Mzanzibari haswa ni mtu aina gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzanzibari haswa ni mtu aina gani?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Geza Ulole, Jan 24, 2012.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  Wana JF,

  Imefika wakati sasa kuanza kuhoji nani haswa ni Mzanzibari Asilia kihistoria maana tunakoenda sasa si huko na katika kujua haya inatupasa kupitia historia yetu hata kabla Waajemi na Waomani hawajatua Zanzibar yaani wakati huo visiwa hivi vikiwa na majina ya Kiasili ya kiafrika yaani Unguja n.k. na pia kipindi cha Wareno pia kipindi cha Wajerumani hadi Waingereza na pia siasa na utaifa wa Kizanzibari baada ya uhuru na mapinduzi ya Zanzibar

  Tuanze na historia ya Unguja kabla ya mwarabu kuja; inasemekana kulikuwa na waafrika (ngozi nyeusi) wakiishi huko wengi wao walikuwa ni wale wavuvi wanaotoka pwani ya Tanganyika wakiienda huko kutokana na shughuli za uvuvi na hata baadhi yao kuwa na makazi yao huko na pwani pia; watu hawa walikuwa na dini za kiasilia wakifanya matambiko na yale yote yanayofanywa na wenzao wa Pwani yaani makabila ya Pwani kiutamaduni.

  Haya yote yalianza kubadilika pale Mwarabu toka Oman alipotia nanga katika visiwa vile kwani utawala wa Asili haukuwa na nguvu ya kumzuia Mwarabu kufanya anachotaka maana alikuwa na silaha za kivita yaani bunduki iliyokuwa bora zaidi ya mkuki, mshale au sime. Kwa mantiki hiyo basi uhuru wa Mwafrika halisi ukapotea pale tu Mwarabu alipotia mguu katika visiwa vile. Mbali na hayo biashara haramu kama utumwa ilianzishwa na Mwarabu na pia biashara ya pembe za ndovu zilizomlazimisha kwenda hadi Ujiji kusaka vipusa hivyo. Kutokana na kushamiri kwa biashara hii ya utumwa na ndovu; visiwa hivi vilitamanisha watu wa mataifa mbalimbali haswa Mashariki ya Mbali hata kusababisha Sultan wa Oman kuamishia makazi yake. Na pia wale wa Magharibi kama Wareno, ambao nia na madhumuni yao yalikuwa kuhodhi biashara ile, matokeo yake mikanganyiko wa kujaribu kuhodhi dola ikawa ni jambo linalojirudia rudia katika jamii hii yenye mseto wa asili yaani Uarabu, Ubantu, Uajemi na Uhindi.

  Japokuwa watu wa mataifa mbalimbali wamepita au wameweka maskani Zanzibar, Mwarabu mbali ya kufanya biashara alifanikiwa zaidi kusimika tamaduni zake katika visiwa vya Zanzibar kuliko mataifa yoote yaliyopata kuwapo ambayo yaliwekea uzito suala la biashara kuanzia Wareno na pia Wajerumani na Waingereza ikiwemo ya mali ghafi kwa wale wa nchi za Magharibi haswa kipindi cha Mapinduzi ya viwanda huko kwao!

  Historia hii itaendelea.....
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  mkuu nasubiri muendelezo wa hii story
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  unajua majina ya ubin(surnames) ya wazanibar? mostly ni ya wabantu wa bara,wavuvi na makuli walioenda kukutana na ustaarabu wa kiarabu na kuchanganya damu
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu nadhani swala hili linatoafsiriwa na WaZanzibar wenyewe maana hata ukiniuliza Mtanganyika ni nani itakuwa kazi kubwa!.. waache wenyewe wajitambulishe na watagombana wenyewe nani Mzanzibar na nani siye!
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  :peace: be with you!!
   
 6. Wisdom

  Wisdom JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 473
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengi wao hawajui hata asili yao, kuna jamaa mmoja anajiita yeye ni mzanzibari nilifanya naye interview katika shirika fulani la Umma hapa Dar na kwa bahati nzuri wote tulipata kazi katika kuja form mbalimbali kuna form mija ilikuwa na sehemu ya kujaza kabila, jamaa hakujaza kwa kuwa hajui kabila lake na hajawahi kubother kutafuta, mpaka leo ile nafasi iko wazi haijajazwa kabila lake, He was very honest kwamba hajui kabila lake.
   
 7. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ukiweza kumjua Mzanzibari bari itakuwa rahisi sana kumjua Mmarekani. Hili ni somo la kihistoria ambalo litakuchukua muongo zaidi ya mmoja kuweza kujua nani ni mzanzibari. Ni somo ambalo litakufanya usafiri kwenye pwani yote ya zanzibari ili uchukue historia na hutaishia hapo itakubidi uende lamu, oman, uajemi, uchina, ujapani, msumbiji, somalia na ureno ili ukatafute historia je hawa watu kutoka sehemu tofauti tofauti walio kuwa wanaenda zanzibar kufanya biashara waliwakuta waenyeji walikuwa ni kina nani? Maani tunaambiwa
  Utaona kwenye maelezo ya hapo juu biashara zanzibar ilianza kufanyika kwenye karne ya 15 sijui wakati huo sisi huku kwetu tulikuwa tunafanya nini? kwenye karne ya 15 sijui miji kama dodoma, singida na shinyanga ilikuwaje?

  Kikubwa hapa ni kuwa wazaznibar wana historia ndefu sana inambidi mtu alie somea historia afanye thesis ya historia ya zanzibar ili kuweza kumjua nani ni mzanzibari.
   
 8. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Shirika fulani la umma halipaswi kuuliza watu kabila zao wala dini zao! hizo details hazisaidii kwenye kuleta tija sehemu ya kazi. Kwa taarifa za mfanyakazi umri, mahali alipozaliwa, mwaka, majina yake, elimu yake na uraia wake ndio vyenye umuhimu.
   
 9. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Bila ya kutafuta makabatini, kwa kifupi Mzanzibari ni kila mzaliwa wa Zanzibar. Unaweza kuongeza vizazi viwili vitatu nyuma, kwa maana ya kuwa ikiwa babu na bibi yake mtu alzaliwa Zanzibar, inatosha kumfanya, kwa sifa ya uzawa wake, kuwa huyo ni Mzanzibari.

  Kwa maneno mengine, kutokana na historia na jiografia ya Zanzibar, Wazanzibari ni mchanganyiko wa watu wenye asili tafauti (Watanganyika, Wakenya, Wakomoro, Wamakonde wa Msumbiji, Wahindi, Waajemi, Waarabu, Wachina...). Kuhusu hawa mwisho, kule Mkoani Pemba na Malindi Unguja, kuna Wachina wa zamani hata kabla ya kuja Waarabu; kwenye Msitu wa Ngezi/Kiuyu Pemba na Dole Unguja, kuna Wamakonde wa hata kabla ya Wareno. Makunduchi kuna Makumbaro (aina ya Wahindi) hata kabla ya Sultani; Kizimkazi kuna watu wenye asili ya Bagamoyo hata kabla kuja Mjerumani.

  Hawa wanazuka leo na kusema asili ya Zanzibar ni Watanganyika au Waarabu, Waislamu au Wakristo, hiki ni kizazi cha watu muflis wa mawazo, kwani Zanzibar ina michanganyiko yote hiyo. Kwa hivyo, ama Zanzibar ni ya wote au si ya yeyote.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,898
  Trophy Points: 280
  Wazanzibari wengi wao ni waarabu, hata wale weusi kama mimi wanajitambulisha kama "waarabu"


  Nina rafiki yangu Mzenji sijui kama anaifahamu hii forum, ngoja nimtumie hii linki pengine atakuwa na mawili matatu.

  Ila nadhani wazanzibari wanaji "nasibisha" zaidi na waarabu kuliko wabantu.

  I stand to be corrected.
   
 11. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kitu kimoja ni mtu "kujinasibisha" yeye mwenyewe, kwa utashi, maslahi, mapenzi yake; kitu chengine ni asili ya mtu.

  Kunaweza kuwa na ukweli kuwa wengi wao wana asili ya Kiarabu kwa sababu wazee wao walitoka huko, au wana damu ya ya mchanganyiko na Waarabu kutokana na maingiliano ya ndoa. Lakini bado, kwa mtoto/mtu ambaye ana damu asili/damu ya Kiarabu, lakini hajui lugha wala utamduni (hapa naweka dini upande ili nisiingie katika makosa ya kuinasibisha dini ya Kiislamu na Uarabu - wapo Wachina Waislamu) wa Kiarabu, hawa wanaeweza kujinasibisha lakini hakuwafanyi wawe Waarabu per sey. Masikini hawa, hata huko wanakojinasibisha nako hawakujui, hawajawahi kufika, hawajulikani. Ni sawa na Mmakonde (au ethnic group yoyote) wa leo wa Zanzibar kujinasibisha na Msumbiji (au popote pale) wakati huko hawamjui wale yeye hakujui.

  Na mimi pia ni mawazo yangu tu, niko tayari kufahamishwa kwa hoja.
   
 12. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Umenena vema wazanzibari ni wale wazaliwa wa zanzibar bila kujali ametoka wapi
   
 13. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  mkuu,
  ukiweza kujua mtanzania ni nani utaweza kujibu swali hili la mzanzibari.
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni Mwanadamu aliye Mwenye rangi ya brown aliyetoka bara, alichukuliwa bara kama Mfanyakazi au Mtumishi au Mtumwa lakini akapendwa na Bwana yake (Kiongozi wa anayewatunza hao watumwa) na kuwabakisha na kuwapa haki kidogo baada ya Mfalme kupewa nchi na Waingereza alihakikisha wanafuata DINI yake ya KIISLAMU na pia kwasababu waarabu walikuwa wachache walitumia system inayoitwa ASSIMILADO - ni ya kofauti uwafanya waafrika wa huko kufikiri kama wao ni waafabu kiutamaduni , kimazingira, kula na hadi jinsi ya kuongea na hadi damu yao na ya kiarabu ni sawa tofauti ni rangi za miili yao kuwa tofauti lakini kila kitu ni sawa huko Zanzibar.

  * ASSIMILADO System also inahakikisha unasahau ulikotoka kwahiyo watoto wako kama ulitoka bara hauwaambii historia yako; Wanaishia kutokuwa na makabila, saa nyingine kuwa na kabila inasaidia. Mila za makabila ni nzuri zinakujenga kuwa bora halafu baadaye ni dini zenu.
   
 15. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,313
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160

  [video]  http://www.mzalendo.net/habari/video...tu-wa-zanzibar[/video]
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
Loading...