Mzee Morris Nyunyusa; Historia itamkumbuka

Mzee Morris Nyunyusa; Historia itamkumbuka

Natamani japo wafanyakazi wachache wa TBC au hata waziri husika alione hili. Nimeona fursa hapo kuna baadhi ya vitu vinapatikana TBC tu ila sina hakika sana na utunzaji wake kama uko vizuri isije ikawa yote haya uliyoyataja yametupwa store iliyojaa mende na mazalia ya panya

TBC ina maktaba kubwa zaidi ya sauti kwa afrika mashariki, na kusini kama sikosei,

Historia ya mzee moris nyunyusa ilielezewa katika kipindi cha Star Special cha TBC TAIFA kinachoruka kila jumamosi kuanzia saa kumi na robo jioni, nakumbuka hadi mwanae morris alikuwepo kwenye kipindi akamuelezea vizuri sana mzee wake.

Si huyo tu hata yule mzee mkali wa kuchora picha ambazo zina umaarufu zaidi duniani kutokea kusini mwa tanzania Mzee Said.. Almaarufu TingaTinga
 
Kama dada yangu Sango na kaka Kipozi wanapitia humu, hebu ishauri idara hii. Hao ni watu ninaowafahamu vizuri ila kuna watangazaji kama Charles Hilary bado wana ushawishi kwa wasikillizaji wa nchi hii popote pale, Hivi Charles Nyaisanga yupo bado?
Alishatuacha mkuu, alikuwa anafanyia kituo fulani huko Morogoro na ndiko alokofia! R.I.P
 
Yeah ikiwemo historia yake kamili alikozaliwa elimu yake mafanikio yake ndoa na familia na hata mwisho wake hii kitu ni muhimu mno kuna watu ngoja nione kama wanaweza kutoa msaada kwenye hilo
niah 1954 Guasa Amboni wengine siwezi kuwakumbuka kwa haraka
Shukran kwa kuniita penye huu uzi kuna mada tulikuwa tunachangia nimeisahau ila nilileta mfano kuhusu mzee huyu kuwa kasahaulika na kuna kipindi familia yake walikuwa na malalamiko yao sijui iliishaje! Sasa kizazi hiki cha. Com hawataweza kumjua ila mbaya zaidi wizara ya habari na utamaduni kama bado inaitwa hivyo maana siku hizi majina ya wizara yanabadilika kutokana na mahitaji wangekuwa mbele kuweza kuwaenzi wazee hawa kina Mwinamila na wengine wengi mtu asikilize kibao cha maonyesho ya Japan atamjua mzee nyunyusa ni nani.
 
Nchi hii ina utajiri wa vitu vingi kama TBC ingependa kujiendesha isingekuwa na haja hata ya kufunga vipindi vya bunge ambavyo ni muda mchche kwa mwaka. Imagine unaweka mikanda ya vita vya Msumbiji ambavyo hata mzee Nnauye alishiriki kuhamasisha huko, vita vya Kagera, matukio kama ya wakati papa amekuja Tz wangeuza kila kanda. Hawa watu wamekalia pesa hawana uchungu. Watu tunaangaika kutafuta miziki ya Nuta, Afro Band 70, Kilwa jazz, Tabora jazz, Makongoro music, Mzee Makasi wakati ule hajaokoka akiwa na Remmy, na miziki yote ile ya sixtees mpaka utanda wazi ulipokuja. Tunapenda vile vile kupata kanda za michezo ya Radio Tanzania ya kila J. mosi nathani mchezo ambao siwezi kusahau ni "Mkataa Pema, pabaya panamwita", Akina Pwagu na Pwaguzi nakumbuka tukio la kuuza senene wakauza na wadudu wananuka pwagu akasema hawanuki haoo. ( kwa sauti ya kisambaa). Jamani turudishieni ya zamani watoto wetu wajue ustarabu tuliokuwa tumefikia. Tumerudi nyuma kihistoria na kiutamaduni. Kizazi cha zamani tulikuwa tunawekewa ngoma za makabila na mila zao siku hizi ni akina diamond. Sidhani kama mzee Moris aliweza kanyaga Ikulu pamoja na kuliwakilisha taifa nje kwa ngoma zetu pamoja alikuwa kipofu. Rais Magufuli nenda Redio Tanzania waambie wachapishe na kutoa maigizo, nyimbo na video za zamani ili wajiendeshe wenyewe.
Swadakta leo kipindi cha mkoa kwa mkoa sijui bado kipo? maana waqt ule utapata kusikia nyimbo mbalimbali kwa mfano kila munu avena kwao kisha mtangazaji anakunyogolea mawili matatu kuhusu huo wimbo sasa vya kwetu hakuna na uzee wetu huu tunachezeshwa ngololo sijui sikileu aah waqt umekwenda wapi? Vipindi kama kombora au ombi lako vilikuwa matata sana huyo pwagu ndo usiseme humuoni ila unacheka jamani mbavu zangu ooooooh jamani mbavu zangu ooooooh leo hawa tunaowana hawachekeshi pamoja na uanaume wao wote na vimini wanavaa na kifuani wameweka vifuu vya nazi bado hawachekeshi.
 
Mshana jr ndomana ukipotea jf hata kwa siku moja watu hujiuliza maswali mengi,,,,,ahsante kwa kumbukumbu hii.
 
Hii ndio Tanzania.Labda angekuwa mwanasiasa maarufu wa Kijani na Njano angekumbukwa.Sio Mzee Nyunyusa tu,hata marehemu Omari Kungubaya naye kafa maskini mno.
 
Inawezekana kabisa ni kweli kwakuwa mara ya mwisho kusikiliza hiyo redio sikumbuki ni mwaka gani nitafanya hivyo jioni ya leo nihakikishe mwenyewe
Hiyo midundo ni kweli bado inatumika TBC saa 2 Usiku
 
alimfundisha pia kijana mdogo hv anaitwa Manyama nae yupo vizur sana kwenye kupiga hiz ngoma sijui Yuko wapi siku hiz huyu dogo last time nlimuona tamasha la sanaa pale bagamoyo miaka 2 hv nyuma
 
Hata TvT ilivyoanzishwa waikuwa wanaiweka wakati wa taarifa ya habari ya saa 2 usiku. Mi wananikela sana hata Tbc kubadili na kuweka miziki mingine. Mbona msumbiji wanaenzi ngoma za asili hadi leo. Msumbiji watu mashuri wa zamani bila kujali fani wanaenziwa sana. Why Tz?
 
Nakumbuka maonesho Japan yalivofana jukwaa la watanzania lilivutia sana because of this man '' Mzee moris''
 
Kama dada yangu Sango na kaka Kipozi wanapitia humu, hebu ishauri idara hii. Hao ni watu ninaowafahamu vizuri ila kuna watangazaji kama Charles Hilary bado wana ushawishi kwa wasikillizaji wa nchi hii popote pale, Hivi Charles Nyaisanga yupo bado?

mshana jr....Julius alitangulia/ametangulia mbele za haki ambako wote tutakwenda kila mtu kwa wakati wake.....
 
Mmh Nyaisanga sina hakika sana yuko wapi lakini kama hao uliowataja wapo hapa ngoja tuone reaction yao
Kwani nyie mnaishi dunia gani? Ancle Julias Nyaisanga alishaaga dunia kama miaka mitatu iliyopita,alikuwa CEO wa Aboud Radio morogoro
 
Back
Top Bottom