Mzumbe University wanawezaje fundisha wanafunzi elfu 3 wa degree ya sheria kwa mwaka mmoja?

Kama heading ilivyo hapo juu niende moja kwa moja kwenye hoja yangu.
Kwa mwaka wa masomo uliopo sasa (2021/22) nimesoma chuo kikuu cha mzumbe kwa kampasi ya Morogoro na Mbeya pekee walidahili wanafunzi elfu moja wa sheria kwa mwaka wa kwanza; na kwa vile wanatoa digrii ya sheria kwa miaka 3, ninakadiria kuwa kwa sasa watakuwa na angalau wanafunzi elfu 3 wa digrii ya sheria.
Hiki kitu kimenifanya nitafakari ubora wa elimu inayotolewa hapo. Je, kuna walimu wa kuwatosha hao wanafunzi wote?
Ufafanuzi ukipatikana toka kwa wadau wa MU itapendeza zaidi.

Nenda Mzumbe kafanye utafiti uje na takwimu sahihi hapa, mambo ya kufikiria ni upuuzi mtupu! Tuletee hapa takwimu safi!
 
Kama heading ilivyo hapo juu niende moja kwa moja kwenye hoja yangu.
Kwa mwaka wa masomo uliopo sasa (2021/22) nimesoma chuo kikuu cha mzumbe kwa kampasi ya Morogoro na Mbeya pekee walidahili wanafunzi elfu moja wa sheria kwa mwaka wa kwanza; na kwa vile wanatoa digrii ya sheria kwa miaka 3, ninakadiria kuwa kwa sasa watakuwa na angalau wanafunzi elfu 3 wa digrii ya sheria.
Hiki kitu kimenifanya nitafakari ubora wa elimu inayotolewa hapo. Je, kuna walimu wa kuwatosha hao wanafunzi wote?
Ufafanuzi ukipatikana toka kwa wadau wa MU itapendeza zaidi.

Hakuna kukadiria wala nini!
 
Kwani, Chuoni mnafatiliwa kama watoto?

Kwamba lazima uhakikishe umemsimamia mwanafunzi kaingia darasani, umsahishie daftari, umwajibishe kwa makosa yake?

Chuoni ni wewe na mambo yako. Kama miundombinu ya kutosheleza pamoja na walimu wapo wa kutosha, basi sioni tatizo.

Miaka mitatu kumbe? Nilidhani Tumaini pekee ndiyo hutumia miaka mitatu.
 
Najua, nadhani hata kibatala kasoma pale pia. Ila ukiangalia prospectus yao inaonesha idadi ya wahadhiri walionao, kwangu nimeiona hiyo idadi ya wanafunzi ni kubwa sana kwa wale walimu.
Part time huwa hawawekwi kwenye prospectus

Walimu wako wengi kuliko hao wa prospectus
 
Kwani, Chuoni mnafatiliwa kama watoto?

Kwamba lazima uhakikishe umemsimamia mwanafunzi kaingia darasani, umsahishie daftari, umwajibishe kwa makosa yake?

Chuoni ni wewe na mambo yako. Kama miundombinu ya kutosheleza pamoja na walimu wapo wa kutosha, basi sioni tatizo.

Miaka mitatu kumbe? Nilidhani Tumaini pekee ndiyo hutumia miaka mitatu.
Hilo la walimu wa kutosha na miundo mbinu ndiyo nimeulizia. Sina uhakika nalo.
 
Miaka hutofautiana na Vipindi hutofautiana. Swali lako ni la kitoto ni sawa kuuliza shule ina wanafunzi 2000 walimu wako 15 tu shule nzima. Umesahau kuna vipindi na wanapishana muda wa kusoma, aina ya masomo nk. Au Wakati unasoma hapo chuoni mlikuwa mnasoma SHERIA TUPU kila kipindi??
 
Umeamua leta hoja nyepesi. Kuna uwiano wa wahadhiri vs wanachuo unaokubalika.
 
Kama heading ilivyo hapo juu niende moja kwa moja kwenye hoja yangu.

Kwa mwaka wa masomo uliopo sasa (2021/22) nimesoma chuo kikuu cha Mzumbe kwa kampasi ya Morogoro na Mbeya pekee walidahili wanafunzi elfu moja wa sheria kwa mwaka wa kwanza; na kwa vile wanatoa digrii ya sheria kwa miaka 3, ninakadiria kuwa kwa sasa watakuwa na angalau wanafunzi elfu 3 wa digrii ya sheria.

Hiki kitu kimenifanya nitafakari ubora wa elimu inayotolewa hapo. Je, kuna walimu wa kuwatosha hao wanafunzi wote?

Ufafanuzi ukipatikana toka kwa wadau wa MU itapendeza zaidi.
Kama wewe umesoma Mzumbe kwenye level ya Chuo Kikuu usingekuja na uliyoyaleta. Binafsi naiona ni idadi ndogo sana hiyo kwa dunia ya leo.

Ukifika level ya degree utaelewa haihitajiki Mwalim kama wa shule ya msingi ambae inabidi akufundishe kusoma na kuandika.

Kinachohitajika ni Wahadhiri (lecturers) tu na "teaching assistants" kutokana na wanafunzi wenyewe. Kwa teknolojia ilivyo sasa, lecturer mmoja anaweza kuhadhiri kwawanafunzi mamilioni wa chuo kikuu waliopo hapona wasiopo hapo tena wakiwa wametapakaa dunia nzima. Mwanafunzi wa Chuo kikuu hasomeshwi bali anajisomea mwenyewe. Yeye ni kuelekezwa tu (kazi ya teaching assistants). asipoelewa. Mihadhara dnia ya leo yote huwa recorde digitally, kwa hiyo hata ukikupita unaweza kuupata muda wowote na ukausikiliza kwa muda wao.

Siku hizi madarasa kuanzia ya chekechea mpaka vyuo vikuu duniani huko, hata yanayoandikwa ubaoni yanarekodiwa yote digitally, kwa kuwa watu wameshaachana na blackboards (soiku hizi kuna smart boards) za kufundishia. Tena mashule na vyuo vingine duniani, darasa lote linarekodiwa kiukamilifu kuanzia Mwalimu mpaka wanafunzi, toka muda wa masomo unapoanza mpaka unapokwisha. Hakuna kuleteana matatizo.Kalagabaho.

Nakumbuka enzi za utawala wa Kikwetew alisisitiza sana shule zote ziwekewe umeme hata wa solar na mawasiliano yafikishe ili wanafunzi waweze kusomeshwa hata na Walimu chache sana waliobora. Nikaelewa huyu katika safari za duniani kishakumbana na shule zenye smartboards na kaelewa anawafahamisha nini Watanzania, sielewi kama watendaji walimuelewa. Ikiwa watendaji wenyewe akili zao ni kama wewe, nnashaka sana kama kuna wengi walimuelewa.
 
Kama heading ilivyo hapo juu niende moja kwa moja kwenye hoja yangu.

Kwa mwaka wa masomo uliopo sasa (2021/22) nimesoma chuo kikuu cha Mzumbe kwa kampasi ya Morogoro na Mbeya pekee walidahili wanafunzi elfu moja wa sheria kwa mwaka wa kwanza; na kwa vile wanatoa digrii ya sheria kwa miaka 3, ninakadiria kuwa kwa sasa watakuwa na angalau wanafunzi elfu 3 wa digrii ya sheria.

Hiki kitu kimenifanya nitafakari ubora wa elimu inayotolewa hapo. Je, kuna walimu wa kuwatosha hao wanafunzi wote?

Ufafanuzi ukipatikana toka kwa wadau wa MU itapendeza zaidi.
Hoja hasa ni nini tatizo la hio idadi kwako ni nini? What has 1000 students for each year to do with your concern? Ubora kivipi kwa mfano?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom