Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,543
Wanabodi,
Karibu, Nipashe ya leo
Uwajibikaji Screen shot.png

Kufuatia Watanzania wengi kuwa ni waumini wa dini kuu mbili, Ukristo na Uislamu, hivyo sii wengi wanaijua "karma" ni nini, kwasababu "karma" ni neno la lugha ya ki Hindi "Hindu" na linafundishwa kwenye dini ya Hinduism na Buddhism, mimi nilijifunza kuhusu "karma" wakati nikiishi jiji la New Delhi nchini India.

Huu ni wito kwa viongozi wetu, unapokosea hata kwa kujikwaa tuu ulimi, tujenge tabia ya kuwajibika kwa makosa yetu, tujitokeze kuomba radhi, na ikibidi kuwajibika!.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastory story, na sii watu wote ni wapenda mastory, wengine ni wavivu tuu wa kusoma vitu virefu, wanapenda vitu vifupi short and clear, wengine ni just wako too busy hawana muda kusoma vitu virefu, ili kuwatendea haki nisiwachoshe wengine, hii mada nimeikata vipande vipande with sub headings, ili wewe usome only what will interest you!, kwa kusoma kile tuu utakachokuwa na interest nacho.

Tuanze kwa Kuijua Karma, ni Nini na Inafanyaje Kazi
anzia hapa

Kuijua karma "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!
Karma ni kanuni ya binadamu kulipwa kwa kadri ya matendo yako, ukitenda mema, unalipwa mema, ukitenda maovu unalipwa maovu. Malipo ya karma ni hapa hapa duniani. Adhabu kubwa kuliko zote ya karma ni kifo.

Ukimtendea mtu jambo baya, hilo jambo likimuumiza, akiumia moyo, kama hukumtendea haki, wewe uliyetenda, litakufika jambo baya ambalo litakuumiza kufidia maumivu uliomsababishia mwenzio.
Karma Kwenye Uongozi wa Umma
Njoo hapa Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!
Kwenye uongozi wa umma, moja ya jambo zuri na la furaha, ni mtu kuteuliwa kwenye nafasi ya wadhifa wa uongozi, iwe ni kwa kuchaguliwa au kuteuliwa, na kinacholeta raha ya kweli, sio malipo ya mshahara mnono na marupurupu, wengine vikiwepo vingora, msafara, na vieite (V8), bali ni ule tuu utumishi wa umma wa kuwatumikia watu.

Vivyo hivyo moja ya vitu vinavyoleta huzuni hadi mtu kupata msongo wa mawazo, ni pale kiongozi wa umma unapotumbuliwa kwa fedheha baada ya kuharibu!. Kutumbuliwa ni kutumbuliwa tuu, hata kama ulikuwepo kwenye uteuzi, kisha rais akafanya mabadiliko ya uongozi, kwenye safu mpya jina lako likawa halipo, maana yake wewe umeachwa, kuachwa sio kutumbuliwa, ila kwenye macho ya jamii lazima itakuona wewe hufai ndio maana umeachwa, hivyo utahesabika umetumbuliwa!.

Ukiachwa lazima utajiuliza kosa lako ni lipi?, usipoona kosa la sababu ya wewe kuachwa, utaumia roho, ukiumia roho kama hukutumbuliwa kwa haki, hukumu ya karma itamhusu mtumbuaji. Hivyo kwa viongozi wetu wa umma, pale unapofanya kosa lolote, la kustahili kutumbuliwa, hata kujikwaa tuu ulimi, usisubiri mpaka rais akutumbue, tujenge utamaduni wa kukubali kosa na kuwajibika kwa kujiuzulu kama alivyofanya Spika, na sio kusuburi kutumbuliwa au kuwekwa pembeni kama walioachwa jana!.

