Naacha kazi serikalini

Big up mkuu nimekupata vyema. Je unahisi nitakuwa sahihi pesa yote ya mkopo kuingiza kwenye biashara moja.
Kabisa ingiza yote humo,wala usijali. Utairudisha vizuri tu. Hiyo kwanza itakufanya kujituma kwa ajili ya hilo duka,akili zote utawekeza hapo. (Kumbuka wakati unajituma kwa ajili ya hilo duka,ndio unatengeneza brand yako iwe kubwa na wateja pia).Isitoshe itakufanya ujue hela ya mkopo iko wapi,kuliko ukaiweka huku na kule kwenye biashara isiyo na uhakika 100%. Ni kosa kubwa kuingiza hela ya mkopo kwenye biashara isiyo na uhakika 100%. Namaanisha mahindi huna uhakika kama hayatashuka au hayatazuiliwa kutoka nje ya nchi. Hilo duka unalifahamu tayari. Namaanisha unajua unajua linaingizaje hela,linatembeaje,linaendeleaje. Hizo biashara zingine bado hujui,una bahatisha tu. NASISITIZA TENA MUDA MWINGI MALIZIA HAPO DUKANI,NGUVU KUBWA IWE HAPO. HAPO NDIO MAHALA PAKO PA KUTOKEA,NIAMINI. ACHA HIZO TAMAA ZINGINE ZA BIASHARA ZINGINE,KABLA HUJAIFIKISHA MAHALA PAKE HIYO
 
Big up mkuu nimekupata vyema. Je unahisi nitakuwa sahihi pesa yote ya mkopo kuingiza kwenye biashara moja.
Fumba macho na masikio kabisa. Usisikie wanaokuambia biashara fulani inalipa na hii inalipa. Hiyo itakufanya uyumbe sana. Stick sehemu moja kwenye biashara unayoifahamu. Halafu kumalizia ningependa unakuwepo wewe mwenyewe dukani. Kazini piga vipindi,ukipata mwanya wa kutoroka we torokea dukani tu. Hata wakikufukuza usijali. Duka kama kuna wateja kwa siku si chini ya laki,hapo si pabaya,pataongezeka,wewe watengeneze hao wateja zaidi
 
Mkuu hata mimi nataka niache kazi ila sio leo wala kesho

Sitaki kukurupuka nakushauri mkuu , kwanza ji set vzur sna
 
H
Mkuu Sauti uisikiayo kutoka nafsi yako ndio usahihi wako...


Mara zote public opinions za mambo yasioyo na ukawaida huwa ni negative .. Kwa maana kuwa haijazoeleka kuona mtu akiacha kazi na kufanya issues zake ... Tegemea kukutana na vitisho na kuvunjwa moyo..



Ila amini nakwambia kuajiriwa ni utumwa na hautakuja kuishi maisha ya ndoto yako kwa kuajiriwa. Utaishia saaaaNa kuishi maisha MAZURI na sio BORA.

Maisha Bora ni kuwa free na familia yako , kupata muda Wa kuumzika etc..



Ushauri wangu ni Sikiliza nafsi yako... Hakuna anaejua hali yako .. Wewe ndio unajijua Gap lako la maisha likoje kuwa kama ukiacha kazi utalifill vipi na kwa muda gani ...


Nakuomba utafute shughuli ya kufanya kabla ha kuacha kazi atleast miezi sita kabla ya kuacha kazi ... Katika kipindi hicho fanya Reformations za unavyoishi ili uanze kuadapt utakavyoishi kwa kujiajiri.. Kama ulikuwa kwa mwezi unatumia 200,000 kwa matumizi ya nyumbani jitahidi upunguze ..


Nunua friji uwe unanunua vifaa vyote kwa mwezi , gharama isiwe hiyo 200,000... Kama ulikuwa unakaa katikati ya mji na unalipa kodi kubwa , jitahidi uhamie nje ya mji kuna nyumba nzuri sana kwa bei nafuu sana na unaweza kupata hata sehemu kubwa ya kuanzisha mradi Wa ufugani Kuku na mayai ...


