Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Nishati ndiyo roho ya taifa lo lote. Uchumi na ustawi wa nchi hutegemea upatikanaji wa kutosha na wa bei nafuu wa nishati. Uharibifu wa tabia nchi unatokana kwa kiasi kikubwa na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa kwa sababu ya ukosefu wa nishati mbadala ya bei nafuu.
Suala la nishati na hasa umeme, na sasa hivi pia mafuta ya petroleum, limekuwa zigo kubwa kuanzia enzi za Lowasa na Kikwete. Mmasai huyo na mswahili huyo wa pwani ya Msoga walishindwa kabisa kulibeba zigo hilo la nishati. Alipopewa zigo hilo mnyamwezi wa Chato aliweza kulibeba vizuri zigo hilo na kuashiria kutimia kwa ndoto ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025 (industrial country by 2025).
Awamu ya sita ilimbebesha zigo hili la nishati mswahili mmoja wa pwani ya Tanga. Kwa miaka takribani miwili mswahili huyu wa Tanga aligara gara na zigo hili hadi kutia huruma. Nchi ikakosa umeme kwa asilimia 60%, viwanda vikasimama kwa asilimia 40% na bidhaa kutoka viwandani vikapanda bei maradufu, ikawa haiwezekani kuanzisha viwanda vipya. Mbaya zaidi ikafikia hadi mafuta ya petroleum kuadimia kwa asilimia 90% na bei zake kupanda kwa asilimia 300%. Hali ikawa mbaya sana, uswahili ukawa mwingi ku justify hali hiyo.
Wahenga walishatuasa kwamba mzigo mzito mpe mnyamwezi abebe. Siku zote wahenga hawasei. Sasa zigo hili kabebeshwa mnyamwezi wa Bukombe. Tena kaongezewa nguvu ya unaibu waziri mkuu kulibeba hilo zigo ambalo kwa sasa limekuwa kubwa zaidi. Anahitaji mbinu za namna ya kulibeba. Jf kama jukwaa la Great Thinkers tumshauri mbinu anazoweza kuzitumia kulibeba zigo hili bila kuumia. Nitaanza na hizi chache:
1. Bwawa la NHPP lilishakamilika tayari kuanza kwa uzalishaji wa umeme. Sababu walizotoa hao waswahili ni kwamba kituo cha Chalinze cha kupitishia huo umeme hakijakamilika na wanatarajia kitakamilika mwezi July 2024. Ushauri: ziwashwe genereta mbili au tatu kati ya genereta 9 zilizopo pale bwawa la Nyerere. Hizi zitatupa MW takribani 600. Hizi ziingizwe kwenye grid ya taifa kupitia njia iliyo karibu na bwawa hilo. Waharakishe kujenga hiko kituo cha Chalinze, kikamilike ifikapo Desemba mwaka huu. Kijengwe mchana na usiku.
2. Umeme kutoka bwawa hilo usiuzwe zaidi ya TSh. 50 kwa kila unit moja ili hata mwananchi wa kawaida aweze kutumia umeme kupikia chakula badala ya kuni na mkaa.
Hao waswahili walishapanga kuongeza bei ya unit mradi huo wa JNHPP utakapokamilika. Walishasema kamwe hawatateremsha bei hiyo ya unit. Walishapanga kwamba kiasi kikubwa kama siyo chote cha umeme huo watauuza nje ya nchi hususani Zambia na Kenya kupata USD dollars, sisi tutaendelea kubangaiza huo umeme wa gesi kutoka Kinyerezi. Sababu waliyotoa eti ni kurudisha pesa iliyotumika kwenye ujenzi wa huo mradi.
Fedha zilizotumika kwenye ujenzi huo siyo zao bali ni kodi za wananchi zilizotumika ili wapate umeme wa bei nafuu na wa uhakika. Huwezi ukajenga hospitali au barabara kwa pesa itokanayo na kodi za wananchi, halafu ukataka kuwatoza tena wananchi hao wakitumia hiyo hospitali au hiyo barabara ili kurudisha pesa iliyotumika kuijenga. Vivyo hivyo kwa miundombinu zingine zinazojengwa na serikali au kwa vifaa na vitendea kazi vinavyonunuliwa na serikali hususani CT scan, MRI na kadhalika. Anayefanya hivyo ni mtu binafsi au kampuni binafsi aliyetumia hela yake binafsi kununua vifaa hivyo au kujenga miundombinu hizo. Pesa ya serikali inatoka kwenye kodi na tozo za wananchi. Hata kama pesa hiyo serikali ilizikopa, marejesho yake yanatoka kwenye kodi za wananchi.
3. Utaalamu (profession) unabidi uheshimiwe. Kwenye tasisi za kitaalamu, mtendaji mkuu anapaswa kuwa ni mtu aliyebobea kwenye hiyo taaluma. Huyo ndiye atakayeweza kuwasimamia, kuwaongoza na kuwaelekeza watendaji wenzake kwenye hiyo taasisi na kamwe haitakuwa rahisi kumdanganya.
Haingii kichwani mtendaji mkuu wa hospitali ya taifa kama Muhimbili akawa ni mwanahabari (journalist) halafu ukategemea ufanisi kwenye hiyo hospitali. Mhasibu akawa mtendaji mkuu wa TANROADS, Medical Doctor akawa mtendaji mkuu wa jeshi la wananchi au la polisi na kadhalika. Watu wapewe kuongoza maeneo ambayo wana utaalamu nayo. Wakurugenzi wa utawala wawe ambao wana taaluma ya utawala wa watu (public administration), wakurugenzi wa fedha lazima wawe wenye taaluma ya fedha na kadhalika.
Shirika la umeme, mtendaji mkuu wake anapaswa kuwa mbobezi kwenye taaluma ya umeme (senior electrical engineer). Vivyo hivyo kwa mameneja wa kanda, mikoa na wilaya. Vinginevyo shirika litaendelea kuchezewa na kudanganywa na wahandisi wake wa umeme.
4. Serikali inunue mafuta ya petroleum yenyewe moja kwa moja kutoka nchi zinzozalisha hayo mafuta. BoT na TPDC zitumike kutekeleza hili. Tutimize ndoto ya nchi yetu ya kuwa hub ya mafuta haya kwa nchi zinazotuzunguka na ambazo ni landlocked.
Tuachane kabisa kutumia hawa middle men ambao wametuchezea sana. Bei ya mafuta haya duniani yalifikia peak ya USD 135 kwa pipa mwezi March 2022. Baada ya hapo yalianza kushuka taratibu hadi kufikia USD 60 kwa pipa. Ni hivi juzi tu nchi za OPEC+ ikiwamo Russia zilipoamua kupunguza kidogo uzalishaji na kuwezesha kuyapandisha bei hadi kufikia USD 90 kwa pipa. Hii ndiyo trend ya bei ya mafuta haya duniani. Serikali kupitia wizara ya nishati na EWURA yao, imekuwa ikijifanya haioni trend hii na hivyo kuruhusu middle men hawa trend za bei zao ni ya kupaa tu kila mwezi kuanzia hiyo March 2022. Yaani leo sisi bei yetu kwa sasa ni maradufu ya bei ya mwezi March 2023 pipa lilipokuwa linauzwa dollar 135 wakati sasa linauzwa dollar 90 tu.
5. Great thinkers wa JF endeleeni kumpa mbinu za kulibeba hili zigo kubwa la nishati huyu mnyamwezi. Hapa mambo ya itikadiza kisiasa hazitakiwi. Na kama wewe siyo Great thinker hautakiwi.