Mzee Wa Upako awavaa Maskofu, asema "Maaskofu wa Katoliki wameitumia nafasi vibaya, wamepotoka"

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,462
ASKOFU LUSEKELO: TEC WAMEPOTOKA KWA KUTOA ANDIKO LA MKATABA WA BANDARI
Askofu Kanisa la Tutashinda, Antony Lusekelo ametoa maoni kuhusu Waraka wa uwekezaji wa Bandari uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) akidai kitendo kilichofanywa na Baraza hilo kutoa Waraka hadharani wakati huu ni kupotoka.

Amesema “TEC mmepotoka, mamlaka mliyopewa na Kanisa mmeyatumia hovyo, hamjaangalia mazingira na hali halisi, jambo linaweza kuwa sawa lakini mahali pake na si wakati wake.”

Ameongeza “Ninawashauri TEC waondoe huo Waraka, wasiendelee kuuzungumza, wakae kimya hauna afya kwa amani na utulivu wa Nchi, hausaidii umoja wa Nchi yetu, unawagawa Watanzania.”


ASKOFU LUSEKELO: MA-BABA ASKOFU MMEKOSEA SANA
Askofu Kanisa la Tutashinda, Antony Lusekelo amesisitiza kuwa kilichofanywa na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ni makosa.

 
Mzee wa upako ni mjasiliamali au vipi bhana. Hawezi enda nchi ya beat ya watawala. Kilichomkuta Mzee kakobe we all know.
 
Back
Top Bottom