Nachanganyikiwa-msaada wenu wa haraka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Wakuu naomba kuelewa kidogo mambo haya, nahisi kuchanganyikiwa
1. Kwanini Mwakalebela amepigwa chini na CCM, wakati Mramba ameachwa? Wote wanatuhuma zinazofanana na za Mramba huenda zikawa nzito zaidi
2. Kwanini Selelii hakupitishwa wakati alikua mshindi wa pili, na badala yake akapitishwa mshindi wa Tatu? Selelii ana matatizo gani?
3. Kwa nini hawa wote, walioshindwa kwenye kura za maoni wasitafute nyia mbadala wa kugombea kama nia ni kuwakilisha wananchi na kuwatumikia?
Nitashukuru kwa majibu yenu
 
mkuu,
1. Mwakalebela ni mtoto wa ''mama wa kambo'' hana haki mbele ya watoto wa mama mkubwa hata kama ni watovu wa nidhamu. Mwakal. hayupo katika inner circle, na katika vikao vya familia hana mwakilishi. Lazima utambue kuwa ndani ya CC au NEC kuna formula ya kulindana.Kwa maneno machache unyonge ndio uliomtoa kafara. Mchicha unaochipua si sawa na mbuyu wa miaka nenda rudi.
2. Selelii alikuwa mwiba ndani ya bunge,kwa hiyo njama zote za kumuondoa zilifanyika, kwa bahati mbaya Bashe anaonekana kuwa ana matatizo mengi kuliko ya uraia kama tunavyoaminishwa. Nyimbo ya kuwa alimzidi Selelii kwa kura nyingi ni siasa za kijinga maana alimshinda Kigwangala zaidi kuliko Selelii. Hapa lengo lilikuwa kumoundoa Selelii hata kama upinzani ungefanikiwa. Umesahau Kitwana alivyotoswa Kigamboni kwa gharama za upinzani!
3. Njia mbadala ipo lakini muda umekwisha. Selelii hakuhitaji mwalimu alitakiwa amfuate mpendazoe kujitoa mapema. Lakini wote wanaamini kuwa mafanikio yapo kwa kubebwa na CCM. Ni kosa la selelii mwemyewe, na Mwakalebela bado ana nafasi akijawa na ujasiri.
Selelii ni mpiganaji wa dhati atumie nafasi hii kuwaunga mkono wakombozi kama marando hata kama ubunge haupo. Mapambano yana uwanja mpana, achukue maamuzi ya haraka na magumu.
 
Wakuu naomba kuelewa kidogo mambo haya, nahisi kuchanganyikiwa
1. Kwanini Mwakalebela amepigwa chini na CCM, wakati Mramba ameachwa? Wote wanatuhuma zinazofanana na za Mramba huenda zikawa nzito zaidi
2. Kwanini Selelii hakupitishwa wakati alikua mshindi wa pili, na badala yake akapitishwa mshindi wa Tatu? Selelii ana matatizo gani?
3. Kwa nini hawa wote, walioshindwa kwenye kura za maoni wasitafute nyia mbadala wa kugombea kama nia ni kuwakilisha wananchi na kuwatumikia?
Nitashukuru kwa majibu yenu

Aisee maswali magumu haya!
 
CCM ina wenyewe, na wenyewe ni akina Mramba. Siyo akina Selelii na Mwakalebela!
 
Back
Top Bottom