Mzee Timothy Apiyo Afariki Dunia


Sanctus Mtsimbe

Sanctus Mtsimbe

Tanzanite Member
Joined
Jul 14, 2008
Messages
1,848
Likes
212
Points
160
Sanctus Mtsimbe

Sanctus Mtsimbe

Tanzanite Member
Joined Jul 14, 2008
1,848 212 160

Ndugu zangu

Mzee Timoth Apiyo amefariki dunia usiku wa jana akiwa katika matibabu South Africa katika Hospitali ya Mill Park South Africa.

Serikali ikishirikiana kwa karibu na ubalozi wetu South Africa unafanya mipango ya kusafirisha mwili kuuleta Tanzania.

Msiba upo nyumbani kwake Sitaki Shari.

Poleni sana wafiwa; Clay; Slyvia pamoja na wanafamilia wote.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa.

Rest in Peace Mzee Apiyo. You lived your life kwa uadilifu wa juu.

Updates: as at 11th June 2013 at 11.00 PM

Unless kama kutakuwa na mabadiliko, status iko hivi:


 • Death Certificate itatolewa kesho Wednesday 12th June 2013
 • Mwili utawasili Alhamis Mchana na SAA
 • Ijumaa itakuwa shughuli ya kuuaga mwili wake nyumbani kwake Sitakishari

Update 2: 13th June 2013 at 12.00 Midnight


 • Kutokana na kukosa nfasi katika ndege ya Alhamis, sas mwili utawasili na ndege ya Ijumaa usiku SAA
 • Mwili utapokelewa na viongozi wa Serikali na Wanandugu
 • Mwili utalala nyumbani Sitakishari
 • Jumamosi asubuhi saa 4 kutakuwa na Ibada ya kumwaga marehemu na kutoa heshima za mwisho
 • Mchana mwili utasafirishwa kwa ndege kwenda Rorya Musoma ukiambatana na wanafamilia tisa
 • Ndugu jamaa na marafiki wengine 50 wataondoka na basi la JWTZ siku ya ijumaa alfajiri
 • Mzee Apiyo atapumzishwa siku ya Jumapili.

Update 3: 14th June 2013 1. Mwili utawasili leo saa moja jioni
 2. Utapelekwa nyumbani Sitakishari
 3. Kesho Jumamosi saa 2 last respect nyumbani kwake
 4. baada ya hapo utapelekwa karimjee Hall kwa last respect ya kitaifa. Public.
 5. Baada ya hapo mwili utasafirishwa kwa ndege kwende Musoma kwa maziko siku ya Jumapili.
 
Fred Katulanda

Fred Katulanda

Verified Member
Joined
Apr 1, 2011
Messages
233
Likes
10
Points
35
Fred Katulanda

Fred Katulanda

Verified Member
Joined Apr 1, 2011
233 10 35
Machache kuhusu Marehemu Timothy Apiyo

Timothy Apiyo ni mmoja wa viongozi nchini ambaye amefanya kazi wakati wa utawala wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Andaiwa kuwa mmoja wa viongozi machachari waandamizi waliokuwapo katika serikali hiyo ambayo Waziri Mkuu wake alikuwa ni Hayati, Edward Moringe Sokine.

Alishika nyadhifa za Ukatibu Mkuu katika wizara mbalimbali na kutokana na uhodari na uchapaji wake kazi baadaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Ikulu), wadhifa ambao kwa sasa unajulikana kama Katibu Mkuu Kiongozi.

Apiyo, alizaliwa katika wilaya ya Rorya, Tarafa ya Suba, mkoa wa Mara, na alipata elimu yake ya msingi na sekondari wilayani hapo na mwaka 1959 nilijiunga na Chuo Kikuu cha East Afrika Makerere Uganda ambako alichukua digrii ya kilimo na baada ya kuhitimu alipangiwa kufanyakazi katika Chuo cha Kilimo cha Ukiliguru.

Mwaka 1960 alipata uhamisho kwenda wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga kuwa Bwana Shamba wa Wilaya na mwishoni mwa mwaka huo alihamishwa tena kwenda Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro ambako alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga.

Agosti 1962 alipata ufadhili wa kwenda kusoma Marekani katika Chuo Kikuu cha West Virginia ambako alichuwa digrii ya pili ya Sayansi ya Kilimo na kutunukiwa cheti mwaka 1963.

Mwaka 1964 alipangiwa kufanyakazi Wizara ya Kilimo na baadaye alipelekwa Shinyanga kuwa Ofisa Kilimo wa Mkoa na Desemba 1965 na kisha kwenda mkoa wa West Lake (Sasa Bukoba) na mwaka 1967 alihamishiwa wizarani akiwa Afisa Mipango Mwandamizi. Mwaka 1968 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango Kilimo katika Wizara ya Kilimo na mwaka uliofuata 1969 aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Nyumba, Ardhi na Maendeleo Mijini.

Novemba 1969 alirudishwa tena Wizara ya Kilimo kuwa Katibu Mkuu na Aprili 1972 alihamishwa na kwenda kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda na Aprili 1974 Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Julai 1986 alistaafu kazi.
 
M

mnyinda

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Messages
277
Likes
0
Points
0
M

mnyinda

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2012
277 0 0
Alikuwa na cheo gani huyo mzee?
 
M

mnyinda

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Messages
277
Likes
0
Points
0
M

mnyinda

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2012
277 0 0
Duh! Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu. Utawala wa Rais wa Kwanza Mwl. Julius Kambarage Nyerere (RIP)
asante kwa tarifa ila nimeshtuka maana macho na masikio dunia nzima sasa yapo africa ya kusini,
 
TUMBIRI

TUMBIRI

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2011
Messages
1,934
Likes
13
Points
0
Age
21
TUMBIRI

TUMBIRI

JF-Expert Member
Joined May 7, 2011
1,934 13 0
R.I.P Mzee Thimothy Apiyo!
 
