Mzee wa Upako Avamiwa, Atekwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee wa Upako Avamiwa, Atekwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 29, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280


  mzeewaupako.jpg

  Haruni Sanchawa na Gladness Mallya
  MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi – Utashinda, Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako usiku wa kuamkia jana alivamiwa kanisani na kundi la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kumteka kwa muda kabla ya kumpora mamilioni ya shilingi.

  Gazeti hili lilifika eneo la tukio kanisani kwake, maeneo ya Ubungo Kibangu na kufanikiwa kupewa taarifa ya jinsi ujambazi huo ulivyofanyika ambapo mtoa habari alisema kundi la majambazi lilivamia kanisa hilo usiku.

  “Kundi hilo la watu lilifika maeneo hayo majira ya saa tisa na kuwateka walinzi ambao walikuwepo hapo hadi saa kumi na moja alfajiri kuamkia jana,” alisema mtoa habari wetu kwa sharti la kutoandika jina lake gazetini.

  Imedaiwa kuwa kabla ya kufanya uvamizi huo, mlinzi wa kanisa hilo (jina tulihifadhi kwa sababu za kiusalama ), alivamiwa na kufungwa kamba na baadaye kunyang’anywa bunduki na majambazi hao.

  Chanzo chetu hicho cha habari kiliongeza kuwa baada ya kumkamata mlinzi huyo, majambazi hao walienda moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Lusekelo na kumteka kwa muda kabla ya kumuamuru atoe pesa alizokuwanazo vinginevyo wangemuua.

  Habari zinasema Mzee wa Upako aliamua kutoa pesa ambazo inadaiwa ni zaidi ya shilingi milioni 20 ambazo inaaminika zilitokana na sadaka za waumini wake. Kiongozi huyo wa kanisa hakujeruhiwa.

  Habari za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa Mchungaji Lusekelo hakai kanisani hapo na kwamba ni mara chache hulala katika nyumba hiyo ya ibada hasa anapokuwa na kazi maalum.

  Gazeti hili lilipowasiliana na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga alikiri kutokea kwa tukio hilo na amedai kuwa hadi sasa watu wawili wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.

  “Uzoefu unaonyesha kuwa kuna baadhi ya makampuni ya ulinzi hapa nchini yana watumishi ambao si waaminifu, natoa wito kwa wamiliki wa makampuni binafsi ya ulinzi kabla ya kuajiri mlinzi , yahakikishe uaminifu wake kwanza,” alisema Kalinga.

  Aliongeza kuwa kampuni za ulinzi zinalinda mamilioni ya mali za watu lakini anashangazwa kuona baadhi ya walinzi wao wanauza siri za muajiri wao kwa watu wasio raia wema.

  Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Mzee wa Upako ili kusikia kauli yake juu ya tukio hilo bila mafanikio.
  Kwa mujibu wa walinzi waliokutwa kanisani hapo ambao hawakupenda majina yao kuandikwa gazetini, kiongozi huyo alikuwa amekwenda nyumbani kwake Mbezi kupumzika
  MZEE WA UPAKO - Global Publishers

   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu_kwa taarifa yako hii habari ni ya long time kitambo saaaana,ilitokea ndani ya miezi ya mwanzoni ya mwaka 2011,.....labda kama una ajenda ya siri unayotaka kuijenga hapa janvini.

  Ushauri wa bure kwako mkuu MziziMkavu:..Una mchango uliotukuka kwenye Jukwa la Jf doctor,lakini huku kwingine hauna jipya zaidi ya kuchochea na kuleta upuuzi wa kidini....hivyo bora ungebaki kule una_fit mkuu.
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Eeeeh...ana bunduki! amshoot nani? Naye anahitaji ulinzi dunia! mungu wake hamtoshi?!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ushauri kama huu wako nilimpa juzi!...ningekuwa mimi ni yeye nisingeingia kwenye mada ambazo zinazua watu kujiuliza kuhusu misimamo yangu!
   
 5. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Watashindana lakini hawatashinda. Kweetu hakuna kuibiwa. Kwaeetu hakuna ujambazi.
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Makubwa watu wameenda kuiba sadaka!
  Kama ni ya kitambo mimi ndo naiona leo si unajua access ya magazeti ya udaku sina!
   
 7. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hapa tukubaliane yeye mwenyewe imani yake ni haba,hakuwa na sababu ya kuwa na bunduki na hata hao walinzi wanatajwa. C anaamini neno?
   
 8. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Duuh,kumbe jamaa ni mdini?
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Watakwenda kuiiiibaaaa Patakapoibikaaaa.
   
 10. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kwa nn unaleta habali hii leo
   
 11. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kweeetu hakuna kuibiwa.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...