Naacha kazi serikalini

Kidogo nna experience ya ujasiria mali coz hata wakati naenda kweny ajiara nlitoka kwenye biashara ambayo nlishaiona inaangalau afadhali ya Maisha so nataka nirudi kulekule
Na hili ndo kosa kubwa mnalolifanya watu wenye elimu kichwani huku akili mkiwa mmeiaminisha kwamba hakuna mafanikio kama hujaajiriwa na hapa ndipo hasa msingi wa majuto yako ulipo,kusoma siyo lazima kuajiriwa elimu ni kupata maarifa mapya na kuongeza ujuzi wa kile ambacho unahisi hukijui vizuri ili ukijue na ukifanye kwa usahihi zaidi.

Acha kazi ukiwa na angalao nusu ya mtaji wa biashara uliyoukiifanya mwanzo kuwa na uzoefu siyo issue uzoefu mwenzake mtaji mtaani kuna show moja la kibabe sana linaendelea tulioko huku tuna-survive kiuzoefu tu wewe uliyekuwa unahesabu siku ukisubiri laki kadhaa na refer maneno yako hapo juu wewe ni baba wa familia ukiingia kichwa kichwa utapagawa tuliza akili kwanza.
 
Maamuzi yako yanaweza kuwa na maana kama una blue print ya unakoelekea, vinginevyo kuacha kazi itakuwa maamuzi mabaya zaidi kuliko hata yale ya kuuchagua ualimu.

Sasa kabla hujaacha ualimu fanya kitu kimoja kwanza.
Anza kusave kiasi katika mshahara wako kuanzia sasa. Alafu ndani ya miezi mitatu uanzishe jambo ambalo linazalisha hela. Jitahidi mwaka huu mzima utengeneze misingi mizuri ya hiyo biashara yako. Kuanzia mwaka kesho uanze kusave hela ya kukusaidia kuishi angalau miezi 6 bila kutegemea biashara yako.

Kumbuka biashara ni too risky. You can loss money and find yourself regretting why you left a job. So in that way a backup plan will help you to continue building with less pressure.

Anza kuexperience maisha ya uraiani ukiwa job kwanza. Itwkusaidia.

Usijaribu kina cha mto usioujua kwa miguu yote
 
Hapo unatakiwa kuongeza fani au kiwango cha elimu kabla ya kuacha hiyo kazi. Au acha kazia baada ya kupata nyingine, kama inahitaji fani nyingine, fanya kama nilivyosema mwanzo.
Huu ushauri nimeuchukua mimi.
 
Usituchagulie cha kuongea wala kukushauri...kila mtu ana ubongo wake.

Km unataka kutiwa moyo na kuchangiwa hoja we tulia pokea michango ya wachangiaji.....

Kitu kibaya na kizuri vyoote vina faida katika maisha yako, watakaokuvunja moyo watakupa mzuka wa kupambana zaidi ili kuwathibitishia kuwa inawezekana... Na watakaokutia moyo pia watakuongezea nguvu ya kupambana zaid.


Tusichaguliane cha kuongea.
 
Usiache kazi kama una mke na watoto...ila Acha hiyo kazi kama bado uko peke ako.

Unapoajiriwa hamna faida yoyote lakini si kwamba kweli hamna faida Zipo faida japo si za kukuvusha kukufikisha malengo yako.

Chakufanya kama mkeo nae kaajiriwa Acha kazi..ila kama mkeo kajiajiri basi muimarishie biashara mkeo hakika utaona matunda ya hiki ninachokushauri.

Ukiwa na mke ni vyema mmoja akaajiriwa na mwingine akawa mfanyabiashara...Huyu alie ajiriwa hela zake zote ni za kuimarisha biashara ya mwenzake...so anaefanya biashara ndio Provider wa kila kitu nyumbani.

Usitegemee mshahara kukutimizia mahitaji ya nyumbani kama una familia HAUTOSHIIIIII...so hakikisha huachi kazi kabla ya kujua mkeo ana nini cha kufanya.

Mnapokua mke na mume sishauri wote muwe wafanya biashara...wala sishauri wote muajiriwe Hamto enjoy maisha ukitaka mu enjoy na mle pepo hapa duniani Mmoja aajiriwe mwingine awe mfanyabiashara.

Kuajiriwa uhakika wa income mwisho wa mwezi ni 100% ila biashara uhakika ni Probability so Mfanyabiashara unahitaji sana mke/mume alieajiriwa ili upate ile flow ya hela kila mwezi wakati wewe hiki kdg kinachopatkana kwenye biashara ndio kinasukuma familia.

Kilio chako ni toafaut na aliyejiajiri maana yake ukifanya biashara hata ukose hela vipi huwezi lia/lalamika na kufikia hali mbaya kama yako mkuu so Jigawe na mkeo kisha ANZA UPYA.
 
