Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Habari za kuaminika zinasema kuwa gazeti la Rai Mwema linatarajiwa kumuomba Radhi Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz kufuatia makala iliyotoka kwenye gazeti hilo wiki chache zilizopita.
Bw. Rostam alitoa tishio la kuchukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti hilo wakati ule ule alipotoa tishio la kushtaki gazeti la MwanaHalisi. Hata hivyo, wachunguzi wa mambo mbalimbali wamegawanyika kama uamuzi wa kumuomba radhi ni sahihi au wangesubiri aende mahakamani kwanza.
Bw. Rosam anadai kuwa aliandikwa vibaya na kuchafuliwa hadhi na heshima yake na gazeti hilo katika makala iliyoandikwa na Bw. Joseph Mihangwa toleo la April 2 na maendelezo yake kwenye April 9.
Hata hivyo, Bw. Rostam hakuchachamalia makala iliyoandikwa na Lula wa Ndali Mwananzela yenye kichwa cha habari "Sipendi Rostam atisike Kiberiti Bungeni". Makala hiyo ilijibiwa wiki moja baadaye na mtu ajiitaye "Joseph Wambura" katika makala yake "Tusimdharau, Rostam hatikisi kiberiti".
Wacha tuone .Kumbe sasa MwanaHalisi ni kidume zaidi .Ulimwengu kaogopa nini ? Wacha kwanza tuone matendo ndipo tuanze debate hapa .
wachunguzi wa nje... sijui ndani kukoje.
Kama hawajapewa barua ya kutakiwa kuomba msamaha na Rostam, ni vema wakachapisha kwa hiari yao usasahihi sehemu anayolalamikia na kuomba radhi kwa kukosea kuchapisha, bila kusubiri kulazimishwa kuomba msamaha kama wanajua hilo kosa lao. Then baada ya hapo wammng'ang'anie kidhani kumwandika Rostam na deal zake mpaka wamnyake tena sawasawa.
____________________________
Wakipata wakili mzuri kama Lissu wanaweza kuamua kutoomba msamaha na kuigeuza hii kesi kuwa ya RA badala ya Raia Mwema na ushahidi uko belele na wanaweza kuwaita wajumbe wa kamati hiyo kama mashahidi wa kutetea walichoandika dhidi ya RA. Halafu wakamchokonoa ili tujue ni kipi alichotaka kusema bungeni na kamati ya CCM bungeni ikamkataza kufanya hivyo.
Hivi Lissu amewahi kushinda kesi gani kubwa? Mimi nimemsikia zaidi kwenye siasa kuliko kwenye sheria. Anyone with his data?
___________________________
Yatakushinda! Tundu Antipas Lissu ni mwanasheria wa mazingira aliyebobea anayefahamika ndani na nje ya Tanzania. Hebu google search jina lake tu utapata habari zake.
Asha
Asha,
Naona unakuwa na shida kidogo na postings zangu. Mimi nimeuliza tu swali kwa nia njema kabisa ya kujua naona wewe ukadakia kishari-shari.
Mimi ninavyojua ni kuwa Tundu ni mwanasheria wa mambo ya mazingira, maana nakumbuka alitajwa tajwa sana wakati wa kesi ya Buliyankulu. Lakini sijui kabisa kesi zake na ku-google kesi za TZ ni kumnyima mtu haki yake maana hazitakuwepo zote if at all kama zitakuwepo. Ninachotaka ni kufahamu ni kuwa, ingawa yeye amejikita zaidi kwenye mazingira, labda pia ni kibaka kwenye criminal na civil law ambayo hapa ndio inayohitajika. Ndio maana nilitaka mtu anayemfahamu vema atueleze otherwise, akina kibenea wanahitaji watu kama akina Marando n.k. I hope umenielewa na pia umeelewa kuwa kwenye sheria nako kuna ku-speshalaizi. Tuendelee na mjadala wetu kiuungwana.
___________________________