Mzee Mtei hajafilisika mawazo - kasema ukweli

Mzee Mtei amedhihirisha kuwa yeye siyo mnafiki. Akiona cheupe anasema hiki ni cheupe. Hamung'unyi maneno. Nchi hii ina wanafiki wengi kuliko wasio wanafiki. Wanamlaumu Mtei lakini mioyoni mwao wanasutwa na nafsi zao. Ptuuuu!!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tusiwe na tamaduni ya kuogopa maoni ya watu hata kama yanaudhi, ilimradi amebainisha kuwa ni maoni yake binafsi basi tumheshimu na wapo watakaokubaliana nao kama tusiokubaliana nae. usishabikie hoja ya mtu kisa ni ndugu yako au mnatoka kijiji kimoja...angalia uzito wa hoja na kama huoni mashiko basi sema hapana umekosea na ukiweza muelekeze kakosea wapi. Akiendelea kuamini anachoamini basi achana nae songa mbele.
 
Inabidi tuliangalie hili swala objectively. Mimi binafsi siangalii dini ya mtu na kusema ukweli sitarajii kwenye kila kitu Wakristo na Waislamu wawepo 50-50. Ila hapa kuna maswala ya kuangalia.

Je kwa Tanzania ingekua wamejaa Wakristo badala ya Waislamu upande wa pili usinge lalamika?
Je ni lazima kwenye kila kitu tuangalie uiano wa kidini?
Hivi Tanzania dini ni Waislamu na Wakristo tu? Je dini zingine?

Mzee Mtei kakosea kulalamika kwamba kwa nini upande mmoja umejaa Waislamu. Kweli hilo ni kosa. Ila pia najua fika ingejaa Wakristo basi kuna baadhi ya Waislamu wange kasirika. Kwa maana hiyo inawezekana mzee Mtei amenena ambacho wengini tunafikiria hata hivyo kwa maana ana wakilisha mawazo ya wengi japo hawa taki kunena.

Ukweli una baki kuna kaushindani kati ya dini hizi mbili miongoni mwa baadhi ya watu. Kuna watu ambao kwenye kila kitu wanaanza kuhesabu idani ya dini fulani. Lakini watu hawa hawa wanasahau kwamba kuna dini zingine. Mtu ata lalamika kuna Waislamu wachache au kuna Wakristo wachache lakini mtu huyu huyu huto sikia akisema mbona hakuna singa singa, mbona hakuna wahindu nk.

JAMANI WATANZANIA NCHI INA ZAIDI YA DINI MBILI. TUSILETE UNAFIKI WA KULALAMIKA PALE WATU WA DINI YETU WANAPO KUWA WACHACHE WAKATI KUNA DINI HAZI WAKILISHWI KABISA. UKIZINGATIA DINI ZINGINE ZINAVYO PUUZIWA TANZANIA HAKUNA MKRISTO WALA MUISLAM MWENYE HAKI YA KULALAMIKA DINI YAKE INAONEWA.
 
Kama mchangiji mmoja hapa alivyochangia,Zanzibar kuna makanisa ambayo mengine yana umri mkubwa kuliko hat yaliyopo bara.Sasa swali hakuna hata member mmoja wa hayo makanisa ambaye angeweza qualify kuwepo kwenye hii tume ya katiba? Kama yupo au wapo,wanatambulika kwenye mambo gani muhimu ya nchi hii.Ukubwa dawa ndugu zangu,huyu mzee yamkini kwa kuujua vyema uwezo na dhamira ya mteuaji(kutokana na uzoefu wake) ndo maana akaja kihivi.Nachelea kumkosoa kwa sababu naweza nikawa sijaona anachoona.Na huyu ni mmoja ya wazee ambao nadiriki kusema ni hazina ya nchi kwa mchango wake ktk siasa za mageuzi nchini,na jinsi alivyokuwa na uwezo mkubwa wa kusomana na Mwl.Nyerere,na hata jinsi Nyerere alivyokuwa akimkubali huyu mzee Mtei.
 
