Muungano Huu Shaghalabaghala: Mzanzibari ni Mtanzania, ila si kila Mtanzania ni Mzanzibari

Muungano Huu Shaghalabaghala: Mzanzibari ni Mtanzania, ila si kila Mtanzania ni Mzanzibari

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
217
Reaction score
860
Kumekuwa na kauli tata kutoka kwa viongozi wa Zanzibar kuhusu Muungano, wakionyesha ubaguzi wa wananchi kutoka Bara kupata huduma au kushiriki fursa za kiuchumi, hali inayozua maswali.

Kauli hizo zimekuja wakati kukiwa na mjadala wa kwa nini raia wa upande mmoja (Tanzania Bara/Tanganyika) wanapokumbana na milango iliyofungwa au vikwazo wanapokwenda upande wa pili (Zanzibar), huku Wazanzibari wakifurahia uhuru mkubwa upande wa Bara.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka 1964 na kuzaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika kwa kudumisha amani na utulivu.

Hata hivyo, ukiacha picha ya nje ya "Tanzania Moja," kiuhalisia kuna mambo mengi ya kiutendaji, kisheria, na kiuchumi yanayouanya muundo huu kuonekana wa kusuasua—au kwa lugha rahisi, shaghalabaghala.

Sekta ya Afya: Vikwazo vya Vitambulisho vya Matibabu

Kauli ya hivi karibuni imetolewa na Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum aliyekuwa akijibu hoja kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar Juni 9, 2026 akisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kugharamia matibabu kwa Watu wasio Wazanzibar.

Waziri Saada alisema kupitia Mfuko wa Huduma za Afya wa Zanzibar (ZDHSF), wanaotakiwa kuhudumiwa ni Wanzibari peke yao.

Alieleza kuwa bajeti ya Zanzibar ya takriban Sh8 trilioni haiwezi kubeba mzigo wa kutibu watu milioni 60 wa Tanzania nzima.

"Mtu ambaye si Mzanzibari, anakwenda katika hospitali zetu, anaonyesha kadi ya matibabu... Sasa hivi tunataka yeyote anayekuja na kadi ya matibabu inayotolewa kupitia Sheha wake, athibitishe kuwa yeye ni Mzanzibari kwa kuonyesha Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi (ZANID)."

Hatua hii inamaanisha kuwa utambulisho wa "Utanzania" pekee hautoshi kupata huduma za afya visiwani humo, jambo linalokiuka dhana nzima ya udugu wa Muungano.

Soko la Ajira na Uhifadhi wa "Wazawa"

Kauli nyingine ilitolewa na Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji wa Zanzibar Hassan Khamis Hafidh, wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi Bajeti ya Vijana katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Juni 6, 2026, akisema licha ya visiwa hivyo kuwa na hoteli nyingine za utalii, walioajiriwa ni wageni (kutoka Bara).

“Zanzibar nzima kuna hoteli zilizosajiliwa 1,184, hoteli zilizosajiliwa, zipo na ukienda mheshimiwa Spika, wanaofanya kazi katika hoteli zile sio wazawa kweli. Ukweli nani anabisha?

“Sasa jukumu letu kama Wizar aya Vijana ni kufanya mapinduzi kwamba sasa waliokuwemo mle sio wazawa, wawe wazawa. Mniachie kazi hiyo naiweza,” alisema.

“Jukumu la Wizara hii ya Vijana ni kuhakikisha vijana wanapata kazi katika mahoteli,” aliongeza.

Alitoa mfano wa hotelimoja visiwani humo, akisema ina wafanyakazi wafanyakazi 156, ambapo kati yao vijana wa Kizanzibari walikuwa 27.

Hoja hiyo pia imezua mjadala kwamba, mona Wazanzibari wapo Bara na wanapewa ajira bila upendeleo bila kuulizwa wanatoka wapi?

Umiliki wa Ardhi

Moja ya kero kubwa inayozua maswali kuhusu usawa ndani ya Muungano huu ni suala la umiliki wa ardhi. Wazanzibari wana haki ya kununua, kumiliki, na kuendeleza ardhi upande wa Tanzania Bara bila masharti yoyote magumu, kama raia wengine.

Hata hivyo, hali ni tofauti kabisa kwa Mtanzania wa Bara anayetaka kumiliki ardhi Zanzibar. Kisheria, mtu asiye Mzanzibari hawezi kumiliki ardhi kwa 100%.

Akizungumza katika mahojiano kuhusu muungano Aprili 16, 2026, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alisema kuruhusu kila Mtanzania kununua ardhi Zanzibar kiholela kungesababisha Visiwa hivyo "kuzama" kwa kuelemewa na ujio wa mamilioni ya watu kutoka Bara.

Hata hivyo, akisema kuna taratibu maalum za kisheria (kama kupitia makampuni), ubaguzi huu wa wazi unawafanya Wanyamwezi, Wasukuma, au Wachagga wajione wageni ndani ya nchi yao wenyewe.

Alitoa sababu ya kufanya hivyo kuwa ni pamoja na ufinyu wa Ardhi, ambapo Zanzibar ni visiwa vidogo vyenye ardhi ndogo sana ikilinganishwa na Bara.

Pia alisema Bara ina idadi ya watu inayozidi milioni 60, wakati Zanzibar ina takriban watu milioni 1.9 pekee.

Maelezo hayo pia yaliwahi kutolewa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla mwaka 2022, akisema Sheria ya Ardhi ya Zanzibar hairuhusu wasio wazawa kumiliki ardhi.

Alisema mtu anaweza kuwa Mzanzibari na akawa Mtanzania, lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibari.

Leseni za Udereva: Sheria za Nchi Mbili Tofauti

Kero nyingine inayowasumbua wananchi wa kawaida ni uhalali wa nyaraka za kiserikali kama Leseni za Udereva.

Imekuwa jambo la kawaida kwa madereva kutoka Tanzania Bara kukataliwa leseni zao wanapofika Zanzibar na askari wa usalama barabarani (Traffic Police).

Askari visiwani humo wamekuwa wakiwatoza faini au kuwataka madereva wa Bara kuonyesha nyaraka za ziada kama Pasi za Kusafiria (Passport) na kadi za chanjo (Yellow Card) kana kwamba wameingia nchi nyingine ya kigeni.

Mmoja wa wananchi kutoka Bara aliyetuma video mtandaoni, alihoji: “Kama nchi ni moja na Serikali ya Muungano ipo, inakuwaje leseni halali ya serikali hiyo isitambalike upande mwingine wa nchi?”

Je, Huu ni Muungano au Ushirika wa Mashaka?

Kama alivyowahi kukiri mmoja wa viongozi wa juu wa Zanzibar, kuna haja kubwa ya wananchi kuelimishwa, lakini zaidi ya yote, kuna haja ya kuondoa mifumo hii ya "shaghalabaghala."

Huwezi kuwa na nchi inayojiita "Moja" lakini ikawa na mifumo miwili tofauti ya umiliki wa ardhi, ubaguzi wa ajira, kutosimamia leseni za udereva kwa pamoja, na kuweka matabaka kwenye huduma za afya.

Ili Muungano huu uwe na maana halisi kwa mwananchi wa kawaida wa kike na kiume kutoka pande zote mbili, ni lazima kero hizi za msingi zitatuliwe kisheria, badala ya kuendelea kufunikwa kwa maneno matamu ya kisiasa jukwaani.
 
Attachments

  • Ajira Zanzibar.mp4
    7.9 MB
Hata hivyo, ukiacha picha ya nje ya "Tanzania Moja," kiuhalisia kuna mambo mengi ya kiutendaji, kisheria, na kiuchumi yanayouanya muundo huu kuonekana wa kusuasua—au kwa lugha rahisi, shaghalabaghala.
Moja ya kero kubwa inayozua maswali kuhusu usawa ndani ya Muungano huu ni suala la umiliki wa ardhi. Wazanzibari wana haki ya kununua, kumiliki, na kuendeleza ardhi upande wa Tanzania Bara bila masharti yoyote magumu, kama raia wengine.

Hata hivyo, hali ni tofauti kabisa kwa Mtanzania wa Bara anayetaka kumiliki ardhi Zanzibar. Kisheria, mtu asiye Mzanzibari hawezi kumiliki ardhi kwa 100%.
Hali halisi ni kama ulivyosema kwenye heading yako, kila Mzanzibari ni Mtanzania ana haki zote za Utanzania, huku bara ikiwemo kumiliki ardhi na ajira ndani ya serikali ya JMT.

ila sio kila Mtanzania ni Mzanzibari!, wenye haki Zanzibar ni Wazanzibari pekee.

P
 
Kumekuwa na kauli tata kutoka kwa viongozi wa Zanzibar kuhusu Muungano, wakionyesha ubaguzi wa wananchi kutoka Bara kupata huduma au kushiriki fursa za kiuchumi, hali inayozua maswali.