Ukijiuzulu mwenyewe, hata ukiumia vipi, hakuna adhabu ya karma kwa aliyekuteua, lakini ukitumbuliwa, ukiumia, kama hukutumbuliwa kwa haki, unambebesha mzigo wa karma Mhe, Rais wetu, bila wewe kujijua na bila yeye kujijua!, hii mizigo ya karma iki accumulates vya kutosha, inasababisha mapigo ya karma!, matomeo ya mwisho ya mapigo ya karma ni ... (naomba nisitaje), hivyo huu ni wito kwa viongozi wote wa umma, ukiharibu, usisubiri kutumbuliwa na kumbebesha mzigo wa karma Mama yetu Rais Samia, wajibikeni kwa kujiuzulu ili kumuepushia kumbebesha Rais Samia mzigo wa karma zisizo mhusu, maana hizi karma, zinadunduliza, zikifika za kutosha kustahili adhabu ya karma, ndio unasikia... mara ghafla,... mara hivi, mara vile, karma inapo hit back, ina hit bila kujali nani ni nani!.

Japo uhai umeumbwa na Mungu, na kifo pia kimeumbwa na ni kazi ya Mungu, lakini kwa waumini wa karma, aina ya kifo, na muda wa kifo, pia unahusishwa na malipo ya karma ama adhabu ya karma. Kwa vile sisi binadamu hakuna yoyote anayejua sababu za Mungu kumtwaa mja wake yoyote au mtu yoyote duniani na jinsi alivyomtwaa, inawezekana kabisa ni karma ya matendo yake ya wazi na sirini, kwa vile tumeishapoteza viongozi wetu wengi kwa kuitwa na Mungu, hakuna ajuaye sababu za wengine kuitwa na wengine kuachwa, hivyo hakuna guarantee ya kuzuia kiongozi yoyote asiitwe, lakini tukiweza kuwaelimisha viongozi wetu kuhusu karma, na umuhimu wa kutenda mema na kutenda haki, tunaweza kuwaepusha na mengi, na labda waliotangulia wangeijua karma na kuishi kwa mujibu wa kanuni za karma, labda ungekuta tuko nao hadi leo!.

Ni ukweli usiofichika kuwa kwenye taifa letu kuna tatizo la uongo, uzushi, fitna na majungu, hivyo ikitokea kiongozi amepigwa zegwe na kuzushiwa uongo, uzushi fitna na majungu, akatumbuliwa, karma itamuhusu mtumbuzi, hivyo hata ukisikia sikia tuu fununu, fungasha pisha, maisha ni popote sio lazima kwenye uteuzi tuu!.
My True Story ya Kuzushiwa, Uongo, Fitna na Majungu na Karma Yake.
TBC ilipoanzishwa enzi hizo TVT, mimi nikiwa na Diploma tuu ya Uandishi wa habari kutoka TSJ, ni miongoni mwa waanzilishi, sifa za kuajiriwa TVT ni shahada ya kwanza ya chuo kikuu. Wakati wetu, kiwango cha juu cha fani ya uandishi wa habari kwa Tanzania ndio ilikuwa Diploma, ila Watanzania waliosoma nje, ndio walikuwa na degree na masters. Pale TVT mwaka huo wa 2000, mimi na diploma yangu na uzoefu wangu wa utangazaji wa miaka 10, sio sawa na mwenye masters na uzoefu sifuri. Hivyo pale TVT mimi nilikuwa boss fulani kwa level ya pale nikiitwa PP1, (principal producer I) juu yangu kulikuwa na PM na top wetu ni Mkuu wa Idara. Hivyo kwa cheo changu, ilibaki nafasi moja tuu kuwa mkuu wa idara yaani mkurugenzi.

Sikuaminigi kuwa serikali kuna uongo, uzushi, fitna na majungu, ila nilipigwa jungu, enzi hizo TVT iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kuna msamaria mwema mmoja akanitonya kuwa kule wizarani kuna barua yenye tuhuma nzito dhidi yangu inazunguka!, hivyo soon nitang'olewa!. Kiukweli sikufanya chochote kwasababu mimi siamini zengwe, majungu wala fitna!.

Kweli siku ya siku, tena mimi ndio nimepangwa kusoma habari siku hiyo, nikiwa kwenye kikao cha idara, mara nikaitwa kutoka nje ya kikao, ndio nikakutana na mesenja wa Confidencial Registry na briefcase nyeusi, ameandamana na FFU wawili, wameshika bunduki standby as if mimi ni terrorist, huyo jamaa anaitwa jina la utani la Isirael, ndio huwa anasambaza barua za watu kupunguzwa kazini. Basi nikapewa barua yangu, na kusaini despatch kuwa nimepokea, kuifungua, niliishiwa nguvu!, nimepigwa "summary dismissal kwa kosa la insubordination!".

Yule Siraeli akarudi nyuma FFU na mitutu yao huku wamenielekezea, ingia ndani kusanya kilicho chako, tunakusindikiza mpaka getini. Kiukweli niliishiwa nguvu, kumbuka ofisini kwangu ndio kuna kikao na niko na watumishi wote wa idara!. Kuna mfanyakazi mwenzangu mdada akanisaidia nikafungasha na kubeba box langu la personal effects na kusindikizwa hadi getini!. Mimi nilikuwa boss na gari na dereva, lakini siku hiyo niliondoka kwa miguu!. Nikiwa getini, nikamuona dereva wangu na gari anakuja, nikasimama nikijua ndio anakuja kunirudisha home, dereva kufika akaniambia amepangiwa kazi nyingine!, Ilibidi kutembea hadi barabarani kutafuta usafiri, hata sikumbuki nilifikaje home, ila kufika nyumbani ni moja kwa moja kujifungia chumbani na kuanza kulia kwa kutoamini kilichonikuta!.

Siku hiyo sikulala ni mawazo na machozi usiku kucha!. Asubuhi nikaamua sikubali, nikaelekea ofisi ya Waziri Mkuu, nikamuona KM, kiukweli aliniangalia tuu!. Nikajiondokea nimenyongonyea huku nimekuwa mdogo kama piriton!. Nikaenda Utumishi kuomba Standing Orders, kwanza nikagomewa eti zinatolewa kwa maofisa utumishi tuu!, nilipoeleza kisa changu, nikapewa na kuambia soma urudishe. Nikaangalia sheria, taratibu na kanuni, kiukweli zote zimekiukwa!, Kwa vile mimi ni mtu well connected, kwa njia zangu ninazozijua nikachimba kilichotokea, kiukweli ilikuwa ni uongo, uzushi, fitna na majungu!. Hivyo hivi vitu vipo sana serikalini na kwenye chama chetu pia vipo!.
Karma Yangu, Karma Yao!.
Baada ya kutimuliwa kazi TVT, ndipo nikaenda shule UDSM kusomea fani nyingine kabisa ili niachane na uandishi wa habari na utangazaji!. Wale walionitenda, kila mmoja yalimkuta ya kwake, ila nikijifanyia tathmini ya life yangu ilivyo sasa na kama ningeendelea kuwa TBC, kiukweli majanga mengine ni a blessing in disguise!. Mwinyi alijiuzulu uwaziri tuu wa mambo ya ndani, akaja kuwa rais wa JMT!, hivyo kuna waliotemwa jana, Uspika au Uwaziri tuu, kumbe urais unawasubiri!. Japo kwa CCM, tayari tunaye mgombea wetu wa 2025 ila ... Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! ila pia kuna hii sauti kuhusu 2025, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke, japo mambo ya voices from within, sio mambo ya kuzingatia sana, ila pia sio mambo ya kupuuzia!.

Kujiuzulu Kwa Spika Kama ni Kwa Haki, Ni Uwajibikaji, Kama Ameonewa Karma Itamfidia.
Hata kujiuzulu kwa Spika, yale matamshi yake ni hoja ya msingi sana, ule alio ongea ni ukweli mtupualipoharibu ni kuomba msamaha batili kwa jambo la kweli alilolisema!, angejiuzule ile siku anaomba msamaha, angejiuzulu kwa heshima na kuonekana shujaa, lakini hii ya kujiuzulu baada ya kudhalilishwa kwa stress za 2025!, kiukweli amejizulu shingo upande kwa shinikizo, ila kama ni kweli alikuwa kwenye kundi hilo, na walioachwa wote ni adhabu ya kuwazia 2025, then Mama ni haki yake, lakini kama kuna uongo, uzushi fitna na majungu, karma itaingilia kati, hivyo tukiweza kumuepushia Mama na maamuzi yanye karma repercussions, tutakuwa tunamsaidia sana Mama yetu asilimbikize bad karma!

