Nadharia ya miaka 1,000 duniani ni sawa na siku moja mbinguni si sahihi kabisa

bwana mdogo Bible ni tofauti na science Bible inazungumzia mambo ya rohoni sasa wewe unaposema maandiko hayo si sahihi umepotoka
 
Ume "quote" aya za Qur'an lakini hujazielewa.

Siku ni kwa Kiswahili. Tafsiri pana ya neno siku kwa Kiarabu ni kipindi (period). Kipindi kimoja kwako kinaweza kuwa na muda tofauti na kipindi kimoja kwangu. Kipindi cha msimu wa mvua Tanzania ni tofauti na kipindi cha msimu wa mvua kwengine.

Allah hana mwanzo hana mwisho so siku yako moja kwake haina maana ni masaa 24. Na miaka 1000 kwako kwake haina maana bali kwako. Time ni "period less" kwa asiye na mwanzo wala mwisho. Anatumia time kukufahamisha wewe uwezo na ukubwa wake. Ni nje ya upeo wa kibinadam.
 
Angalia pia kwa sababu Dunia sio Sayari pekee , hata masaa ya siku yanatofautiana kutoka sayari moja hadi nyingine. Angalia masaa ya siku ya baadhi ya sayari .
Mercury1,408 hours
Venus5,832 hours
Earth 24 hours
Mars25 hours
Jupiter10 hours
Saturn11 hours
Uranus17 hours
Neptune16 hours

Kwa hiyo uko mbinguni itakuwa siku moja hapa ni miaka elfu moja huko inawezekana yaani hiyo sayari ya mbinguni inachukua muda huo kuzungukuka jua lililoko huko , kwani Universe ina majua mengi na mengine makubwa zaidi mara hata milioni moja ya hili la kwetu.
 
Hapo tutaelewana.. kwa Mungu Time is Timeless. Anasema hivo ili kutuelewesha jinsi ukuu wake ulivo..
 
Njoja nijenge hoja

Mwaka 1 duniani ni sawa na miaka mingapi kwenye sayari ya Jupiter au pluto. Kwa maana ya Jua kuzunguka dunia au sayari ya pluto .

Ukishajibu hapo haishindikani mwaka 1 duniani kuwa sawa na miaka 1000 mbinguni!
Hivi sayari ya mbinguni ni sayari ya ngapi? Labda tuanzie hapo
 
Alie kwambia mbingu ni sayari ni nan
 
Mbingu ni hali not a place so there is nothing counted
 
Yasiowezekana kwa mwanaadamu basi kwake allah inawezekana!je ulishawahi kujiuliza ngamia anawezaje kupita kwenye tundu la sindano?.
 
Si ngamia mnyama, ila ni kamba zinazofunga vitu vizito, nenda bandarin utaziona ngamia, au vivukoni kama busisi mwanza nk, ngamia ni kamba nene iliyosokotwa,ni kama mkono wako,mara nyingi inashikilia meli ikiwa bandarini, au kwenye nanga pia inatumika,

Sasa hiyo ipenye kwenye tundu la sindano, kazi ipo
Yasiowezekana kwa mwanaadamu basi kwake allah inawezekana!je ulishawahi kujiuliza ngamia anawezaje kupita kwenye tundu la sindano?.
 
Aiingii akilini !!!!! akili zako wewe mwendawazimu hayo mambo ya madrassa unayabadili kuwa ya biblia hautaweza utaona kila kitu hakiwezekani zaidi utajinyonga tu

Bila Mungu kufungua akili yenye ukungu hiyo.hapn kuelewa hekima yake.mfyuuuu!
 
Aiingii akilini !!!!! akili zako wewe mwendawazimu hayo mambo ya madrassa unayabadili kuwa ya biblia hautaweza utaona kila kitu hakiwezekani zaidi utajinyonga tu

Bila Mungu kufungua akili yenye ukungu hiyo.hapn kuelewa hekima yake.mfyuuuu!
Umeongea kimbea kama wadada wa sinza bila kujua kua mm ni Mkatoliki nayeielewa vizuri imani yangu na dini yangu kwa ujumla. Mungu kaifungua akili yangu ndio maana nimeweza kutiririka hayo
 
Hakuna sayari ya mbingu.. mbingu haifahamiki ilipo
Umejuaje hili ?

Unaposema mbingu haifahamiki ilipo una maanisha nini ?

Mimi nikisema mbinu iko juu nakosea tena nikaonyesha kabisa kwa ishara ?

Msaada tafadhali .....
 
Mbingu ni hali not a place so there is nothing counted
Unataka kusema mbingu ni kama joto au baridi au kama au njaa ?

Umejuaje hilo kama mbingu ni hali ? Maana hali zinajulikana na hali ili iwe hali ina hitaji "nafasi" na "muda",kadhalika mbingu ina sifa hizi mbili,kama nakosea nisahihishe nipate kujua.

Nasubiri ufafanuzi wa kielimu juu ya hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…