Nafasi 4 za kujitolea Elimu Tech Foundation (ETF)

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
4,876
10,593
Elimu Tech Foundation (ETF) ni shirika jipya lisilo la kiserikali linalojishughulisha na maendeleo ya tehama kwenye elimu hususani kwenye shule za serikali kwa kuhakikisha miundombinu ya tehama kwenye shule nchini inaboreshwa na kuhimiza matumizi sahihi ya tehama kwenye elimu kama msingi wa maendeleo endelevu kwa taifa kwenye karne ya 21. Shirika linafanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo upande wa tehama na elimu. kwa kushirikiana na wadau kwa sasa shirika limeanza kutekeleza program yake ya "technology in education" yenye kauli mbiu "shule zetu kidigitali" kwa kuwezesha huduma mbalimbali za tehama kwenye shule za serikali za msingi na sekondari nchini.

Elimu Tech Foundation (ETF) inatafuta (volunteer) kujaza nafasi ya program manager, finance officer, research & statistics officer.

Post: program manager 1 (volunteer)

Majukumu ya kazi

  • kusimamia mradi
  • kusimamia na kupanga gharama za mradi
  • kusimamia na kuandaa ratiba ya mradi
  • kuainisha vipao mbele vya mradi
  • kuandaa maandiko ya miradi midogomidogo
Elimu na uzoefu
Degree ya project management uzoefu ni kuanzia mwaka 1 na awe ameshiriki katika mradi wowote wa maendeleo katika nafasi ya usimamizi

Post: finance officer 1 (volunteer)

Majukumu ya kazi

  • Usimamizi wa Fedha
  • Kuwezesha Malipo
  • Kuandaa Hesabu za Mwisho wa Mwaka
  • Ushauri na Uthibiti wa fedha za mradi
  • Ukaguzi wa Awali wa nyaraka zote za fedha

Elimu na uzoefu
Degree ya usimamiz wa fedha na uzoefu ni kuanzia mwaka 1 na awe ameshiriki katika mradi wowote wa maendeleo.

Post: research & statistics officer 1 (volunteer)

Majukumu ya kazi;

  • Kusaidia kuandika na kukusanya ripoti za utafiti wa elimu na tehama
  • Kukusanya, kurekodi na kuchanganua takwimu za kazi za utafiti zinazoendelea
  • Kuandika mapendekezo ya utafiti
  • Kuandika ripoti za mradi na utafiti
  • Kufanya kazi zozote kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

Elimu na uzoefu
Degree ya research & statistic au inayofanania na hiyo na uzoefu ni kuanzia mwaka 1 na awe ameshiriki katika mradi wowote wa maendeleo.

Post: digital officer 1 (volunteer)

Majukumu ya kazi

  • Ukaguzi wa mahudhui na Usimamizi wa mitandao na kurasa zote za organization
  • Kuwezesha kutangaza program zote za organization kidigitali
  • Kutangaza na usimamizi wa posti zote za program kwenye mitandao ya kijamii
  • Uthibiti wa mahudhui kwenye mitandao na kurasa zote za organization

Elimu na uzoefu
Diploma au Degree yoyote
Awe na uzoefu wa digital marketing, Ubunifu ni sifa ya ziada

Maombi yote yatumwe kupitia elimutech4@gmail.com au kwa maelezo zaidi wasiliana kwa namba 0757563328 mwisho wa kutuma maombi ni tarehe: 20/08/2021
 
Back
Top Bottom