Hivi tujiulize waislam ndo wangekuwa wachache kwenye hiyo tume ingekuwaje? Kwa nii waislam wanajiona wana haki zaidi ya wengine? Mbona kila siku ndo kilio chao cha kutaka usawa? Iweje wamshangae Mzee Mtei kuongelea usawa huohuo wanaoupigania kila kukicha?
 
Kinacho nisikitisha mimi mkereketwa wa Chadema ni kwanini Mtei amefikiria kwenye Ukristo na Uislam?
 
On my dead body mpango wake wa kuleta Mahakama ya kadhi na OIC hautafanikiwa Tanganyika.
 
JAMANI WATANZANIA NCHI INA ZAIDI YA DINI MBILI. TUSILETE UNAFIKI WA KULALAMIKA PALE WATU WA DINI YETU WANAPO KUWA WACHACHE WAKATI KUNA DINI HAZI WAKILISHWI KABISA. UKIZINGATIA DINI ZINGINE ZINAVYO PUUZIWA TANZANIA HAKUNA MKRISTO WALA MUISLAM MWENYE HAKI YA KULALAMIKA DINI YAKE INAONEWA.

Hao wa dini zingine hakuna aliyewazuia kulalamika.

JK analeta udini Tanzania, lazima akemewe kwa hali zote
 
Tatizo letu sisi ni kwamba tunakata matawi halafu tunategemea mti utaanguka!!!!! Hakuna hata chama kimoja cha siasa kilicho serious. Vyote ni matapeli na wasanii tu wanaojipanga kuendelea kuwadanganya watanganyika kwa zamu. Hivi kwa nini hamna hata chama kimoja cha siasa kilicho serious kinachotambua kwamba nchi yetu ya Tanganyika haiwezi kuendelea katika mfumo huu wa muungano? CCM inaeleweka wanataka serikali mbili. Vyama vingine vyote vya upinzani vilivyo serious vinataka serikali tatu. Hiyo serikali ya tatu ya nini kama si kuzidi kufuja hela za Watanganyika ambao tayari wanastahili kuitwa watangahoi?

Sasa haya mambo lazima tuyakubali kwa sababu Zanzibar ni nchi inayojitegemea iliyoungana na Tanganyika. Hatuwezi kuwapangia wamlete nani kwenye kamati za mambo ya muungano.

Nataka kiundwe chama ambacho ni serious. Chama kinachoelewa kwamba bila kuvunja huu muungano feki basi Watanganyika hawatakuja kujikwamua kiuchumi milele.
 
Nilitegemea pia na wengine.Rais hakuliona hili kwani kimtazamo watanzania wengi tupo too simple minded kiasi tunadhani hata common sense ni lazima iwe true.Serikali makini inalinda minority.Wel, Jaji Ramadhani anaweza wakilisha wakristu au serikali kwani pia ni mcha Mungu ,Ila sijui uwepo wake ulibase ktk uwezo wake au dini yake?Pengine serikali ilipaswa wasogeza angalau kwa uwiano wa asilimia ya wakristu zanzibar.Sijui Sikhs,Hindu, etc kwa Visiwani.Ila bara wapo.Pia makabila yaliyopigwa marufuku ktk kampeni za 2010 kutawala nchi ..teh teh.
 
Kiby,

Hili ni swali ambalo wengi hawataki lijadiliwe hapa.
Wengi wamekimbilia tu kumlaani mzee Mtei bila
ya kujadili kile alichosema kama kina ukweli au la

Ukweli ni kuwa JK ni mdini - sasa ameanza kujionesha
wazi wazi.

Ukweli pia ni kuwa, kama angekuwa Mkapa ndiye kateua
tume ya katiba na akaweka wakristo wengi kuliko waislam,
maandamano yangekuwa ndio chakula cha mchana na jioni
kwa wakazi wa Dar.

