Mzungu angeongoza Tanzania!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Leo hii Mzungu, Mjapani, au hata Mchina na Mkorea ukimpa nafasi ya kuongoza Tanzania hataruhusu demokrasia!
Jambo la kwanza kabisa atakalo lifanya ni kusitisha kila kitu na kuongoza nchi kwa decree kwa miaka kama 50 au zaidi, ndiyo aje kuruhusu, kuna sababu kwa nini apartheid AK Wazungu walikataa Waafrika wasipige kura kuwachagulia Viongozi!

USA ilianzishwa miaka ya 1700 lkn Wanawake walianza kupiga kura mwaka 1920, Native Americans waliruhusiwa kwenye mwaka 1924 wakati Wamarekani wenye asili ya Afrika waliruhusiwa kuanza kupiga kura mwaka 1965, izingatiwe kwamba USA ili uweze kupiga kura ilikuwa ni lazima uonyeshe uwezo wakujua kusoma na kuandika lugha ya Kiingereza na reasonig jambo ambalo makundi hayo niliyoyataja hapo juu yalishindwa kuthibitisha kutokana na sababu mbali mbali! Kuna sababu kubwa sana kwa nini ilikuwa hivyo, nayo ni kwamba demokrasia inahitaji binadamu kufikia ngazi fulani ya uelewa kuweza kuimudu!

Angalia leo hii Afrika yetu ni chaos tu, misunderstanding ya demokrasia inazidi kulibomoa na kulirudisha nyuma bara la Afrika, watu wanatetea Wauza unga tena Bungeni na kujaribu kuwaadhibu na wale wanaojitokeza kupambana nao ili kuokoa jamii, wakati huo huo hawatoi njia mbadala na bora zaidi ya iliyotajwa lkn wanaikataa iliyopo ingawaje watu wetu wanaendelea kuathirika na Madawa huu ni mmoja tu wa mifano mingi ambayo inaonyesha kwamba Afrika tumeanza na demokrasia mapema sana, ilipaswa tuwe na One ruler for all!

Mpiga kura (pichani) nchini Kenya akisajiliwa (Kielektroni) ili aje kupiga kura, hivi huyu Mama anaelewa nini kuhsu Demokrasia?
1303544.jpg

Nchini AK Wabunge wa Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) wakichapana Bungeni!

eff-vs-zuma.jpg
 
Kwa decree ya konda chini ya gsm hatufiki popote, nchi itabinafsishwa.

Baba mwenye nyumba nae aache unafiki, anasema hataki wapiga dili wakati anamruhusu mwanae konda apige madili makubwa mpaka anadharau viongozi wenzake, na kunyanyasa walipa kodi wakubwa kwa faida ya gsm.

Kwa njia anazotumia watu wenye majina wote watampinga, bila kujali vyama, vita dhidi ya madawa ya kulevya isiwe sababu ya kudhalilisha watu bila ushahidi (chuki binafsi).

Angeanza kwanza kutueleza polisi wameshindwa wapi katika vita hii, ndipo aombe msaada kwa raia, sio alazimishe msaada utakaompa umaarufu. Mbona mateja wa manzese hawakamatwi na kuhukumiwa kuripoti polisi kila mwezi? (badala ya rehab).
 
Sijawahi kuona mtu mwenye mawazo na fikra za hovyo kama wewe!! Ni mtu mwenye fikra za hovyo tu ndie anaweza kuamini kubana demokrasia kwa nchi kama Tanzania kunaweza kumsaidia JPM!

Ni hii hii demokrasia ndogo tuliyonayo ndiyo ilisaidia kufahamu kwamba utawala wa JK ulijaa ufisadi kwa sababu watu walikuwa very open kueleza what's going on!

Kinyume chake, ingawaje serikali ya Mkapa ilikuwa very corrupt lakini haikufahamika hadi alipotoka madarakani kwa sababu na yeye hakuwapa watu uhuru wa kuongea!!!

Sasa kama unadhani kuminya demokrasia kutasaidia, elimika tu kwamba hiyo itasaidia kuficha maovu!

Na ukitoa nchi zenye utajiri wa asili wa kupindukia usiolingana na idadi ya watu wake, utagundua ni nchi moja tu ndiyo iliweza kufanikiwa pamoja na kuminya demokrasia... na nchi hiyo ni Cuba!

Kinyume chake, Afrika ingawaje tuna utajiri mkubwa wa asili lakini bado tumebaki maskini kwa sababu, ukosefu wa demokrasia na uhuru wa watu kuji-express, kunafanya walio madarakani maovu yao kutoonekana!

Tanzania ni linchi likubwa sana lililo na changamoto lukuki kuweza kuifikia kila mahali! Huko kwenye halmashauri hadi kesho watu wanapiga pesa! JPM na chuki zake zote dhidi ya ufisadi, asiporuhusu demokrasia ataweza kuzifikia taasisi kubwa kubwa tu zilizo Dar es salaam manake huko kwingine kunahitaji msaada wa watu wasio na hofu ya kueleza what's going on!
 
Hili suala mi naona ni mpana sana ila huwa halijadiliwi kwa kina,si wenye kuona kuwa afrika haina maendeleo kwa sababu hakuna demokrasia wala wenye kuona demokrasia ndiyo inatucheleweshea maendeleo afrika wote hawaelezi kwa kina hoja zao.
 
Demockrasia ndio imesadia kuibua uozo mwingi katika serikali kandamizi kwa wananchi wake Afrika ba dunia kwa ujumla.Na kama sio demokrasia ya vyama vingi leo hii huyo Magu wako asingekuwepo hapo juu.wamemweka kwa makusudi aje kukandamiza demokrasia.
 
Waafrika ni wanafiki na wabinafsi hawaiwezi demokrasia, Kwa hii Vita aliyoianzisha Makonda!! Ni Vita kubwa sana. Unapambana na watu usiwawajua katika ualisia, Wewe uko kwenye Mwanga wao wanakupiga toka gizani, Ni vita ngumu, ukitaka kujua ugumu wa vita hiyo angalia reaction ya Bunge ndio utajua nini kinaendelea!!!
 
Mkuu umechanganya mada tofauti kuunga uunga lakini bado hamna kitu cha maana ulichoandika EFF huko AK wanamshutumu Zuma kwa kuongoza Nchi hovyo kwa kuogopa kushtakiwa baada ya kumaliza muda wake anampigia kampeni Mke wake ili kuogopa Lamaphosa asiwe Rais..juzi katangaza wanajeshi 450 waongezwe katika viunga vya bunge ili kuimarisha ulinzi atakapokua anahutubia Taifa hizo fujo unazoziona hapo ni EFF walitaka kupinga kwa hoja Zuma asiutubie sasa Spika akaamuru walinzi wa bunge wawatoe kwa nguvu ili Zuma aje aongee sijui huko mbele iliishaje maana ilipita karibu saa nzima Zuma akuhutubia kwa ratiba iliyopangwa.
 
Sijawahi kuona mtu mwenye mawazo na fikra za hovyo kama wewe!! Ni mtu mwenye fikra za hovyo tu ndie anaweza kuamini kubana demokrasia kwa nchi kama Tanzania kunaweza kumsaidia JPM!

Ni hii hii demokrasia ndogo tuliyonayo ndiyo ilisaidia kufahamu kwamba utawala wa JK ulijaa ufisadi kwa sababu watu walikuwa very open kueleza what's going on!

Kinyume chake, ingawaje serikali ya Mkapa ilikuwa very corrupt lakini haikufahamika hadi alipotoka madarakani kwa sababu na yeye hakuwapa watu uhuru wa kuongea!!!

Sasa kama unadhani kuminya demokrasia kutasaidia, elimika tu kwamba hiyo itasaidia kuficha maovu!

Na ukitoa nchi zenye utajiri wa asili wa kupindukia usiolingana na idadi ya watu wake, utagundua ni nchi moja tu ndiyo iliweza kufanikiwa pamoja na kuminya demokrasia... na nchi hiyo ni Cuba!

Kinyume chake, Afrika ingawaje tuna utajiri mkubwa wa asili lakini bado tumebaki maskini kwa sababu, ukosefu wa demokrasia na uhuru wa watu kuji-express, kunafanya walio madarakani maovu yao kutoonekana!

Tanzania ni linchi likubwa sana lililo na changamoto lukuki kuweza kuifikia kila mahali! Huko kwenye halmashauri hadi kesho watu wanapiga pesa! JPM na chuki zake zote dhidi ya ufisadi, asiporuhusu demokrasia ataweza kuzifikia taasisi kubwa kubwa tu zilizo Dar es salaam manake huko kwingine kunahitaji msaada wa watu wasio na hofu ya kueleza what's going on!
Wewe mbona hatukuelewi????Mara serikali ya JK ilijaa ufisadi Mara serikali ya mkapa ilijaa corruption lkn hukujua hadi ilipoachia madaraka...
Mara linchi LA Tz litajiri..
Unapiga ngoma na kuicheza mwenyewe au...
 
Waafrika ni wanafiki na wabinafsi hawaiwezi demokrasia, Kwa hii Vita aliyoianzisha Makonda!! Ni Vita kubwa sana. Unapambana na watu usiwawajua katika ualisia, Wewe uko kwenye Mwanga wao wanakupiga toka gizani, Ni vita ngumu, ukitaka kujua ugumu wa vita hiyo angalia reaction ya Bunge ndio utajua nini kinaendelea!!!

Alipokosea Makonda ni kujaribu kucheza filamu na sio kupigana vita dhidi ya madawa.. Kucheza filamu na vita dhidi ya madawa ni vitu viwili tofauti kabisa.

Makonda alitakiwa akusanye ushahidi kwanza kwa kutumia vyombo nyeti vya usalama, akishajiridhisha na ushahidi upo angewakamata wote na kutupa jela bila dhamana halafu angewasongesha mahakamani huku dhamana ikiwa hamna, hapo ungesema kweli ameanzisha vita.

Huwezi kusema umeanzisha vita kwa kuwaita eti uwahoji na kuwauliza then ukawaachia, huo ni utoto na kupoteza muda tuu...
 
Bora serikali zilizopita japo mnasema.zinana ufisadi lkn hali ilikua ahuweni.serikali ya Leo haina ufisadi lkn kitumbua kimoja mia 7
 
Mpaka sasa hatujui tunataka nini wala tunafanya nini, .NO SETTINGS, NO DIRECTION.
 
Hapa kazi tu..hakuna ajira hakuna mvua hakuna kiliko....sasa tunapelekwa akili zetu kujadili Madawa ya kulevya..bora wakti uleeee serikali.ileeee ilikua ishu ya Escrow na Eppa tukahamshiwa akili zetu wa Tz kwa babu wa Loliondo
 
Mtu sahihi wa kupambana na madawa ya kulevya nchini ni;
1.Rais wa Jamhuri
2.Waziri Mkuu wa Jamhuri
3.Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Wengine ni maigizo na kupotezeana muda tu.
Mwenyewe anasema mwishoni atakuja kutangaza kuwa dar hakuna tena madaya ya kulevya.
 
Yaani kama Tanzania ikipita hii, " ili upige kura lazima uthibitishe unajua kusoma na kuandika na pia uwe na reasoning capacity ya kiwango fulani" hapo sidhani kama chama chetu kile cha CCM kitapata hata 35%..
Kwanini mnaamini ni ccm tu ndiyo wanatumia ujinga wa wananchi?
 
Wewe mbona hatukuelewi????Mara serikali ya JK ilijaa ufisadi Mara serikali ya mkapa ilijaa corruption lkn hukujua hadi ilipoachia madaraka...
Mara linchi LA Tz litajiri..
Unapiga ngoma na kuicheza mwenyewe au...
Uwezo wa kuelewa ni moja ya mambo yanayoweza kutofautisha mtu mmoja na mwingine! Be assured, you're not alone!
 
Barbarosa hiki kichaa cha kuutamani udicteta unatokana na 2015, wananchi walivyowanyima kura mpaka mkalazimika kutumia vyombo vya dola kubaki madarakani, na hivyo kuingia na mfumo wa kidicteta mkidhani mtawalazimisha watu kukipenda CCM . You are very wrong.

Nchi zote hizo mnazoenda kutembeza bakuli na zenye kupigiwa mfano zina mifumo ya kidemocrasi na mihimili iliyojitegemea isiyoingiliwa na mtu aliye hai bali katiba sheria za nchi.

Udicteta poote duniani hakuwahi kurithisha maendeleo endelevu ya kupigia mfano.
 
Mtu sahihi wa kupambana na madawa ya kulevya nchini ni;
1.Rais wa Jamhuri
2.Waziri Mkuu wa Jamhuri
3.Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Wengine ni maigizo na kupotezeana muda tu.

Mkuu wa mkoa anahusika pia kwani yeye ndiye rais katika mkoa anao tawala. Tanzania hatuhitaji demokrasi kwa sasa, tunahitaji Magufuli aendeshe nchi hii kimabavu kama afanyavyo sasa. Mbona wananchi wa nchi nyingine za Afrika zinamlilia Magufuli? Watu wamechoka na tawala za kijinga na magumashi. Angalieni Kikwete, alijifanya kaleta demokrasia....mtoto wake mwenyewe anauza unga, akapewa majina ya wauza unga awachukulie hatua, kaacha kwani alijuwa angewafichua basi na yeye angetajwa. Hii ni haki kweli kwa akili yako? It's too early for demokrasi hapa nchini. Hapa kazi tu.
 
Back
Top Bottom