Sanctus Mtsimbe

Sanctus Mtsimbe

Tanzanite Member
Joined
Jul 14, 2008
Messages
1,848
Likes
212
Points
160
Sanctus Mtsimbe

Sanctus Mtsimbe

Tanzanite Member
Joined Jul 14, 2008
1,848 212 160
Last time nilisikia huyu mzee analalamika kutelekezwa na serikali
maisha yalikuwa magumu mno kwake...
The Boss, hicho ni kipindi cha nyuma sana. Serikali miaka mingi imempatia gari na msaidizi wa kudumu na kumsaidia katika matibabu. Hata gharama za matibabu ni serikali imekuwa ikimpatia. Last year or so alipewa gari nyingine mpya Discovery 4.

Kama mapungufu yapo ni ya kawaida.
 
Last edited by a moderator:
P

Phillemon Mikael

JF Gold Member
Joined
Nov 5, 2006
Messages
9,290
Likes
3,065
Points
280
P

Phillemon Mikael

JF Gold Member
Joined Nov 5, 2006
9,290 3,065 280
Alikuwa na cheo gani huyo mzee?
Wewe kijana...soma historia ...

Huyu ni Katibu mkuu kiongozi mstaafu...toka enzi za mwalimu...na mara ya mwisho alimsaidia mzee mwinyi ...miaka miwili ya kwanza ya utawala wake.....kuweka muendelezoo...
 
Tiba

Tiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2008
Messages
4,537
Likes
158
Points
160
Tiba

Tiba

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2008
4,537 158 160
RIP Mzee Apiyo. Hawa ndio watu waliofanya kazi kwa uaminifu wa hali ya juu katika nchi hii. Mwalimu Nyerere alikuwa anamuamini sana Mzee huyu. Kwa sasa kuwapata watu kama Mzee Apiyo, ni ndoto.

Tiba
 
Gang Chomba

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
9,067
Likes
960
Points
280
Gang Chomba

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
9,067 960 280
Last time nilisikia huyu mzee analalamika kutelekezwa na serikali
maisha yalikuwa magumu mno kwake...

Sasa kama alistahafu, na mafao yake akapewa...nini kingine alichokuwa anakitaka Mgosingwa huyu?
 
Tiba

Tiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2008
Messages
4,537
Likes
158
Points
160
Tiba

Tiba

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2008
4,537 158 160
The Boss, hicho ni kipindi cha nyuma sana. Serikali miaka mingi imempatia gari na msaidizi wa kudumu na kumsaidia katika matibabu. Hata gharama za matibabu ni serikali imekuwa ikimpatia. Last year or so alipewa gari nyingine mpya Discovery 4.

Kama mapungufu yapo ni ya kawaida.
Nimefurahi na kufarijika kusikia serikali ilikuwa inamjali. He deserved it.

Tiba
 
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
37,824
Likes
23,233
Points
280
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
37,824 23,233 280
The Boss, hicho ni kipindi cha nyuma sana. Serikali miaka mingi imempatia gari na msaidizi wa kudumu na kumsaidia katika matibabu. Hata gharama za matibabu ni serikali imekuwa ikimpatia. Last year or so alipewa gari nyingine mpya Discovery 4.

Kama mapungufu yapo ni ya kawaida.
asante kwa clarification
 
Highlander

Highlander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Messages
3,097
Likes
10
Points
135
Highlander

Highlander

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2012
3,097 10 135
Ndugu zangu

Mzee Timoth Apiyo amefariki dunia usiku wa jana akiwa katika matibabu South Africa katika Hospitali ya Mill Park South Africa.

Serikali ikishirikiana kwa karibu na ubalozi wetu South Africa unafanya mipango ya kusafirisha mwili kuuleta Tanzania.

Msiba upo nyumbani kwake Sitaki Shari.

Poleni sana wafiwa; Clay; Slyvia pamoja na wanafamilia wote.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa.

Rest in Peace Mzee Apiyo. You lived your life kwa uadilifu wa juu.

So sad a remaining example of patriotic honesty in this nation has left us. May this quiet, soft spoken man rest in peace! We will miss you honest builder of our nation. Rest in Peace Mzee Apiyo.
 
Songoro

Songoro

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2009
Messages
4,129
Likes
51
Points
0
Songoro

Songoro

JF-Expert Member
Joined May 27, 2009
4,129 51 0
Afadhali Nafasi imepatikana kwa maana vyumba siku hizi shida sana Dar, watu wakipungua wengine tunapata nafasi ya chumba!

huna haja ya kupiti vipimo unapaswa kuanza Matibabu ya Afya ya Akili ikiwa ni pamoja na sindano za kuzuia kichaa cha Nguruwe mara moja!
 
K

Kuntakint

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Messages
1,515
Likes
990
Points
280
K

Kuntakint

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2011
1,515 990 280
Afadhali Nafasi imepatikana kwa maana vyumba siku hizi shida sana Dar, watu wakipungua wengine tunapata nafasi ya chumba!

Kabla ya kuchangia fuatilia historia ya mtu kuliko kukurupuka. T. Apiyo alikuwa katibu mkuu kipindi cha JK Nyerere na alishastaafu na alikuwa anaishi katika nyumba yake. Ambayo alishindwa hata kuimalizia vizuri pamoja na kuwa alikuwa katibu mkuu kwa kipindi cha miaka kibao. Lakini kutokana na uadilifu wako hakuweza kuvuta hata senti.
 

Forum statistics

Threads 1,272,606
Members 490,036
Posts 30,455,044