Kwa kadri ya siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika kizazi cha sasa, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni new generation ya utawala wa Mwinyi, Mkapa, JK, na JPM, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu, walipofanya makosa ya wazi, sio tuu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika, hivyo nauliza, kwa viongozi wetu hawa wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa, au makosa ya kujikwaa kisiasa, jee tuwaache waombe tuu msamaha na maisha kuendelea kwa “life as usual”, au sasa tujenge utamaduni wa viongozi wetu, wanapofanya makosa, hata kupishana tuu kauli na mkuu wanchi, kuwajibika kwa makosa yao, na wasiishie kuomba tuu msamaha, tena misamaha mingine ni misamaha batili, mtu unafanya kosa la wazi, badala ya kuomba tuu msamaha na kusema ulighafilika, wewe unaanza kwanza kwa kutoa visingizio, vya eti nilinukuliwa vibaya!, au nimebambikiwa maneno hayo, ndipo unaomba samahani!, tena msamaha wa Kikatoliki wa "ninekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana!".

Ili kujenga nidhamu ya kweli ya uwajibikaji, pale kiongozi anapokosa, asiishie kuomba msamaha tuu, bali msamaha huo uandamane na barua ya kuwajibika, kama enzi za Nyerere.
Uwajibikaji Enzi za Nyerere, Mwinyi Kujiuzulu na Kisa cha Mzee Mayalla (RIP)
Mfano mzuri wa ombi la msamaha likiandamana na uwajibikaji, ni kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi kufuatia vifo vya mahabusu wakiwa mikononi mwa polisi, vilivyotokea mwaka 1976 mkoani Mwanza na Shinyanga, ambapo mwaka 1977, Waziri Mwinyi aliandika barua kwa rais, Mwalimu Nyerere ya kuomba msamaha na kuwajibika.

Tena kwenye kadhia hiyo, haikuishia kwa kwa Mwinyi pekee kwa kujiuzulu, bali Rashidi Kawawa aliondolewa kwenye umakamo wa pili wa rais. Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa alijiuzulu. Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Emelio Mzena alistaafishwa, IGP, Samuel Pundugu alistaafishwa, Kamisha Mkuu wa Magereza alistaafishwa. Kisha moto huo ikahamia Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Peter Kisumo, alimwaga unga. RPC, RSO, OCD na DSO wa Mwanza sio tuu walimwaga unga, kwa kustaafishwa kwa manufaa ya umma, mimi nikiwa ni mtoto wa mmoja wa maofisa hao, Marehemu Baba, Mzee Andrew Mayalla, (RIP), sio tuu unastaafishwa na kuamua kuishi popote, bali unastaafishwa na kufuatwa usiku usiku kusafirishwa kurudishwa kijijini kwenu kwa Landrover 109 za enzi hizo na baba kukabidhiwa kwa serikali ya kijiji, huruhusiwi kutoka nje ya kijiji bila ruhusa!.

Mtu ulikuwa ni mtoto wa bosi, ukipelekwa shule kwa gari la kazini kwa bosi, mara ghafla mnarudishwa kijijini kuwa mwanakijiji wa kijiji cha ujamaa, na haikuishia hapo maofisa hao walifikishwa mahakamani kwenye ile “Kesi ya Mauaji Mwanza” Tena maofisa wa baadhi ya idara za serikali wa enzi hizo, mimi mpaka niko darasa la nne, ndio nakuja kujua Mzee Mayalla alikuwa nani, tena kwa kusoma kwenye gazeti la Mzalendo, lakini maofisa wa siku hizi, wanatambia nafasi zao hadi kugombea mabibi bar, ukimshinda, unaonyeshwa yeye ni nani!. Maofisa na wote walihukumiwa vifungo virefu, isipokuwa mshitakiwa mmoja tuu, Mzee Mayalla, yeye ndiye pekee alikutwa hana hatia nadhani ni kwa sababu alikuwa anatetewa na wakili mahiri, Murtaza Lakha, ndie aliemuokoa.
Huu uwajibikaji wa enzi za Mwalimu, umepotelea wapi?. Mahabusu wangapi siku hizi wanakufa mikononi mwa polisi na hakuna uchunguzi wowote wala hatua zozote zinazochukuliwa, na hakuna mtu yeyote anayewajibika?!

