Robertinho ni kocha wa mpira kweli, naomba wana Simba tumheshimu kuanzia leo

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Mara baada ya mchezo wa leo kuisha kwa sare ya bao 1 1, nimekaa chumbani kwa dakika 30 nikimfanyia assessment kocha Robertinho kwa kile nilichokiona leo pale uwanjani Misri.

Kuna baadhi ya wachezaji ambao mashabiki wa Simba waliojifunza mpira miaka ya 2010 hadi sasa hawawakubali kabisa na hawako tayari kuwakubali lakini huwezi amini Robertinho ametia pamba masikioni na anawatumia wachezaji hao na kiukweli wanamsaidia sana, yaani wachezaji ambao sisi mashabiki tunawaona ni mzigo yeye Robertinho anawaona ni asset.

Mechi ya leo wengi hawakufurahishwa kuona Bocco akianza, lakini master Robertinho anamuona Bocco ni mzuri kiufundi kuliko Phiri, Baleke, Chilunda.Bocco anaonekana ana msaada sana kwa Robertinho kuliko tunavyofikiri sisi, wanasimba tumelalamika weeee lakini Robertinho ametuambia hapana, Bocco ni the best.

Wachezaji kama Esomba Onana sisi tunamuona sio mchezaji mzuri lakn Robertinho anamuona ni mtu hatari sana mcameroon huyo, Onana yuko kwenye majaribu tu lakini kiukweli ni mchezaji mzuri na style yake haitobadilika, wana Simba msimzomee Onana, ni mchezaji anayeaminiwa na Robertinho na ndio maana hajawahi kukaa benchi, asipoanza ataingia kipindi cha 2.Huyo ndio Esomba Onana.

Wachezaji kama Kibu Dennis, Saido, Mzamiru nao wanalalamikiwa sana lakini Robertinho ndio anajua uzuri wao, kwa kweli kocha huyu nimemvulia kofta kuanzia leo.

Wachezaji hao ndio wamepambana na kuiletea heshima Simba leo ingawa tumeondolewa kwa sheria ya bao la ugenini, tunawabeza akina akina Kapombe, Shabalala lakini ndio hao leo wamemweka katika wakati mgumu sana kocha wa Al Ahly.

Wana Simba tuheshimu taaluma za watu, sio kila anajua kufundisha mpira jamani, kumkabili mwarabu kwao kwa dakika 100 halafu matokeo ni 1 1 sio jambo dogo, kazi kubwa imefanyika.
 
Jamaa anajua sana, hizi mechi ndio Simba tumezoea wanakufa 5, pia kama umeangalia mechi utaona Simba wametengeneza nafasi nyingi ni uzoefu mdogo tu ndio umewatoa. Mechi nzima imeisha Al Ahly ana on target 2 tu, sababu ya ukuta wa Simba iliwabidi kujaribu mashuti ya mbali mda mwingi.
 
Mara baada ya mchezo wa leo kuisha kwa sare ya bao 1 1, nimekaa chumbani kwa dakika 30 nikimfanyia assessment kocha Robertinho kwa kile nilichokiona leo pale uwanjani Misri.

sha mpira jamani, kumkabili mwarabu kwao kwa dakika 100 halafu matokeo ni 1 1 sio jambo dogo, kazi kubwa imefanyika.
Mashabiki wa mbumbumbu akili zenu ni sawa na za viwavi jeshi, uyo Robertinho unayemsifia mbinu zake ni za kizamani na atowapeleka kokote, mechi za kuvuka zinachezwa kwa hesabu na akili kubwa, angekuwa ni kocha mzuri Leo hii Simbwa ingefuzu but mbinu dhaifu za kocha ikichangiwa na aina ya wachezaji mlionao ndio kilikuwa kitanzi kwenu,

Aly ahly alicheza ili afuzu hatua inayofata na amefanikiwa Sasa Robertinho Kama sio kupata goli lililombabatiza Baleke na kuingia golini alikuwa Hana plan yoyote ya maana! Kuitwa mwakarobo mnastahili kwa maana mtakuwa mnaishia kubwata kuwa mmekufa kiume Kila mwaka!!! Mechi 4 za kimataifa na droo 4, no ushindi ndio kocha wenu Bora uyo!
 
Nitajie kocha wa simba mwenye matokeo kama ya robertinho toka umeijua simba
Juzi niliwaambia simba wana kocha mzuri ila analaumiwa tu.sababu ya msingi hakuna.

Mimi nasema hivi..!!
MATORA alisababisha makocha wengi wa kigeni kufukuzwa, na sasa amekuja MGUNDA nae naona makocha bado wanapata usumbufu kama ilivyokua kipindi cha matora.

Watu hawa ndio virusi vinavyofanya makocha wazuri kutukanwa na kulaumiwa. Maaana sioni sababu ya kocha kama mbrazil kutukanwa na kuzalauliwa bila ya sababu.
 
Jamaa anajua sana, hizi mechi ndio simba tumezoea wanakufa 5, pia kama umeangalia mechi utaona Simba wametengeneza nafasi nyingi ni uzoefu mdogo tu ndio umewatoa. Mechi nzima imeisha Al Ahly ana on target 2 tu, sababu ya ukuta wa simba iliwabidi kujaribu mashuti ya mbali mda mwingi.
Ukuta umewasaidia Nini Sasa pamoja na kujazana kule nyuma Kama kumbi kumbi? Kinachoangaliwa ni kufuzu vipi huo ukuta umewafanya mfuzu hatua inayofata?
 
Nitajie kocha wa simba mwenye matokeo kama ya robertinho toka umeijua simba
Robertinho ni kocha wa kawaida,,kutoa sare na Al ahly sio jambo la ajabu na tunaita kukamia kama vile Ihefu ilivyokaamia yanga
 
Robertinho ni kocha wa kawaida,,kutoa sare na Al ahly sio jambo la ajabu na tunaita kukamia kama vile Ihefu ilivyokaamia yanga
Simba iliyopigwa tano haikukamia game? Wapeleke singida big star wakakamie game afu uone
 
Simba iliyopigwa tano haikukamia game? Wapeleke singida big star wakakamie game afu uone
Simba ya leo aina mtu kama miqueson wala mtu kama okwi mbele, watu alionao rober ndo hao wakina kibu na boco lakini anajitaidi kutengeneza timu na wachezaji wavunja miwa
 
Simba iliyopigwa tano haikukamia game? Wapeleke singida big star wakakamie game afu uone
Singida walikamia wakapigwa goli 4 na Future FC katimu kadogo ukilinganisha na Al Ahly.Ihefu hajakamia kawafunga mara 2 mfululizo.Tena mara zote mkitangulia kufunga.Mpo kundi moja mkamie na wewe.
 
Back
Top Bottom