Nashukuru sana mkuu kwa ushauri wako.Nitaufanyia kazi.
Ubarikiwe 🙏🙏🙏🙏🙏
 
Acha kazi mara moja, roho yako inayo kuongoza haiwezi kukupoteza, nilifanya huko kazi lakini mafanikio niiyapata kwa rushwa tu, tena rushwa ndefu, bila rushwa mshahara wao hautoshi, tena wanakubana sana kila asubuhi uko kazini, hata muda wa kufikiri huna, kariakoo unaisahau. sasa ningeishije kwa wizi ?mpaka lini? nikayakoroga yasije nikuta

Ujue hao wanaopata raha serikalini wana ma-godfather wao wana tanua sana, au kama unaweza ujipendekeze sana kiasi cha kujidhalilisha, na kufanyiwa ya hovyo,

Wale wenye godfather wanapewa semina na mishahra ina panda kama kawa, wanapanda madaraja, wanapewa nafasi nzuri hata wa chini yako anawezakuwa na mshahara mkubwa kuliko wewe ilimradi tu ana godfather. wakiona umemenunua gari, umejenga umeenda kusoma, wanakuzushia tu ili uhame au

wanakukatia mshahara kwa muda usojulikana bila sababau ilimradi tu utumie resources zako zote,

kwa kufidia pengo la mshahra, utafuatilia mpaka miguu iote kutu, na usisubili hayo yakukute ondoka mara moja, huko serikalini imejaa misukule mitupu, yana visukari, ma high BP, ni shida sana huko. labda magufuli ayaondoe kwa sasa.

Top layer ya serikalini itakupenda Kama unaishi kwa shida shida sana, huna mpango wa kwenda kujiendeleza (kusoma), mfano mlevi, teja( mlandukaji), mgonjwa wa ukimwi, hapo hutoki, lkn eti kijana una afya yako mjanja unadundulize hela yako unapojua mwenyewe, ujenge nyumba gari weeee! utaona kila rangi ya fitina.

Navyo kuona wewe tayari ni mjanja, umeshtuka ka mshahara kadogo, ina maana utatengeneza vyanzo vingine vya pesa, wakikujua tu tegemea hayo hapo juu, Yaani wanaweza lengesha rushwa tu, kuna mawili godfather akutose, au aendelee kukuunga mkono hivohivo, akihamishwa umeumia.
UKIKAA KAA KI MAGUTU SANA ISIVO KAWAIDA. yangu ni hayo!

kila la kheri!
 
Hahah kauli za kishujaa hizi zitakuja mponza mtu walahi...
Sisi tusiokuwa kwenye ajira za serikali mbona tushazoeaga kupambana, halafu kitaa mbona mi napaona pa kawaida tu.
Sijui watu wanachokiogopa ni nn
wasomi wanakiogopa kitaa kinoma unajua wengi wamekulia shule, kitaa hawakielewi kabisa so kurudi huko ni stress tupu.
 
Mkuu hujui ni kwa kiasi gani umenitia moyo. Mimi ni mwajiriwa and kiapo changu kilikuwa nilazima nopate wife mchakarikaji. Nimefanikiwa kumpata dada ambaye ni mpampanaji na anayajua maisha, ana some little knowledge kwenye kada ya afya so tumefungua duka la Dawa mhimu one of the busness ambayo ukijipanga vizuri ina faida Sana. The problem mama hataki kukubaliana kabisa na maamuzi yangu anataka nitafute msomi wa level yake tene from a rich family, Mimi nimekaza kwa sababu i see prosperity ndani ya huyu dada. Ukiacha upambanaji ni wife material, a pure African wife material. Mkuu umenipa moyo sana ujue kwa kile ninachokifanya na ambacho na amini nisahihi kwangu!
 
Kuomba ushauri wa kuacha kazi kwa watu ambao wameajiriwa ni kupoteza muda tu,hawatakuwa na la maana kukushauri zaidi ya kukujaza uoga na mwisho wa siku hutaacha hiyo kazi na ndoto zako zitapotea.Fanya kile moyo wako unapenda,usifanye kile waajiriwa wanapenda!....Nimemaliza
 
Wakati wengine wakifunga na kuomba wapewe ajira serikalini kuna wengine wanataka kuacha!

Maisha hayako sawa kabisaaa!!

Jaribu kuangalia wa nyuma yako Mkuu, hali walizonazo halafu mshukuru Mungu kwa ulichonacho!

Hujachelewa bado! Jipange, hakikisha unaishi maisha ambayo yapo chini ya kipato chako, weka akiba kila mwezi, kuwa na malengo ambayo unatamani uyafikie kwa hiyo akiba! ..

Ukishafanikiwa hilo unaweza sasa kujipanga kuacha kazi!
 
unayo plan B tayari?
 
Kidogo nna experience ya ujasiria mali coz hata wakati naenda kweny ajiara nlitoka kwenye biashara ambayo nlishaiona inaangalau afadhali ya Maisha so nataka nairudi kulekule
Usache kazi na pia biashara huku ukiendelea na kazi yako pia
 
Naona mnataka mpige hela zake. Acheni utapeli nyie.
Utapeli gani? Kama wewe huwezi kufanya waache wenzio wachukue fursa. Utapeli uko kwenye nini? toa ushahidi wa utapeli
 
By the way ni wazo zuri, maana inaonyesha ni kiasi gani una umiza kichwa chako kurich your target.

But ni vema ukaandaa vizuri kabisa alternative way ya kuelekea, before ujatoka hapo ulipo....

All in all napenda kukutakia kila la kheri chief....may God bless you.

Welcome.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…