Nafasi za Kazi TAKUKURU

Nafasi za Kazi TAKUKURU

Abtali Mwerevu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
795
Reaction score
704
TAKUKURU imetangaza nafasi za kazi, nafasi mpya za kazi zilizotangazwa na TAKUKURU zimegawanyika katika makundi mawili:

Kundi la kwanza, Muombaji awe na angalau elimu ya shahada ya kwanza iliyotolewa na chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika moja ya fani zifuatazo: Uhasibu, Usanifu Majengo, Usimamizi wa Biashara, Usanifu wa Majengo, Ukadiriji wa Majengo (Quantity Surveying), Uhandisi wa Usindikaji wa Kemikali, Maendeleo ya Jamii, Sayansi ya Kompyuta/TEHAMA, Uhandisi wa Ujenzi, Uchumi na Mipango, Uhandisi wa Umeme. Lishe na Sayansi ya Chakula, Usimamizi wa Rasilimali Watu, Usimamizi na Tathmini ya Ardhi, Sheria, Uhandisi wa Mitambo, Uhandisi wa Mafuta na Gesi, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Miradi, Ushauri Nasaha, Utawala wa Umma, Mahusiano ya Umma/Mawasiliano ya Umma, Usimamizi wa Kumbukumbu, Sayansi ya Michezo/Elimu ya Viungo, Takwimu, na Uhandisi wa Maji.

Kundi la pili: ulinzi, ufundi wa magari, ujuzi wa udereva, huduma kwa wateja, msaidizi wa uhasibu, masomo ya ukatibu, fundi wa kompyuta na fundi wa mashine za ofisi.

Kama una sifa, changamkia fursa hiyo, Kupata Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi TAKUKURU Soma Hapa
 
Kwani mishahara yao bei gani haswa na mafunzo yanachukua mda gani
 
Mwisho tarehe 3 kwa walokua hawajakamilisha wajihimu wakamilishe
 
Mwenye uzoefu na usaili wa written au aptitude test za TAKUKURU atusaidie jamani tujue zinavyokua, maana wameitwa watu wenye taaluma mbali mbali Sasa ningependa kujua kama mtihani unakua Mmoja kwa watu WA taaluma zote au Kila taaluma watakua na mtihani wao
 
Mwenye uzoefu na usaili wa written au aptitude test za TAKUKURU atusaidie jamani tujue zinavyokua, maana wameitwa watu wenye taaluma mbali mbali Sasa ningependa kujua kama mtihani unakua Mmoja kwa watu WA taaluma zote au Kila taaluma watakua na mtihani wao
Soma Mfano wa Maswali Yanayotoka Hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom