General Stalin
JF-Expert Member
- Mar 6, 2014
- 652
- 501
Ubinadamu kazi wakuu,
Vitendo ninavyopata toka kwa ninaowasaidia kutoka ni vya kukatisha tamaa kwa kweli.
Huyu ni mtu wa nne sasa; anahitaji ajira unampa shavu anakua na life lake lakini akishatoa matongotongo tu anaanza visa vyake.Unaonekana mjinga na mshamba tu.
Yeye ndio anajua kila kitu anajifanya kama hakujui vile kumbe wewe ndio umempa hiyo nafasi.Sasa hata nikiona nafasi mahali bora nikae kimya tu maana napata dharau toka wema wangu.
Wakuu binadamu watu hatari mno,nimekuja jua maana kama ingekua ni huyu tu nisingekua na wazo tofauti ila huyu ni wa nne kwahiyo hii ndio tabia halisi ta binadamu kwamba akishatoka anasahau kua kuna jamaa walihenyeka kumpa support mpaka kufikia hapo alipo.
Watu wabaya
hilo sawa kabisa japo sio wote, nakumbuka kuna mtu hivyohivyo japo uwezo nimemzidi sana kuna siku after 1 year nikampigia as a friend hakupokea hata simu, siku nyingine nikakutana naye akawa na haraka ila psycholocally nikamsoma nkamwambia napenda tu tukapate kinywaji wengine ndo hivyo nshawasahau kabisa.
all in all lengo nikupata company tu ya kupiga story weekend but ndo hivo na wapo wanaoshukuru ila huwa nawaambia hicho kidogo wasaidie wasiojiweza mtaani kwako au peleka kanisani!!!!