Msamaha wa Spika JYN Ulikuwa ni Msamaha Batili, Kajiuzulu Shingo Upande Kwa Shinikizo!
Hivi majuzi Mkuu wa Mhimili wa Bunge ametofautiana na Rais katika jambo la kweli na la msingi kabisa, kuhusu mikopo na deni la taifa. Kiongozi huyu badala ya kusimama kwenye hoja yake na kujiuzulu kwa heshima kwa kutofautiana na bosi wake, yeye akaamua, sio kuandika barua ya kuomba msamaha, bali kuita waandishi na Bunge kulipia matangazo ya moja kwa moja na kuomba msamaha live kwenye TV, kwa nini pia asingetangaza kujiuzulu kwa heshima?.

Muombaji msamaha badala ya kukiri tuu kosa, akatafuta visingizio vya uongo, na hivyo kuufanya msamaha wake kuwa ni msamaha batilifu Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu!
bila ubatilifu kuondolewa, ukawa ni msamaha batili na ukakataliwa, hivyo ndio kulazimika kujiuzulu kwa aibu na fedheha!.

Tena ule msamaha batili haukuishia kwenye msamaha tuu, hata taarifa kwa vyombo vya habari, kuhusu kujiuzulu, kunaonyesha barua ya kujiuzulu imeandikwa kwa Katibu Mkuu wa CCM nakala kwa Bunge, badala ya kwa Katibu wa Bunge nakala kwa CCM!, Hii ni barua batili ya kujiuzulu, na Bunge letu lilivyo la ajabu, limekubali nakala ya barua hiyo batili na kutangaza limeipokea!. Kama katiba imeelekeza jinsi ya kujiuzulu Spika na utaratibu, kwanini ifanyike batili na kuruhusiwa na chombo cha juu kama Bunge letu?. Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge? baadae Bunge lilirrkrbishs ubatili huo na tukalipongeza Serikali inapokosolewa kwa Constructive Criticism, je, Ifuate Ushauri? Hongera Bunge letu tukufu kufuata ushauri na kutuondolea ubatili huu
Kwenye Hotuba ya Rais, Kuna Kiongozi Ametajwa, Anasubiri Nini?
Kwenye hutuba ya rais Samia, kuna kiongozi mwingine ametajwa kujihusisha na harakati za urais wa 2025, tufike mahali viongozi wetu wa kisiasa wawe na viwango vya uadilifu vya mke wa Kaizari, hata ukituhumiwa tuu hata kama sii kweli, ile kutuhumiwa tuu, unakaa pembeni, halafu kama sii kweli, sii utaitwa tena?.

Samia alipoingia, tulimshauri kiongozi mmoja mkubwa tuu ajiuzulu ili kumpa Samia fursa ya kuisuka timu yake, halafu kama bado anahitajika, si atateuliwa tena?. Sasa jina la kiongozi huyo limetajwa tena!, Rais Samia kasema hivi karibuni atafanya panga pangua nyingine, hivi huyu kiongozi anasubiri nini mpaka sasa kuwajibika na kupisha?, ili kumpa mama fursa ya kuunda timu yake?. Kama bado anahitajika, si ataitwa tena?.
Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Sio Wote Walioachwa ni Wametumbuliwa, Wengine Ni...
Jana kumefanywa mabadiliko ya baraza la mawaziri, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu. Mabadiliko ni kitu cha kawaida, lakini kwa vile Mama alisema atafanya mabadiliko na kuwapumzisha wale wa 2025 ili kuwapa muda wa kutosha kushughulikia 2025, kutapelekea kila aliyeachwa kuonekana ni ametumbuliwa, wale ambao ni kweli ni 2025 stress, hata wakiumia, hawana karma repercussions, lakini wale waliosingiziwa na wakatumbuliwa kwa uonevu, karma yao itambebesha mzigo wa bure Mama yetu!.
Rais Mama Samia Sio Malaika, Naye Ni Binaadamu, Hivyo Anaweza Kukosea, Tumsaidie!
Angalia hapa Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Hitimisho
Ni lini uwajibikaji kwa viongozi wa umma utarejeshwa kwa kiwango cha uwajibikaji wa enzi za Mwalimu?. Yaani kiwango cha uadilifu wa mke wa Kaisari?. Kiongozi wa umma ni mpaka afanye kosa kubwa kiasi gani ndipo awajibike?.
Wito kwa Viongozi Wetu
Viongozi wetu, cheo ni dhamana, ikitokea ukatuhumiwa tuu, tuhuma za wazi, hata bila uthibitisho, ama kanusha ama wajibika, hata mkapishana tuu kauli na mamlaka yako ya uteuzi, ukiona tuu hamko wamoja, jikalie pembeni, usisubiri kuwekwa pembeni!, msimponze bure mama yetu Samia kwa kumtwisha mzigo wa karma zenu, kama mlivyomponza yule mwingine na karma ikafanya mambo yake!.

