Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,695
- 40,721
Habari za kuaminika zinasema kuwa gazeti la Rai Mwema linatarajiwa kumuomba Radhi Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz kufuatia makala iliyotoka kwenye gazeti hilo wiki chache zilizopita.
Bw. Rostam alitoa tishio la kuchukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti hilo wakati ule ule alipotoa tishio la kushtaki gazeti la MwanaHalisi. Hata hivyo, wachunguzi wa mambo mbalimbali wamegawanyika kama uamuzi wa kumuomba radhi ni sahihi au wangesubiri aende mahakamani kwanza.
Bw. Rosam anadai kuwa aliandikwa vibaya na kuchafuliwa hadhi na heshima yake na gazeti hilo katika makala iliyoandikwa na Bw. Joseph Mihangwa toleo la April 2 na maendelezo yake kwenye April 9.
Hata hivyo, Bw. Rostam hakuchachamalia makala iliyoandikwa na Lula wa Ndali Mwananzela yenye kichwa cha habari "Sipendi Rostam atisike Kiberiti Bungeni". Makala hiyo ilijibiwa wiki moja baadaye na mtu ajiitaye "Joseph Wambura" katika makala yake "Tusimdharau, Rostam hatikisi kiberiti".