- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Disemba 03, 2025 Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku aliandaa kongamano la amani na kuzungumza masuala mbalimbali kuhusiana na jambo hilo.
Madai
Kupitia mitndao mbalimbali ya kijamii ikiwemo X na Instagram kipo kipande cha vide kinachomuonesha Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungumza na waandashi wa habari. Kipande hik pia kimeambatana grafiki yenye ujumbe unaosomeka;
Mzee Butiku - #D9 maandamano yapo tutake ama tusitake vijana msifanye vurugu tuandamane kwa amani
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo na kubaini inapotosha uhalisia.
Ufuatiliaji umebaini kuwa kipande hiko cha video kimekatwa kutoka katika video ya awali na hivyo kuondoa baadhi ya sehemu na kupotosha uhalisia kwa kuleta maana tofauti.
Video halisi ilichapisha na Global online TV kupitia Chaneli yao ya Youtube December 3, 2025 ambapo wapotoshaji walikata kipande cha mwanzo na kuharibu maana. Butiku alisema kuwa;
Na yapo mazungumzo ya vijana kutokana na makundi yale yale ya vijana kwamba tarehe 9, maandamano yapo tutatke tustake
Hivyo mzee Butiku alieleza kuwa amesikia kuna tetesi za maandamano December 9 yaliyopangwa na vijana wanaosisitiza kuwa maandamano yapo watake au wasitake na si kuwa mzee Butiku yeye ndiye anayedai kuwa maandamano lazima yawepo.