Mzumbe University wanawezaje fundisha wanafunzi elfu 3 wa degree ya sheria kwa mwaka mmoja?

Kama heading ilivyo hapo juu niende moja kwa moja kwenye hoja yangu.

Kwa mwaka wa masomo uliopo sasa (2021/22) nimesoma chuo kikuu cha Mzumbe kwa kampasi ya Morogoro na Mbeya pekee walidahili wanafunzi elfu moja wa sheria kwa mwaka wa kwanza; na kwa vile wanatoa digrii ya sheria kwa miaka 3, ninakadiria kuwa kwa sasa watakuwa na angalau wanafunzi elfu 3 wa digrii ya sheria.

Hiki kitu kimenifanya nitafakari ubora wa elimu inayotolewa hapo. Je, kuna walimu wa kuwatosha hao wanafunzi wote?

Ufafanuzi ukipatikana toka kwa wadau wa MU itapendeza zaidi.
MU? Hamna kitu pale. Na kwa sababu ya uduni wa elimu inayotolewa pale, wahitimu ni mbumbumbu wa kutupwa, wakiajiriwa Wasumbufu Kwelikweli kuficha udhaifu wao. Ni sawa na wahitimu wa OUT.
Ubora wa elimu huenda sambamba na idadi ya wanafunzi ktk darasa. Darasa linakuwa na wanafunzi 3,000?!
 
Mleta thread ana point, ila watanzania hawawezi muelewa. Si kwa kozi hii ya Mzumbe tu, ni vyuo vyote na kozi karibia zote. Unaweza linganisha na vyuo vikongwe duniani kwa nyanja husika. Nadhani hii ndio huleta aina ya graduates ambao tumehitimu kwenye vyuo hivi vyetu.

Hii issue inafanana sana na uzazi wa mpango.
 
Kama heading ilivyo hapo juu niende moja kwa moja kwenye hoja yangu.

Kwa mwaka wa masomo uliopo sasa (2021/22) nimesoma chuo kikuu cha Mzumbe kwa kampasi ya Morogoro na Mbeya pekee walidahili wanafunzi elfu moja wa sheria kwa mwaka wa kwanza; na kwa vile wanatoa digrii ya sheria kwa miaka 3, ninakadiria kuwa kwa sasa watakuwa na angalau wanafunzi elfu 3 wa digrii ya sheria.

Hiki kitu kimenifanya nitafakari ubora wa elimu inayotolewa hapo. Je, kuna walimu wa kuwatosha hao wanafunzi wote?

Ufafanuzi ukipatikana toka kwa wadau wa MU itapendeza zaidi.
Ubora hapo itakuwa hakuna.
 
Kwani, Chuoni mnafatiliwa kama watoto?

Kwamba lazima uhakikishe umemsimamia mwanafunzi kaingia darasani, umsahishie daftari, umwajibishe kwa makosa yake?

Chuoni ni wewe na mambo yako. Kama miundombinu ya kutosheleza pamoja na walimu wapo wa kutosha, basi sioni tatizo.

Miaka mitatu kumbe? Nilidhani Tumaini pekee ndiyo hutumia miaka mitatu.
Niongeze Tu hapo!

Walimu wasahihishe homework kila siku, kama shule, wakague miandiko n.k
Watoe test za wiki na kusahihisha, test za mashindano ya kata, wilaya mpaka kanda!

Haaahaaahaaa!
 
Kama wewe umesoma Mzumbe kwenye level ya Chuo Kikuu usingekuja na uliyoyaleta. Binafsi naiona ni idadi ndogo sana hiyo kwa dunia ya leo.

Ukifika level ya degree utaelewa haihitajiki Mwalim kama wa shule ya msingi ambae inabidi akufundishe kusoma na kuandika.

Kinachohitajika ni Wahadhiri (lecturers) tu na "teaching assistants" kutokana na wanafunzi wenyewe. Kwa teknolojia ilivyo sasa, lecturer mmoja anaweza kuhadhiri kwawanafunzi mamilioni wa chuo kikuu waliopo hapona wasiopo hapo tena wakiwa wametapakaa dunia nzima. Mwanafunzi wa Chuo kikuu hasomeshwi bali anajisomea mwenyewe. Yeye ni kuelekezwa tu (kazi ya teaching assistants). asipoelewa. Mihadhara dnia ya leo yote huwa recorde digitally, kwa hiyo hata ukikupita unaweza kuupata muda wowote na ukausikiliza kwa muda wao.

Siku hizi madarasa kuanzia ya chekechea mpaka vyuo vikuu duniani huko, hata yanayoandikwa ubaoni yanarekodiwa yote digitally, kwa kuwa watu wameshaachana na blackboards (soiku hizi kuna smart boards) za kufundishia. Tena mashule na vyuo vingine duniani, darasa lote linarekodiwa kiukamilifu kuanzia Mwalimu mpaka wanafunzi, toka muda wa masomo unapoanza mpaka unapokwisha. Hakuna kuleteana matatizo.Kalagabaho.

Nakumbuka enzi za utawala wa Kikwetew alisisitiza sana shule zote ziwekewe umeme hata wa solar na mawasiliano yafikishe ili wanafunzi waweze kusomeshwa hata na Walimu chache sana waliobora. Nikaelewa huyu katika safari za duniani kishakumbana na shule zenye smartboards na kaelewa anawafahamisha nini Watanzania, sielewi kama watendaji walimuelewa. Ikiwa watendaji wenyewe akili zao ni kama wewe, nnashaka sana kama kuna wengi walimuelewa.
Nakumbuka wakati vyuo vinaongeza udahili wakati wa mkapa mwishoni na JK mwanzoni kuna hoja zilikuwa zinatolewa na vyuo husika kukinzana na matakwa ya wanasiasa waliokuwa wanataka udahili uongezeke maradufu. Hoja za uwiano wa wanafunzi na wahadhiri na miundombinu wezeshi ilikuwa ni hoja kuu toka kwa DVCs.
Hivyo usiseme uwiano huo na miundombinu haina mashiko.
Unajua mziki wa kufunza na kusimamia research (proposal na dissertation) kwa mwanafunzi mmoja? Saa uwe na wahadhiri 30 na wanafunzi elfu moja, mwanafunzi atafunzwa vyema kweli??
Binafsi ninakuwa na mashaka.
 
Upo kizamani zaidi. Miundombinu ya kisasa, elimu kiganjani, hivi upo dunia ipi wewe?
 
Back
Top Bottom