Kama utahisi masihara basi we hisi hivyo, ila me ndo nimeamua hivyo,
Nimefaulu vizuri ila shule nimeshindwa kwenda kwa hali ngumu, napambana na maisha lakini mwangaza siuoni, sina mbele wala nyuma, wachawi kila siku wananiwinda ili kunirudisha nyuma
Mama yangu ananipenda ila hana maisha na ana hali ngumu huku akinitegemea pamoja na mdogo wangu,
Baba yangu hana msaada na mimi na pia hana chochote, kiukweli nahisi nilizaliwa KIMAKOSA TU
sioni haja ya kuishi
Usijiue bado kuna tumaini,na ushahidi ni huu
Ulizaliwa uchi,je hadi sasa unaandika haya bado upo uchi?
kama umevaa nguo hata kama zimechanika,jiulize ulizipata wapi?
Na kama una nafasi ya kupata computa au simu janja kupost uzi huu
wewe una nafuu kuliko wapambanaji wengine.usijiue.
Nenda hospitali yoyote uangalie wanaosotea afya zao hata kama wana pesa,wanahangaika kwa maumivu
usiku na mchana wanapambana kumshinda adui mauti,wewe mwenye afya
unataka kujipeleka mdomoni mwa mauti bila gharama?
Usikufuru ndugu yangu maadamu una afya njema, Mungu anakupenda.Fanya chochote atakibariki
Usikate tamaa,usijiue,ipo kesho yako ambapo utauona ukuu wa Mungu.
Ikatae roho ya mauti,mkaribie Mungu naye atakukaribia