May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,820
Kwamba maendeleo huletwa na mfumo wa ujamaa au ubepari?. kwamba huwezi kuendelea ukiwa Mjamaa au huwezi kuendelea ukiwa Bepari?. au nini haswa tafsiri ya maendeleo uliyonayo kichwani? maana mimi ninatizama maendeleo kwa mlengo tofauti.Nyerere alikuwa na akili ila akishindwa kutumia akili zake kipindi cha mwisho kuwa na maono juu ya uelekeo wa dunia kutoka ujamaa kwenda ubepari. Kiburi chake ndio kimesababisha hadi sasa tupo nyuma kimaendeleo.
Mimi nilidhani maendeleo ni Elimu ya kujua kwamba nyumba lazima iwe bora, iwe na madirisha ya kutosha, kula chakula bora, kufahamu kanuni za kilimo uvune mazao ya kutosha n.k.
Tatizo hapa ni kutafuta tu Mtu wa kumlaumu kwa matatizo yetu wenyewe....hivi nchi iwe ya kijamaa au kibepari inakuzuia vipi vichwa vyenu kubuni mashine za kubadilisha pamba mliyolima kuwa nguo?.
Kuishi kwa kutegemea akili za wengine kutatua matatizo yetu ndio tutaishia kukaa vijiweni kusubiri Kiongozi anachagua mfumo gani wa kuendesha nchi.
Kiongozi akifanikiwa kusimamia Amani, Usawa, Elimu, Huduma za Afya n.k nadhani inatosha sana tu...tuliobaki tutimize wajibu wetu tutaendelea.