tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,427
- 28,473
Kuna haja ya serikali kumchunguza nabii Titto kama inavyomchunguza Askofu Kakobe ili kubaini kama pombe anazokunywa hadharani kila kukicha anazinunua kwa fedha za sadaka au ana chanzo kingine cha kipato. Pia nitoe wito kwa TRA kuchunguza vyanzo vyote vya mapato vya nabii huyu ijiridhishe kama analipa kodi stahiki serikalini.
Pamoja na hayo, naishauri serikali imdhibiti Titto asiharibu kizazi cha watanzania kwa mahaubiri yake tata na yasiyozingatia biblia. Mungu hadhihakiwi. Siku zote serikali imekuwa mstari wa mbele kukemea udhalilishaji wa kijinsia, kuzuia maambukizi ya VVU na kuzuia mimba za utotoni. Lakini, ama kwa makusudi au kwa kutokujua, huyu nabii amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha uvunjaji wa sheria, huku akijua fika anaenda kinyume na sheria za nchi na mafundisho ya dini.
Katika siku za hivi karibuni Nabii Titto ameonekana akihamasisha watu kunywa pombe. Unywaji wa pombe ni kinyume na azma ya serikali ya kupunguza ajali za barabarani kwani ajali nyingi husababishwa na madereva walevi pale wanaposhindwa kufanya maamuzi sahihi wanapokuwa barabarani. Juzi tumeshuhudia ajali iliyoua ndugu zetu 11 papo kwa papo na huenda dereva alikuwa amelewa. Mtu yeyote anayewahamasisha watu kunywa pombe ni wa kumuogopa kama ukoma.
Aidha, nabii huyu amekuwa akiwahamasisha akina baba kutembea na kuzaa na wajakazi (house maids) wao. Ili kusisitiza azma yake hiyo, amekuwa siku zote akitangaza kutembea na mjakazi wake na amekuwa akitamba hadharani. Kitendo cha kutembea na mjakazi sio tu kinaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa ya ngono na VVU, bali kinadhalilisha wanawake – kwamba wao ni viburudisho vya mabosi wao sehemu za kazi. Hapa haki za binadamu zimevunjwa. Mjakazi anayo haki ya kufanya kazi kwa uhuru pasipokuwa na wasiwasi wa kuingiliwa kimwili na “baba”. Kwa kweli, hili suala halijakaa sawa mbele za watetezi wa haki za wanawake.
Kana kwamba hilo halitoshi, nabii Titto amekuwa akivaa hereni masikioni mwake na kucheza nyimbo za taarabu, jambo linalohusishwa na ushoga. Kwa maana nyingine ni kwamba anatangaza vitendo vya kishoga hapa nchini. Vitendo, vya ushoga sio tu ni chukizo kwa serikali ila ni dhambi kubwa kwa Mungu.
Kufuatia matukio haya na mengine mengi ambayo nabii Titto amekuwa akijihusisha nayo, serikali haijakaa kimya. Juzi nimeongea na mtaalamu mmoja wa masuala ya kijamii akanitonya kwamba serikali inamsaka nabii Titto ili imfikisha katika vyombo vya sheria kwani vitendo vya uvunjivu wa maadili anavyofanya ni zaidi ya ugaidi.
Naungana na watanzania wazalendo kwa kukemea vitendo hivi na ninaipongeza serikali kwa hatua zake za kumuwajibisha nabii Titto ili liwe fundisho kwa wachochezi wengine wanaovunja sheria za nchi kwa makusudi. Najua kuna wafuasi wa nabii Titto wapo humu na wasingependa kuona nabii wao akitiwa msukosuko na serikali kwa namna yoyote ile. Tulizeni munkari. Sheria za nchi hazina dini. Ndio maana hadi sasa hivi polisi wanamhoji Askofu Kakobe kwa kuvunja sheria za nchi. Sheria ni msumeno.
Habari zaidi soma=>Polisi Dodoma: Daktari toka hospitali ya Milembe athibitisha kuwa nabii Tito ana tatizo la akili