KwA ufupi nifanyie self assessment yako halafu njoo na Work plan yako ...



Amini nakwambia utapitia uchungu kwa kipindi kifupi ila utamu wake utakuwa Wa muda mrefu kuliko walioajiliwa ambao wanakuona hujielewi ..



Please Follow Where Your Heart Tells You To Follow.
Nimesoma ushauri wa wadau kwa huyu ndugu yetu, binafsi nadhani huu wa ndugu Daud1990 ndiyo mujaarabu sana. Bonge la ushauri. Huu ukopi kabisa mahali kwa marejeo. Haya maisha kwa kweli saa ingine tunakuwa kama watumwa. Mishahara haikutani kamwe!! Le us think outside the box kwakweli.
 
Kuajiriwa ni hatua ya kawaida kwa wanao tafuta mtaji

Kupata mtaji ni moja ya njia ya kuanzisha mradi mpya utako kupa kipato cha ziada

Kuacha kazi ni baada ya kuona mradi wa pili umesimama imara una uwezo wa kujiendesha na kubakiza kichache cha kukusaidia kulea familia

Kama umeanza mradi mpya bado hauja fikia hatua ya kujiendesha basi jiwekee muda maalum kwa ajili ya kuuwezesha mradi kujiendesha na kubakiwa na akiba kwaajili ya wewe kutumia na familia

Wengi tunahisi tunaweza kujitegemea kirahisi ila mazingira ya nje na ajira yana changamoto ambazo utajikuata umekuwa kama kituko kwa jamii na kufanya walio nyuma yako wakudharau zaidi ya ulivyo kuwa na kazi
swali ambao hawajaajiriwa wanaishio vipi, unajua shule hizi zinatupoteza sana mtu akisoma anataka aishi maisha ya juu sana kwa mantiki hiyo kujitegemea ni ngumu. tufike mahali tujifunze kuishi maisha ya kawaida huku unatafuta zaidi.

Biashara na usupastaa haviendani labda ubaki huko huko kwenye ajira, mtu ukitaka kujitegemea lazima ujitoe haswa na kukana nafsi yako.
 
Sawa nimekuelewa. Ninachokikataa mimi ni huko kujikopesha kwenda kufanyia kazi zingine,wakati duka bado linahitaji liongezewe hela. (Labda mpaka utakaponiambia limejitosheleza). Yaani kujitosheleza kwa maana ya vifaa vilivyopo dukani,uwe na kama hivyo tena stool. Na hapo kila bidhaa itakayokosekana dukani usiwe na wasiwasi wa kuiagiza. Sio tena bidhaa haipo dukani,halafu ni muhimu,huku hela umejikopesha imekaa kwenye mahindi. Nakuhakikishia hivyo vyote utavifanya mbele,ila jitosheleze kwanza kwenye duka. Usiwe na tamaa ya kufanya vitu vingi utakwama mahala. Niamini. Deal na kitu kimoja kwanza. Hivyo vyote vitakuja tu mbele. Halafu umesema vijana dukani. Muda mwingi wewe uwe unakuwepo. Hesabu zote endesha wewe,agiza mzigo wote wewe. Usilidharau hilo duka kama una wateja. Wewe ndio utawakimbiza wateja kwa kukosa bidhaa muhimu,baada ya kujikopesha hela ya dukani
Jamaa ana tamaa wakati kaduka kafinyu,anatakiwa apambane na duka angalau lifikie mtaji wa 25.Ndio anaweza kutoa angalau 3milioni kuanzisha mradi mwingine.Sasa kwa tamaa hizo akianza kufirisika ataanza kuwalaumu madogo wa dukani kuwa wanamuibia.Halafu kaduka hakohako anataka kukapeleka shambani kakalime na mtaji finyu.Biashara unatakiwa ujipe muda hata wa miaka 5 ndio utaona range ya mafanikio.Nakumbuka kuna mwanajf humu alijipa miaka 5 ya kufa na kupona ya kudeal na biashara yake,yaani faida anaiwekeza kwa kununua bidhaa mpya huku akiachana na anasa zote.Na Leo anaenjoy life
 
Jamaa ana tamaa wakati kaduka kafinyu,anatakiwa apambane na duka angalau lifikie mtaji wa 25.Ndio anaweza kutoa angalau 3milioni kuanzisha mradi mwingine.Sasa kwa tamaa hizo akianza kufirisika ataanza kuwalaumu madogo wa dukani kuwa wanamuibia.Halafu kaduka hakohako anataka kukapeleka shambani kakalime na mtaji finyu.Biashara unatakiwa ujipe muda hata wa miaka 5 ndio utaona range ya mafanikio.Nakumbuka kuna mwanajf humu alijipa miaka 5 ya kufa na kupona ya kudeal na biashara yake,yaani faida anaiwekeza kwa kununua bidhaa mpya huku akiachana na anasa zote.Na Leo anaenjoy life
Wengi wanaharibu biashara zao kwa mtindo huo wa kuwa na tamaa. Anaanza kukuharibu kulikomtoa badala ya kukuendeleza
 
Habari wakuu wote wa jf
nawapenda sana hasa kwa mambo mazur nnayopata
Mmi ni mtumishi wa serikali kada ya elimu (mwl)

Sababu hasa ni hizi
1.interest au hob
Kiukweli hii kazi siipendi niliisomea bada ya kuwa sina otenative najitaidi niikubali but inashindikana so naona kama napoteza muda

2.kipato
Najua kuwa watumishi weng hasa awamu hii ya 5 weng wanalalamika hali ya uchumi but mmi naona hii yangu ni too much

Kiukweli najitahidi sana kujibana ila naona nashindwa, nashindwa kufanya hata mambo ya kawaida tu nikiwa kama baba natamani familiar yangu angalau iishi standard hata kias tu but huku nliko naona kama ndoto
Yan labda uwe mzee wa topup jambo ambalo naona pia ntaongeza ufukara mana ukiisha ndo utataabika kama nnavyoona wengine

Lengo la uzi huu ci kuwatangazia msimamo wangu bali ni kuwaomba wale ambao walishachukua maamuzi kama yangu au wanaotarajia hivyo waendlee kunipa moyo pia wote ambao watakua na wasaa basi wanisaidie kimawazo nifkie lengo langu

Naomba kuwaslisha

NB: Pls nmejitaidi kutumia lugha nzuri naomba bro o sister kama unanishaur bas lugha iwe ya kunielewesha isiwe ya kebehi au kunitusi kwan kuyaheshimu maamuzi ya mtu ni jambo la busara
Una mtaji kias gan mkuu?
 
Hapo unatakiwa kuongeza fani au kiwango cha elimu kabla ya kuacha hiyo kazi. Au acha kazia baada ya kupata nyingine, kama inahitaji fani nyingine, fanya kama nilivyosema mwanzo.
 
swali ambao hawajaajiriwa wanaishio vipi, unajua shule hizi zinatupoteza sana mtu akisoma anataka aishi maisha ya juu sana kwa mantiki hiyo kujitegemea ni ngumu. tufike mahali tujifunze kuishi maisha ya kawaida huku unatafuta zaidi.

Biashara na usupastaa haviendani labda ubaki huko huko kwenye ajira, mtu ukitaka kujitegemea lazima ujitoe haswa na kukana nafsi yako.
Sawa mkuu ila wengi tunashindwa kujiwekea mtaji kutokana na kazi tunazo fanya
 
Mkuu wenzako wanaacha kazi wakiwa tiyari wana mitaji mizuri ama tiyari wame shafungua njia nyingine za vyanzo vya mapato we umejipangaje.

Pasi ndefu utaziweza mkuu? Siku ukikosa mkate. Maana kama ukiacha na ukiwa huna shughuli mtaani si lelema mkuu.
Mambo ya kushindia mkate wiki nzima... daah jamaa ataitesa familia yake namwonea huruma
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom