Naacha kazi serikalini

Big up mkuu nimekupata vyema. Je unahisi nitakuwa sahihi pesa yote ya mkopo kuingiza kwenye biashara moja.
Kabisa ingiza yote humo,wala usijali. Utairudisha vizuri tu. Hiyo kwanza itakufanya kujituma kwa ajili ya hilo duka,akili zote utawekeza hapo. (Kumbuka wakati unajituma kwa ajili ya hilo duka,ndio unatengeneza brand yako iwe kubwa na wateja pia).Isitoshe itakufanya ujue hela ya mkopo iko wapi,kuliko ukaiweka huku na kule kwenye biashara isiyo na uhakika 100%. Ni kosa kubwa kuingiza hela ya mkopo kwenye biashara isiyo na uhakika 100%. Namaanisha mahindi huna uhakika kama hayatashuka au hayatazuiliwa kutoka nje ya nchi. Hilo duka unalifahamu tayari. Namaanisha unajua unajua linaingizaje hela,linatembeaje,linaendeleaje. Hizo biashara zingine bado hujui,una bahatisha tu. NASISITIZA TENA MUDA MWINGI MALIZIA HAPO DUKANI,NGUVU KUBWA IWE HAPO. HAPO NDIO MAHALA PAKO PA KUTOKEA,NIAMINI. ACHA HIZO TAMAA ZINGINE ZA BIASHARA ZINGINE,KABLA HUJAIFIKISHA MAHALA PAKE HIYO
 
Big up mkuu nimekupata vyema. Je unahisi nitakuwa sahihi pesa yote ya mkopo kuingiza kwenye biashara moja.
Fumba macho na masikio kabisa. Usisikie wanaokuambia biashara fulani inalipa na hii inalipa. Hiyo itakufanya uyumbe sana. Stick sehemu moja kwenye biashara unayoifahamu. Halafu kumalizia ningependa unakuwepo wewe mwenyewe dukani. Kazini piga vipindi,ukipata mwanya wa kutoroka we torokea dukani tu. Hata wakikufukuza usijali. Duka kama kuna wateja kwa siku si chini ya laki,hapo si pabaya,pataongezeka,wewe watengeneze hao wateja zaidi
 
Mkuu hata mimi nataka niache kazi ila sio leo wala kesho

Sitaki kukurupuka nakushauri mkuu , kwanza ji set vzur sna
 
H
Nimesoma ushauri wa wadau kwa huyu ndugu yetu, binafsi nadhani huu wa ndugu Daud1990 ndiyo mujaarabu sana. Bonge la ushauri. Huu ukopi kabisa mahali kwa marejeo. Haya maisha kwa kweli saa ingine tunakuwa kama watumwa. Mishahara haikutani kamwe!! Le us think outside the box kwakweli.
 
swali ambao hawajaajiriwa wanaishio vipi, unajua shule hizi zinatupoteza sana mtu akisoma anataka aishi maisha ya juu sana kwa mantiki hiyo kujitegemea ni ngumu. tufike mahali tujifunze kuishi maisha ya kawaida huku unatafuta zaidi.

Biashara na usupastaa haviendani labda ubaki huko huko kwenye ajira, mtu ukitaka kujitegemea lazima ujitoe haswa na kukana nafsi yako.
 
Jamaa ana tamaa wakati kaduka kafinyu,anatakiwa apambane na duka angalau lifikie mtaji wa 25.Ndio anaweza kutoa angalau 3milioni kuanzisha mradi mwingine.Sasa kwa tamaa hizo akianza kufirisika ataanza kuwalaumu madogo wa dukani kuwa wanamuibia.Halafu kaduka hakohako anataka kukapeleka shambani kakalime na mtaji finyu.Biashara unatakiwa ujipe muda hata wa miaka 5 ndio utaona range ya mafanikio.Nakumbuka kuna mwanajf humu alijipa miaka 5 ya kufa na kupona ya kudeal na biashara yake,yaani faida anaiwekeza kwa kununua bidhaa mpya huku akiachana na anasa zote.Na Leo anaenjoy life
 
Lazima uwe Against mkuu. tuna sumbuliwa na Fear of Uknown?
Tuna hofioa vitu visivyo kuwepo, hizi ni fear mbaya mno kuziondoa sio mchezo.
Ni kweli mkuu, japo point yangu ya msingi ni kuwa lazima awe involved in the process ya kuondoa huo uoga na kujivika ujasiriamali. And there's no way around it.
 
Wengi wanaharibu biashara zao kwa mtindo huo wa kuwa na tamaa. Anaanza kukuharibu kulikomtoa badala ya kukuendeleza
 
Una mtaji kias gan mkuu?
 
Hapo unatakiwa kuongeza fani au kiwango cha elimu kabla ya kuacha hiyo kazi. Au acha kazia baada ya kupata nyingine, kama inahitaji fani nyingine, fanya kama nilivyosema mwanzo.
 
Sawa mkuu ila wengi tunashindwa kujiwekea mtaji kutokana na kazi tunazo fanya
 
Mkuu wenzako wanaacha kazi wakiwa tiyari wana mitaji mizuri ama tiyari wame shafungua njia nyingine za vyanzo vya mapato we umejipangaje.

Pasi ndefu utaziweza mkuu? Siku ukikosa mkate. Maana kama ukiacha na ukiwa huna shughuli mtaani si lelema mkuu.
Mambo ya kushindia mkate wiki nzima... daah jamaa ataitesa familia yake namwonea huruma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…