Mzee Timothy Apiyo Afariki Dunia

Mzee Timothy Apiyo Afariki Dunia

hii mpya, tena kali sana!... Ulitaka tumfahamu kupitia simulizi (oral tradition)? Huyu mzee hayupo kwenye vitabu, hata vinavyouzwa kwenye bookshop bwana. Unataka tukamtafute kwenye nyaraka za serikali?... Si kioja hiki?!!!...

Wewe eleza tujue tu tumepoteza mtanzania mwenzetu na mzee wetu.. Habari za historia mzee huyu hajawa recorded na history yake kuwa wazi kwa wote.

Naomba ubaki na msimamo wako nami nitabaki na wa kwangu....good day dear compatriot
 
Hii mpya, tena kali sana!... Ulitaka tumfahamu kupitia simulizi (oral tradition)? Huyu mzee hayupo kwenye vitabu, hata vinavyouzwa kwenye bookshop BWANA. Unataka tukamtafute kwenye nyaraka za serikali?... Si kioja hiki?!!!...

Wewe eleza tujue tu tumepoteza mtanzania mwenzetu na mzee wetu.. Habari za historia mzee huyu hajawa recorded na history yake kuwa wazi kwa wote.

we kweli kilaza!
Hujui kuwa Oral tradition ni miongon mwa source za historical info, pamoja na archives, museums,etc?
Huwezi tenganisha mzee huyu na history ya nchi hii, hasa utumishi wa umma. Km humfaham, we kilaza tu!
 
RIP MZEE Apiyo Msalimu sana mtakatifu julius Nyerere mwambie ccm imegeuka kuwa chama cha matajiri na mafisadi.. Kimegeuka kuwa si cha wanyonge tena...
 
we kweli kilaza!
Hujui kuwa Oral tradition ni miongon mwa source za historical info, pamoja na archives, museums,etc?
Huwezi tenganisha mzee huyu na history ya nchi hii, hasa utumishi wa umma. Km humfaham, we kilaza tu!

Yeye anataka vitabu tu na mitihani sijui tutaandika vitabu na kufanya mitihani juu ya watu wangapi wa nchi hii! Pengine hata hajui kuwa Mzee Sykes (ambaye naye sidhani kama ana kitabu) kama amefariki......vijana wengi wa sasa bwana!
 
REQUIEM... R.I.P Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Utawala wa Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mungu Akuweke mahari pema peponi...
 
RIP MZEE Apiyo Msalimu sana mtakatifu julius Nyerere mwambie ccm imegeuka kuwa chama cha matajiri na mafisadi.. Kimegeuka kuwa si cha wanyonge tena...

... Lo! Pumziko la Milele uwape ee Bwana, Na mwanga wa Milele uwaangazie, Wapumzike kwa amani...
 
RIP Mzee T Apiyo. Labda kuna siku nchi ikija kuwa na uadilifu, basi kitajengwa hata chuo kipewe jina lako.

Kila binadamu ana mapungufu yake ila ukweli ni kuwa kwa cheo alichokuwa nacho, angelitaka kuvuta hela ya nguvu basi leo hii watoto wake na wajukuu wake akina Timoth nk nk wangelikuwa na hela nzito sana hapa Tanzania.

Poleni sana familia nzima ya Apiyo na Watanzania kwa ujumla wanaoukumbuka uadilifu wa Serikali ya JK Nyerere.

Mungu akupe mapumziko mema huko ulikotangulia, AMEN.
 
MWENYEZI MUNGU ALIUMBA KIFO KWA AJILI YA BINADAMU.

KIFO CHA MZEE APIYO NI MAPENZI YAKE MUNGU.

HAKUNA BINADAMU ANAYEWEZA KUKIKIMBIA KIFO.

Tunakuombea ufike salama mbinguni. R.I.P
 
RIP Mzee Apiyo. Hawa ndio watu waliofanya kazi kwa uaminifu wa hali ya juu katika nchi hii. Mwalimu Nyerere alikuwa anamuamini sana Mzee huyu. Kwa sasa kuwapata watu kama Mzee Apiyo, ni ndoto.

Tiba

wapo ila hawapati fursa maana Tanzania ya sasa iko mikononi mwa genge la walafi,mafisadi,wazinzi,wasio na huruma na watu wenye majivuno na kejeli hivyo ukionyesha uadilifu hata kidogo kwao ama zao ama zako!
 
The Boss, hicho ni kipindi cha nyuma sana. Serikali miaka mingi imempatia gari na msaidizi wa kudumu na kumsaidia katika matibabu. Hata gharama za matibabu ni serikali imekuwa ikimpatia. Last year or so alipewa gari nyingine mpya Discovery 4.

Kama mapungufu yapo ni ya kawaida.

Kabla ya Blandina Nyoni kuingia wizara ya Afya Mzee huyu alipata taabu sana kupatiwa matibabu ; mara baada ya Blandina Nyoni kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ya Afya alikuwa msaada mkubwa sana kwa viongozi wastaafu kama mzee Apiyo. Ukweli ndio huo.
 
Back
Top Bottom