
Pamoja na kuwa katika nyakati za upendeleo na upigaji hoja au tuhuma hii ingekuwa na mashiko sana kama ungeweka mfano halisi wa hao ambao hawana sifa lakini wameteuliwa kushika nafasi hizo.
 
Tunatoa malalamiko kuhusu mfumo wa uongozi katika Idara ya Afya ya Halmashauri ya Mpimbwe (CHMT), ambapo baadhi ya nafasi za uratibu na uongozi bado zinaendelea kushikiliwa na watumishi wenye kiwango cha elimu cha Diploma na Certificate, licha ya kwa sasa kuwepo kwa watumishi wenye sifa za juu zaidi, wakiwemo Madaktari (MD) na Nursing Officers wenye shahada.
Inaeleweka kuwa wakati Halmashauri inaanzishwa, watumishi wenye elimu ya juu hawakuwepo kwa wingi, hivyo baadhi ya watumishi walipewa nafasi hizo kwa mazingira yaliyokuwepo wakati huo. Hata hivyo, hali imebadilika lakini nafasi hizo bado hazijapitiwa upya. Mfano, Clinical Officer (CO) anakuwa mratibu wa UKIMWI na kutoa uongozi/uratibu unaowahusu Madaktari, wakati mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto mwenye Certificate anasimamia Nurse Officers wenye shahada. Hali hii inazua maswali kuhusu vigezo vinavyotumika katika uteuzi wa viongozi na waratibu.
Aidha, baadhi ya viongozi hao wanadaiwa kutumia nafasi zao kujipendekeza na kufanya uchawa kwa viongozi wakubwa ili kulinda nafasi zao, hali inayosababisha baadhi ya watumishi wengine kukandamizwa na kutotendewa haki kwa hofu kwamba wakuu hao wanaweza kuondolewa kwenye nafasi zao.
Pamoja na hayo, kuna malalamiko ya baadhi ya viongozi/waratibu kutofanya kazi ipasavyo, kutofika hospitalini na kutumia muda mwingi kufanya shughuli zao binafsi mtaani, huku mzigo wa kazi ukiwaangukia watumishi wengine. Baadhi ya watumishi tayari wamewasilisha suala hili kwa Mkurugenzi, lakini hadi sasa hakuna mabadiliko yanayoonekana.
Tunaomba mamlaka husika ichunguze suala hili kwa haki na bila upendeleo, ipitie sifa za viongozi na waratibu wote wa CHMT, izingatie taaluma na uwezo wa kila mtumishi katika kugawa majukumu, pamoja na kuchukua hatua kwa watumishi wa CHMT wasiotimiza wajibu wao wa kazi. Lengo si kumlenga mtu binafsi, bali kuhakikisha uongozi wa Idara ya Afya unazingatia sifa, taaluma, uwezo, uwajibikaji na haki kwa watumishi wote, kwa maslahi ya huduma za afya kwa wananchi wa Mpimbwe.
 
Back
Top Bottom