Ukibebwa kwa mbeleko bebeka kwa kujiachia, lakini ikitokea mbeleko iliyokubeba imelegea, sasa wewe lazima ujibebe mwenyewe, danda na kushikilia kwa nguvu zako zote ili usianguke, na ikitokea wewe umeishiwa nguvu huwezi kushikilia tena, achia mwenyewe udondoke taratibu usiumie, hiyo maana yake ni umefikia kiwango chako cha mwisho cha kubebeka hivyo sasa wewe ni zigo, lisilobebeka tena, ni busara kuachia mwenyewe usipoachia, utabwagwa chini kama zigo na utaumia!, ukiumia karma inamrudia aliyekuumiza!, hivyo kujijutia kwako na maumivu ya kubwebwa, mtatuponzea bure na huyu!, wajibikeni wenyewe msituponzee bure Mama yetu kwa mi karma yenu!.

Safari bado ni ndefu.
Jumapili njema.
Wasalaam,

Paskali.
 
Sasa karma ya nini kama uamuzi aliochukua Rais hauna tatizo?

Unapomuonea mtu kwa sababu amehoji jambo lenye maslahi kwa taifa hiyo karma kama ipo lazima ikutafune tu, au kumtumbua yeyote kwasababu ameonesha dalili za kuutaka urais kama wewe pia itakutafuna tu.

Hakuna sababu ya mtoa hoja kujiuzulu bila kosa kisa ametofautiana na mkubwa wake.
 
Kwa nchi yetu somo la UWAJIBIKAJI kwa viongozi bado halieleweki.

Sababu kubwa ni ukosefu wa Uzalendo/uadilifu.

Baadhi ya Viongozi wetu wamejawa na Uchu na tamaa ya kujinufaisha wao wenyewe.

DHAMIRA yao kuu ni kujilimbikizia mali sio kuwatumikia wananchi, ndio maana huwa inakuwa vigumu sana kwao kuwajibika/kuachia madaraka maana hufikiria kuwa atapoteza/watapoteza manufaa yake/yao sio ya wananchi.

Ndio maana ktk nchi za Afrika Uongozi/Madraka hutafutwa kwa udi na uvumba, rushwa na ikibidi hata kumwaga damu yote hayo sio kwa uchungu wa kuwatumikia Wananchi bali kujinufaisha wao!

sasa kama viongozi wanapatikana kwa njia hizo...wanawezaje kuelewa somo la uwajibikaji?!!
Bado tunasafari ndefu ya kutengeneza viongozi wazalendo/waadilifu.
 
Sikuaminigi kuwa serikali kuna uongo, uzushi, fitna na majungu, ila nilipigwa jungu, Enzi hizo TVT iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kuna msamaria mwema akanitonya kuwa kule wizarani kuna barua yenye tuhuma nzito kunihusu inazunguka, hivyo nitang'olewa. Sikufanya chochote kwasababu mimi siamini zengwe, majungu wala fitna.