Ndugu,
Unafikiria mwenyewe au kuna mtu anafikiri kwa niaba yako? Nakuuliza kitu kimoja ukiweke wazi hapa jamvini. Marais walotangulia walishaunda tume nyingi sana ,na hata ikiwemo pia tume ya marekebisho ya katiba. Unakumbuka uwiano kati ya waislam na wakristo ulikuwaje?,ili tutumie kuwa reference JK kateua tofauti na wenzake?
Tume inaundwa na wakristo wengi zaidi bara kuliko waislam. Huu udini unatoka wapi? Au kwa tafsiri yako ni sawa na ile ya wengine hapa JF kuwa muislam ni mdini.(Maana kwa hapa JF inaeleweka mdini maana yake ni muislam) Haijawahi kutokea mkristo akaitwa mdini. Na ndio maana kauli ya udini kaitoa Mtei lakini hajaitwa mdini, lakini ambaye Jk ni mdini kwa kuwa ni muislam. Chukua muda kidogo kufikiri,once in yor life time, pengiune huna kawaida ya kufikiri kabla ya kuandika au kusema..
 
Aah! Hii ishu ya katiba ni sensitive sana,najaribu ku imagine kama oic na kadhi vitatakiwa kupigiwa kura miongon mwa wajumbe wa tume hii,unafikiri lipi litapitishwa?
 
Ninaamini wazi kuwa Edwin sasa ndio anashituka na kuona hilo na kuepuka ile tarbia ya wengi Tanganyika ya kuficha ukweli ima kwa sababu zako binafsi au kwa maslah ya kutaka kupumbaza WaTanzania. Naomba kukujuza kuwa siku zote lisemwalo Lipo na kama halipo Laja.

Ningependa nikurejeshe kwenye Historia za Ukoloni ndani ya Afrika mashariki kwa maana nitakudadavulia nchi kuu nne yaani Tanganyika, Kenya , Uganda na Zanzibar.

Naomba ujue kuwa wakoloni walitumia devide and Rule system katika kutaka kututawala. Tukianzia na Kenya na Uganda huku waliona kila nchi moja ilikuwa na makabila machache. Hivyo ndani ya Uganda na Kenya walitumia kuwagawa kwa njia ya Ukabila. na hicho kitu mpaka leo kenya na Uganda limkuwa tatizo kuu kwao kila kabila linajiona bora kuliko lingine na kila kabila linajinasibu kwa lugha yake ukilinganisha na lingine. Hayo ni makovu ya utawala wa mwingereza na mambo ambayo yanaendelea mpaka leo.

Nikija Tanganyika. wazungu hawa waliona kuna makabila mengi sana zaidi ya 50 hivyo wasingeweza kutawala kwa kutumia sstyle ya kenya na Uganda. Hivyo huko walitumia style ya UDINI kwa maana ya Ukristo na Uislam. Hapo Wakristo walipewa nguvu nyingi na elimu kiasi cha kujiona wao ni first citizen ukilinganisha na waislam. wao ni wasomi zaidi kuliko waislam kitu ambacho mpaka leo wakristo wanajiona bora na wasomi zaidi ya waislam.

Sasa utaona suala la UDINI Tanganika ni kovu la utawala wa kikoloni ambalo sio rahisi kulificha. kama unataka kubaini hili soma kitabu cha Padre Dr Silvalon kinachoitwa '' kanisa katoliki na siasa za Tanzania bara 1953-1985'' utaona mengi sana.

Sasa hilo sio tu la kulifumbia macho bali ni kulitafutia ufumbuzi kwani nao waislam wamesoma na kuelimika japo kwa uchache wao na kufanya mgawanyo wa rasilimali za taifa lenu mzigawe kwa uwiano ulio sawa na si kwa mmoja kujiona ni Bora zaidi ya mwengine au hata dini moja kujinasibu kuwa ni bora na imesoma na kuwa na wasomi wengi zaidi ya nyengine.

 
Back
Top Bottom