Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,270
- 105,441
Kulikuwa na madai ya Mzee Apiyo kutofautiana na Mwinyi mwaka hasa kuhusu teuzi mbalimbali alizokuwa akizifanya Mwinyi ambapo marehemu Mzee alikuwa anawasiliana na Mwalimu kabla ya uteuzi kuwa rasmi. Wapo waliodai kuwa hata Mwinyi alifikia kususa Ikulu na kurudi Zanzibar mpaka marehemu Mzee Thabit Kombo na Nyerere walipoingilia kati na Mzee Apiyo kustaafu rasmi.......in came Paul Rupia
Wengine watasema hizi hata kama si tetesi hapa si mahala pake, hususan wakati huu wa msiba.
Wengine watasema ukweli ni muhimu zaidi ya yote, na obituary nzuri ya uongo ni kumtusi marehemu zaidi ya obituary mbaya ya ukweli .
Kwa wanaosema la kwanza nitawaomba samahani, ukweli utabaki Mzee Apiyo was a Nyerere man and this showdown did actually happen, and what Safari described is accurate, according to various reputable Ikulu insiders.
Pichani naona Pinda kaenda kumuona Mzee wake waliyefanya naye kazi Ikulu ya Nyerere zamani, na Mzee Apiyo kaweka heshima mbele kwa Waziri Mkuu wake.