Hujanielewa kitu gani?mleta mada ni kama sijakuelewa ulitaka mzee awe mme mwenza au ulitakaje mkuu?
Alimsamehe ila hakutakabkurudiana naye ikumbukwe kusamehe si lazima kurudiana moreover inawezekana kua alimwachia aliyekua anamiliki wakati huo aendelee kujilia vyake
mandela kashakufa, jadili yalio hai haitakusaidia kitu
WanaJF, ni wazi kwamba makaburu walimfanyia kitu mbaya sana Mze Nelson Mandela kwa kumswenka ndani ya jela takribani kwa nusu ya maisha yake na kumfanyisha kazi ngumu. Mzee huyu alidhalilika, alipuuzika, malengo yake yalionekana kupotea na akanynyapariwa sana. Jambo zuri Mzee huyu aliamua kuwasamehe watesi wake (Makaburu) kwa lengo moja tu la kuijenga south afrika moja isiyokuwa na ubaguzi wa rangi, inayojali haki kwa wote na kweli hilo alilitimiza. Wanadunia wote tumeaswa kuenzi na kuiga kusameheana kama alivyofanya Mdingi huyu na hapa namkumbusha hashwa Rais wa Rwanda Paul Kagame ajifunze kusamehe na hili alazimike kukaa meza moja na waasi wa FDLRA wayazungumze na kuamaliza. Back to my point; katika kusamehe kwa Mzee Mandela kuliingiliwa na dosari moja ya kutomsamehe mke wake Winnie kwa kosa linalosemwa la kutoka nje ya ndoa. Hili Mzee hakulisamehe kwake ni zaidi ya kukaa jela miaka 27 na kazi ngumu. Tumeelezwa tujifunze kutoka kwa Mzee Madiba, hili nalo tulichukue?? hivi kusalitiana hakusameheki???Nimeamini kufanyiwa kubaya. WanaJF, nimechokoza tu lete mauzoefu yenu na maono yenu na wenye nondo zaidi bandikeni
Hili linaukweli...kwa kufahamika sio siri Michael Jackson anafahamika zaidi ya Mandela...tena saaaaana aisee hili huwezi pinga hasa tukiliongelea kwa Dunia nzima...Michael mbali sanaKuna watu hawamjui Mandela usione wewe unatazama TV unamjuwa kuna watu hawajui TV ni nini.
Hata useme nini, mimi naamini Michael Jackson anajulikana zaidi ya Mandela. Wengi wamemjuwa Mandela baada ya kutoka jela na si kabla, Michael Jakson ni maarufu kwa kui entertain dunia. Mziki hauna rangi hauna siasa hauna kabila hauna lugha.
Kuna watu duniani siasa hawana habari nayo kabisa, lakini nani asiye na habari na mziki? hata kama hapendi atausikia tu japo kwa mbali.
Hili linaukweli...kwa kufahamika sio siri Michael Jackson anafahamika zaidi ya Mandela...tena saaaaana aisee hili huwezi pinga hasa tukiliongelea kwa Dunia nzima...Michael mbali sana
Michael J hata alikua akienda Korea watu wanazimia..... umaarufu wake haukuwa wa kawaidaWakati wengine wanajipeleka kujipendekeza, Mandela mwenyewe alimualika MJ kwenye BD yake.