Naamini lengo la CCM ni zuri lakini hili la kuteua wagombea siku moja kabla ya uchaguzi linafikirisha

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Kidumu Chama cha mapinduzi,

Pongezi na hongera kwa kila mmoja aliyefanikisha uchaguzi wa Chama na jumuiya kwa ngazi zote. Mmefanikisha kuitekeleza demokrasia kwa vitendo.

Kesho tarehe 07/12/2022 Chama kinakwenda kuhitimisha uchaguzi kwa kuchagua viongozi wakuu wa chama na wajumbe wa NEC Taifa.

Katika hili sina wasiwasi na mashaka na uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wenyeviti kwa sababu kwa utamaduni wa Chama wagombea wa nafasi hizi wanafahamika.

Mashaka yangu yapo kwenye uchaguzi wa nafasi za NEC. Kwanza, wagombea wa nafasi hizo wanatarajiwa kutoka mikoa ya mbali na Dodoma kwa maana hiyo walitakiwa kupewa taarifa mapema ya uteuzi wao ili kujiandaa na safari sasa mpaka Leo siku moja kabla ya uchaguzi hawana taarifa ,je watajiandaaje na safari?

Pia mpaka kufikia muda huu jioni hii hakuna majina yaliyotoka ya walioteuliwa lakini tunaona tayari kuna wagombea kama Nape Nnauye na Shaka Hamdu Shaka wameanza kujinadi ,je taarifa wametoa wapi?

Je, kwa vile shaka ni moja wapo wa wahusika wa vikao vya mchujo amejua kinachoendelea je wale wasio wajumbe wa vikao wategemee nini?

Ninaamini kufanyika uteuzi wa wagombea siku moja kabla Chama kina makusudi yake lakini naomba Chama itazame upya huu utaratibu maana unamnyima mtu fursa na kushindwa kuhudhuria kutokana na umbali wa maeneo wagombea wanayotoka.

Nakitakia uchaguzi na mkutano mkuu mwema wa 10 Chama cha Mapinduzi
 
Hili la kushtukiza ni katika harakati za kuepuka kuchafuana na kutengeneza mitandao, kudhibiti rushwa na makundi.
 
Chama chakavu kimemteua Dr Hangaya kugombea nafasi ya uenyekiti kidumu chama chakavu

"Fikra huru huletwa na mijadala huru"
 
CCM inanuka Rushwa mpaka iajiogopa harufu yake yenyewe.

Hii pia ni mbinu ya walamba Asali kutotaka wajumbe kupata muda wa kuwajadili.

Rushwa....Rushwa.....Rushwa!
 
Back
Top Bottom