Mzee aiba pesa na kuzitoa kama zawadi akisema 'Merry Christmas'

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
1577285425780.png

Bwana mmoja mwenye ndevu nyeupe alifanya uvamizi wa benki siku mbili kabla ya Krismasi na kuzirusha juu kwa furaha na kuwatakia kheri ya siku kuu wapita njia, mashuhuda wameeleza.

Polisi wamethibitisha "mwanaume mzee wa kizungu" alivamia benki ya Academy mjini Colorado Springs, Marekani siku ya Jumatatu.

"Aliiba pesa benki, akatoka nje na kuzitawanya kwa watu," shuhuda Dion Pascale alikiambia kituo cha Colorado's 11 News.

"Alianza kurusha fedha kutoka kwenye begi na kisha akaanza kusema, 'Merry Christmas!'"

Kwa mujibu wa mashuhuda, mtuhumiwa huyo akapiga hatua chache kutoka benki na kuketi mbele ya mkahawa wa Starbucks akisubiri kukamatwa.

Katika hali ambayo inaweza kuwa ya kustaajabisha kwa wakazi wa Afrika Mashariki, wapita njia wanaripotiwa kuwa walichota fedha zote zilizozagaa na kuzirudisha benki.

Polisi wamemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la David Wayne Oliver, mwenye miaka 65.

Polisi hawadhani kuwa alikuwa na usaidizi wowote.


BBC swahili
 
Duh! Ama kweli wazungu wametuzidi vingi! Raia wa Bongo waokote pesa na kuzirudisha Benk?
 
Mwanaume mmoja aliye fahamika kwa jina la David Wayne Oliver, mwenye umri wa miaka 65 alifanya uvamizi katika benki siku mbili kabla ya Krismasi na kuzirusha fedha juu kwa furaha na kuwatakia kheri ya siku kuu kwa wapita njia.

E1pi2DpQ05Zxb5juhQznSjzbuRhW8FOkIr1UeB_5bnPXAQk3tVQT72zFVo4LvUX6nLvVCVZIWjClRYR6By-cl-Gq2My7ZIwbrNVi_gOyeqT3UcmhGkVyJnxeYC7hUFHQjp4rAnZS-noguic=s0-d


Polisi wamethibitisha mwanaume huyo kuvamia benki ya Academy mjini Colorado Springs, Marekani siku ya Jumatatu.

“Aliiba pesa benki, akatoka nje na kuzitawanya kwa watu,”Shuhuda Dion Pascale alikiambia kituo cha Colorado’s 11 News”

kwenye begi na kisha akaanza kusema, ‘Merry Christmas!'”

Kwa mujibu wa mashuhuda, mtuhumiwa huyo akapiga hatua chache kutoka benki na kuketi mbele ya mkahawa wa Starbucks akisubiri kukamatwa.

Katika hali ambayo inaweza kuwa ya kustaajabisha, wapita njia wanaripotiwa kuwa walichota fedha zote zilizo zagaa na kuzirudisha benki.

Polisi wamemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la David Wayne Oliver, mwenye miaka 65.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom