Kionambele
JF-Expert Member
- Jan 14, 2010
- 236
- 93
Sii busara kabisa kwa mtu kutumia mgongo wa kanisa kutaka heshima kwa watawala wa kisiasa(kaisari). Labda kama ingekuwa dini kusingekuwa na mshangao sana. Kuna tufauti kubwa sana kati ya kanisa na dini. Nini ni organisation(muungano) wenye malengo mchanganyiko ya kimungu na kisiasa pamoja. Kanisa ni wale wlioitwa watoke kibinafsi yaani kuzaliwa upya ktk ufalme wa mbinguni na bila lengo lingine lolote. Sasa ukatoliki, uluteri kama anavyovitaja lusekelo ni organisation na yeye kama anataka kuheshimiwa na watawala aanzishe ya kwake. Haikuwahi kutokea bwana yesu au wanafunzi wake kulalamika kwamba hawaheshimiwi na kaisari ila walisisitiza kama kaisari au watu wa jinsi yake waliowaita mataifa wangetaka uahirika nao ni sharti kwanza wazaliwe upya(okoka). Historia ya kanisa la katoliki inajulikana vizuri. Hili kanisa ndio muungano(dhehebu) la kwanza kujitengeneza nje ya kanisa na malengo yake yalikuwa ni ya kisiasa na kidini kwa pamoja. Siasa iliwachipusha kutoka ukristo hadi kuwa mapagani wenye jina la ukristo. Jambo hili lilipelekea Martin Luther kujitenga na kutoa mapingamizi 95 ya ubaya wa watawala wa dhehebu la katoliki. Nulisema hawa walikuwa na malengo ya kisiasa zaidi na hivyo ilipelekwa bunge llililofanyika ktk mji wa speyer(spires) wakatoliki walikuwa wengi zaidi wakatoa tangazo kwamba yasiwepo mabadiliko ya dini zaidi ktk maeneo ya walutheri, yaani wakatoliki wawe huru kuabudu kikatoliki ktk maeneo ya walutheri lakini wao walutheri wasiwe huru maeneo ya wakatoliki kufanya hivyo. Waluteri waliitikia kanuni hiyo kwa kukataa(protest) matokwo yake walipewa jina la PROTESTANT mwaka 1529. Waluteri wa sasa kujinabisisha jina la luther huku wakiwa tofauti kabisa na luther kimtizamo na kimatendo ni sawa na katoliki kujinabisisha na Kristo wakiwa tofauti kabisa na Kristo mwenyewe. Huu ni unafiki wa kiwango cha juu. Waluteri sawa na Neno la Mungu wanamrudia mama yao katoliki na pia wapentekoste sharti nao warudi kwa mama yao. Na mathihirisho ni kama unavyoona wakililia utambulisho kisiasa sawa na katoliki na Lutheran. Kibaya zaidi kwa wapentekoste wao hawana baba(kiongozi) wanaeitwa kwa jina lake kama walivyo wakatoliki na walutheri. Wao wametawanyika mno kila kakikundi kidogo wanajitambulisha kivyao vyao. Upinzani walioupata walutheri kwa wakatoliki ndio wanaoupata wapentekoste kwa haya madhehebu makubwa. Hivyo kuna kazi kubwa sana kwa kina Lusekelo kuweza kukubaliwa kundini na kupewa heshima za kisiasa kama lutheran nao walivyokubaliwa
Hapa nikiongeza nitaaribu.Yaani alichoandika Kiby hapo juu ni vizuri Anthony Lusekelo na wenzake wakakisoma kwa nia njema tu na kukifanyia kazi. Hiyo ndiyo injili. Inachoma.
Inachoma lakini Inaponya.