Mzuka wa ushangiliaji wa Kocha Robertinho haukuanzia hapa Simba; alikuwa hivyo toka anacheza mpira wa miguu kwao nchini Brazil

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Jan 26, 2019
1,932
4,086
Kohh koooh...

Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo, ukipenda unaweza kumuita Robertinho alikuwa mshambuliaji nguli aliyechezea vilabu vikubwa nchini brazil, mwisho mwa miaka ya 70 mpaka mwishoni mwa miaka ya 80. Kocha huyu anayewaonoa wekundu wa msimbazi kwa sasa, aliwahi kukipiga katika vilabu vikubwa nchini brazil kama vile Fluminense, Flamengo, Palmeiras, Atletico mineiro na Sport recife kabla ya kutimkia barani ulaya kukipiga katika timu ya Nacional nchini ureno na kisha kumalizia soka lake nchini Uswiss.

Akiwa katika klabu ya fluminese iliyosheheni mastaa wa kikosi cha selecao, timu ya taifa ya brazil kama branco na edinho, mwaka 1978-1982, Robertinho pia alipata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha taifa la brazil na kucheza na mastaa kama Zico, Socrates, Batista, Luizinho, julio cesar na bwana mdogo Bebeto.

Klabu ya fluminense ilikuwa inanolewa na kocha nguli wa brazil, Mario Lobo Zagallo.

Robertinho-Claudio-Adao-Zeze-Fluminense-1980.jpg

Pichani Robertinho kushoto akiwa na mastaa wa kikosi cha fluminense, Adao na Zeze.

Mara baada ya kutoka fluminense winga wa kulia mwenye kasi sana , namzungumzia Robertinho, alisajiliwa katika klabu ya Flamengo ambayo aliisaidia kutwaa ubingwa wa brazil, kwenye kikosi cha flamengo kulikuwa na mastaa wakubwa kama Zico, julio cesar,bebeto na junior.

Robertinho alisaidia kutengeneza goli la tatu lililofungwa na Adilio na kuifanya timu yake iweze kuifunga timu ya Santos kwa jumla ya magoli 3-0 na kutwaa ubingwa.

brazil80.jpg


Pia klabu ya flamengo ilishiriki mashindano ya Coppa Supermondiale Clubs nchini italy, ambapo katika mechi dhidi ya intermillan , Robertinho alitupia bao la kwanza na kuisaidia timu yake kushinda kwa magoli 2-1, katika fainali walikipiga dhidi ya Juventus iliyokuwa na magwiji wa soka kama gwiji wa ufaransa Michel Platini, gwiji wa Poland Zbigniew Boniek, Claudio Gentile, Marco Tardelli na Paolo Rossi ambaye alikuwa mfungaji bora wa michuano ya kombe la dunia mwaka 1982. Flamengo ilimaliza mashindano hayo ikiwa nafasi ya pili nyuma ya juventus.

Mara baada ya kutoka flamengo alijiunga na klabu ya Palmeiras na kisha kurudi tena kukipiga katika klabu ya flamengo.

flamengo86.jpg

Pichani kutoka kushoto waliochuchumaa ni Robertinho akiwa na mastaa wa kikosi cha flamengo.

Mwaka 1987 alisajiliwa na klabu ya Sport Recife iliyokuwa na mastaa kama Ribamar,Betao na Marco Antonio, aliiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa brazil na kisha kusajiliwa ya internacional na baada ya hapo klabu ya Atletico mineiro mwaka 1989 ambapo pia alitwaa ubingwa wa brazil akiwa na mastaa kibao wa taifa hilo kama kina marquinhos, Eder lopez, Zanata, batista,Gerson na Romulo.

mineiro89.jpg


Mara baada ya kutoka Atletico Mineiro, Robertinho alitimkia nchini Ureno na kisha kutundika daluga nchini Uswisi ambapo alianzia taaluma ya ukocha toka mwaka 1995 mpaka hivi sasa ana takribani miaka 28 anafundisha soka.

Unaweza kujiuliza mbona huyu kocha huwa ana mizuka sana pindi simba wakifunga magoli, jibu ni kuwa Robertinho licha ya kuwa winga mshambuliaji hatari pia alikiwa akipenda sana kushangilia pindi alipokuwa akifunga mabao nchini kwao brazil. Hivyo si ajabu bado akiendelea na mzuka uleule kama pindi anasukuma gozi nchini kwao brazil.

Unaweza kuona baadhi ya highlights zake za magoli wakati anacheza nchini Brazil



Kocha Robertinho alinifurahisha juzi alipohojiwa na Afisa habari wa simba, Ahmed Ally kuwa je anahisi presha pindi simba atakapocheza katika uwanja wa Mohammed V pale jijini Casablanca dhidi ya Wydad? Robertinho alicheka akamwambia hapana kwasababu kwanza huwa anapenda derby kwani wakati anacheza mpira kashapitia yote hayo kucheza ktk uwanja wa maracana uliosheheni idadi kubwa ya mashabiki kuliko hata huo uwanja wa morocco hivyo haofii chochote na anapenda mazingira hayo ya mashabiki kujaa uwanjani.

Kocha Robertinho anaamini kuwa Simba ina wachezaji wakubwa wenye uzoefu wa kutosha wa mashindano ya CAF champions league na anaamini kuwa wataifunga Wydad CA na kufuzu hatua ya nusu fainali. Mwisho Robertinho alilisisitiza kuwa anapenda kuona wachezaji wakikimbia pindi wawapo na mpira na wasipokuwa na mpira na anaamini katika Mungu, kisha wachezaji wake wa Simba na mashabiki wake kwa ujumla.

WE ARE SIMBA, WE ARE UNSTOPPABLE!!!!

Cc
NALIA NGWENA
Labani og
 
"Mara baada ya kutoka Atletico Mineiro, Robertinho alitimkia nchini Ureno na kisha kutundika daluga nchini Uswisi ambapo alianzia taaluma ya ukocha toka mwaka 1995 mpaka hivi sasa ana takribani miaka 28 anafundisha soka."

Ungemalizia , bila mafanikio
 
"Mara baada ya kutoka Atletico Mineiro, Robertinho alitimkia nchini Ureno na kisha kutundika daluga nchini Uswisi ambapo alianzia taaluma ya ukocha toka mwaka 1995 mpaka hivi sasa ana takribani miaka 28 anafundisha soka."

Ungemalizia , bila mafanikio
Mbona una SHANGA..ZAA
 
Safi sana. Ili uwe mkubwa lazima ukutane na wakubwa, Simba hii ndio njia sahihi ya kufuata kuelekea ukubwani maana huwezi mfunga Zolan (Sudan kusini) bao 10 eti ndio utegemee kutambuliwa kuwa mkubwa
 
Robertinho umethibitisha ubora wako jinsi gani umembadilisha JINI BALEKE kuwa merciless infront of the goal
 
Izo Picha ungewatumia Wydad labda wange ogopa historia ya kocha wenu.
 
Ata Juma Mgunda alikua mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania pia ali isaidia costal union kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara na alikua mmoja ya washambuliaji hatari katika mashindano ya vilabu Africa mashariki na kati 1989 (CECAFA) mashindano yaliyofanyika Kenya.

Alifanikiwa kuipeleka Costa final katika mashindano hayo japo katika fainali walifungwa na Kenya Breweries.

Lakini Mgunda Hana Mbwembwe za Robertinyo.
 
Back
Top Bottom