Kweli siku ya siku, tena mimi ndio nimapangwa kusoma habari siku hiyo, nikiwa kwenye kikao cha idara, mara nikaitwa kutoka nje ya kikao, ndio nikakutana na mesenja wa Confidencial Registry na briefcase nyeusi, ameandamana na FFU wawili, wameshika bunduki standby as if mimi ni terrorist, huyo jamaa anaitwa jina la utani la Isirael, ndio huwa anasambaza barua za watu kupunguzwa kazini. Basi nikapewa barua yangu, na kusaini despatch kuwa nimepokea, kuifungua, niliishiwa nguvu!, nimepigwa "summary dismissal kwa kosa la insubordination!".

Yule Siraeli akarudi nyuma FFU na mimitu yao huku wamenielekezea, ingia ndani kusanya kilicho chako, tunakusindikiza mpaka getini. Kiukweli niliishiwa nguvu, kumbuka ofisini kwangu ndio kuna kika na niko na watumishi
 
Sasa karma ya nini kama uamuzi aliochukua Rais hauna tatizo?

Unapomuonea mtu kwa sababu amehoji jambo lenye maslahi kwa taifa hiyo karma kama ipo lazima ikutafune tu, au kumtumbua yeyote kwasababu ameonesha dalili za kuutaka urais kama wewe pia itakutafuna tu.

Hakuna sababu ya mtoa hoja kujiuzulu bila kosa kisa ametofautiana na mkubwa wake.
We jamaa bhana...

Yaani Mwigulu Nchemba anaingia bungeni na mkoba kwa ajili ya kusoma bajeti huku Ndugai na wenzake wakimpigia shangwe kama lote!!

Nchemba anaeleza mambo kadhaa, na kwa muktadha huu ana-highlight vyanzo mbalimbali vya mapato kwa ajili ya kugharamia bajeti husika!!

Wakati akiendelea kusoma, hatimae anafikia hapa:-
Loans 2.png

Hapo sijataja mikopo ya kibiashara!! Mwisho wa hotuba, Mwigulu anatoa hoja na kuliomba bunge lipitishe bajeti hiyo!!

Baada ya hapo, majadiliano fake yanaanza, and finally, Ndugai anawauliza wenzake: "Wanaosema Ndiyo?"

Wabunge: "NDIYOOOOOOOOOOOOOOO"

Kisha Ndugai anatoa kila kicheko chake halafu tena anauliza "Wanaosema siyo?"

Wabunge wawili watatu wanajibu "siyo"!

Ndugai tena, kwa mbwembwe, tambo na majivuno anasema "Waliosema NDIYO wameshinda"!

Na kama kungekuwa na wapinzani, anaanza kuwakejeli huku akisifia "bajeti bora kuliko zote kuwahi kutokea!!"

Unajua tafsiri ya hiyo "NDIYOOOOOOOOOO"

Manake ni kwamba Ndugai na wenzake, pamoja na mambo mengine pia wanamruhusu Samia na timu yake akiwemo Mwigulu Nchemba, wakakope!!

Miezi michache baadae, Ndugai yule yule anatoka tena hadharani na kukejeli kile kile ambacho taasisi anayoiongoza iliidhinisha tena kwa shangwe kubwa, halafu unasema "ameonewa"?

Hivi unajua maana ya collective responsibility?
 
Pole sana Mkuu Paskali.
huwa nasoma hicho kisa chako cha kufukuzwa kazini kwa ajili ya Majungu na fitina naumia sana.

kwani tabia hizo hadi leo hii bado zipo sana, kuna watumishi makini na waadilifu wanaumizwa na fitina na majungu na hawana wa kuwatetea.

kisa chako kinafaa kiwe somo na fundisho.
viongozi mlio pewa madaraka tendeni Haki kwa walio chini yenu vinginevyo tegemeeni kuangamizwa na nguvu ya Mungu.
 
Kuna wanaosema Ndugai katumia njia sahihi sababu Bunge bado halijaanza...

Kuna wewe unayesena kakosea kui address chamani, angei address bungeni...

Au angesubiri mpaka Bunge lianze ndiyo ajiuzuru....

Which is which?
 
Tujikumbushe kidogo wakati impunity ilipokuwa inaishi na kutawala Tanzania😁😁😁
 
Kuna wanaosema Ndugai katumia njia sahihi sababu Bunge bado halijaanza...

Kuna wewe unayesena kakosea kui address chamani, angei address bungeni...

Au angesubiri mpaka Bunge lianze ndiyo ajiuzuru....

Which is which?
Anyway ila kwa Ndugai hata kama amelazimishwa kujiuuzulu, hata kama taratibu hazikufuatwa kikatiba, tuunge mkono tu kilichotokea kwa kuwa UFEDHULI aliofanya una madhara kuliko hizo taratibu za kumtoa. The end justifies the means
 
Wanabodi,
Karibu, Nipashe ya leo
View attachment 2074235
Kufuatia Watanzania wengi kuwa ni waumini wa dini kuu mbili, Ukristo na Uislamu, hivyo sii wengi wanaijua "karma" ni nini, kwasababu "karma" ni neno la lugha ya ki Hindi "Hindu" na linafundishwa kwenye dini ya Hinduism na Buddhism, mimi nilijifunza kuhusu "karma" wakati nikiishi jiji la New Delhi nchini India.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastory story, ili nisiwachoshe wale wavivu wa kusoma story ndefu, nitaikakata kata hii mada ili wewe usome kile tuu utakachokuwa na interest nacho.
Ili kuijua Karma, kwanza karibu mitaa hii

Karma Kwenye Uongozi wa Umma

My True Story ya Kuzushiwa, Uongo, Fitna na Majungu na Karma Yake.

Karma Yangu, Karma Yao!.

Baada ya kutimuliwa kazi TVT, ndipo nikaenda shule UDSM kusomea fani nyingine kabisa ili niachane na uandishi wa habari. Wale walionitenda, kila mmoja yalimkuta ya kwake, ila nikijifanyia tathmini ya life yangu ilivyo sasa na kama ningeendelea kuwa TBC, kiukweli majanga mengine ni a blessing in disguise!. Mwinyi alijiuzulu akaja kuwa rais wa JMT, hivyo kuna waliotemwa jana, Uspika au Uwazi Mkuu au hata urais unawasubiri. Japo kwa CCM, tayari tunaye mgombea wetu wa 2025 ila ...

Kujiuzulu Kwa Spika Kama ni Kwa Haki, Ni Uwajibikaji, Kama Ameonewa Karma Itamfidia.

Uwajibikaji Enzi za Nyerere, Mwinyi Kujiuzulu na Kisa cha Baba Yangu Mzee Mayalla (RIP)


Huu uwajibikaji wa enzi za Mwalimu, umepotelea wapi?. Mahabusu wangapi siku hizi wanakufa mikononi mwa polisi na hakuna uchunguzi wowote wala mtu yeyote anayewajibika?.

Msamaha wa Spika JYD Ulikuwa ni Msamaha Batili, Kajiuzulu Shingo Upande Kwa Shinikizo

Kwenye Hotuba ya Rais, Kuna Kiongozi Ametajwa, Anasubiri Nini?

Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Sio Wote Walioachwa ni Wametumbuliwa, Wengine Ni...

Rais Mama Samia Sio Malaika, Naye Ni Binaadamu, Hivyo Anaweza Kukosea, Tumsaidie!


Hitimisho
Ni lini uwajibikaji kwa viongozi wa umma utarejeshwa kwa kiwango cha uwajibikaji wa enzi za Mwalimu?. Kiongozi wa umma ni mpaka afanya kosa kubwa kiasi gani ndio awajibike?.

Viongozi wetu, cheo ni dhamana, mkiweza wala msipishane kauli, ukiona tuu hamko wamoja, jikalie pembeni, msimponze mama yetu Samia kwa kumtwisha mzigo wa karma, ukifikia kiwango cha kutosha kutobebeka, mtatuponzea tena!.

Safari bado ni ndefu.
Jumapili njema.
Wasalaam,

Paskali.
Pole sana bro kisa cha Baba yako I hope kimekujenga kwenye ustahimilivu kimaisha. Siku hizi kika kitu ni fake kwanzia nafsi ya Rais hadi sisi mmoja mmoja na pia pengine kiwango cha udikteta na umwinyi kimepungua.
 
Back
Top Bottom