Kaulielea kufunikwa kwa maneno matamu ya kisiasa jukwaani.
Sasa tulio na ndugu, ambao ni wazanzibar na bara,tunasemaje?Hapo sio sawa Kuna wazanzibar wanafanya kazi bara,na wengine wamestaafia huku huku bara na wapi bara!
 
Sijawai wapenda wazinzibar BILA shaka nao hawanipendi.

Nataka tu kero za muungano zimeisha Sasa kero ni muungano wenyewe.
Mzanzibari kutawala BARA ni sawa ILA mtanganyika kutawala zenji ni haramu
Una hoja nzuri.Watanganyika kutawaliwa na mdebwedo ni kharamu.
 
Rais ,waziri wa fedha waziri mambo ya nje, waziri wa uchukuzi Mkuu WA usalama WA Taifa, mkuuwa operation wa jeshi la polisi uhamiaji magereza na wengine ndani ya JWTZ, Bado idara na mashirika ya umma manaibu mawaziri wakuu WA mikoa na wilaya.

Kwa maoni yangu kwenye eneo la ajira wenzetu wananufaika sana.

WA Tanganyika Kwa upande wa Zanzibar hakuna waziri , Mkuu wa mkoa wilaya hata shirika zaidi ya kuajiliwa kwenye mahoteli na sasa wanatakiwa kuondoka. Wanaitwa malaya, na WA Tanganyika hawezi kutibiwa huko wakumwa wakatibiwe kwao

Nchi ya watu million 2 na nchi ya watu milioni 60 hapo usawa uko wapi kwenye eneo la ajira na mgawanyo wa rasilimali.

Hapa muungano unapswa kuangaliwa Tena hilo sio kosa la wazanzibar bali ni mapungufu ya waasisi na wa Tanganyika ambao ni viongozi . Viongoziwa Zanzibar ni wazalendo Kwa nchi yao. LAKINI WA Tanganyika Sasa mhhh
 
Nimesoma maoni yako nimelia sana.Natulia kwa muda wa nusu saa naendelea kulia.
 
Go go go mnyukano uendelee mpaka wana muungano tupaghalanyike
 
Sasa tulio na ndugu, ambao ni wazanzibar na bara,tunasemaje?Hapo sio sawa Kuna wazanzibar wanafanya kazi bara,na wengine wamestaafia huku huku bara na wapi bara!
Ukipata muda kasome story kilchotokea Korea baada ya kuvunjika
 
Naunga mkono hoja ,pia kuna hili la Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.Kila baada ya Uchaguzi Mkuu, Baraza la Wawakilishi Znz ,huchagua Wawakilishi watano(5) kama sijakosea idadi, ili kwenda kuwakilisha na kulinda Maslahi ya serikali ya Znz ndani ya Bunge la Muungano wakati tayari huwa kuna wabunge wa Majimbo 50 toka Znz, Wabunge wa viti maalum na hata wale wa kuteuliwa na Rais..Kwangu mimi hili sio sawa

ii. Pili hiki kisiwa ni kidogo , Wabunge wote wa nini?, na waliokuwepo hawana UWEZO or what?
iii. Mwisho, kwanini hakuna Wawakilishi toka Bunge la Jamhuri ya Muungano wanao toka Bara ,ndani ya Baraza la Wawakilishi ili kulinda Maslahi ya Tanzania, na hata kupunguza UPOTOSHAJI huu unaoendelea ndani ya Baraza la Wawakili?
 
Hali halisi ni kama ulivyosema kwenye heading yako, kila Mzanzibari ni Mtanzania ana haki zote za Utanzania, huku bara ikiwemo kumiliki ardhi na ajira ndani ya serikali ya JMT.

ila sio kila Mtanzania ni Mzanzibari!, wenye haki Zanzibar ni Wazanzibari pekee.

P
Zanzibar nzima pamoja na wazanzibari wote idadi yao haijavuka milioni 2, yaani pamoja na Diaspora wote.

Nina uhakika wilaya ya Kinondoni peke yake tupo zaidi ya watu milioni 2. Jiografia ya Tanzania imeifanya iwe na muungano wa aina hii ya sasa.
 
Chuki dhidi ya Zanzibar zinapamba moto muda huu wakati Samia yupo ikulu. Akiondoka pale mwaka 2030 huu ujinga utasahaulika mpaka atakaporudi tena Rais mwingine kutoka huko visiwani.
 
Suluhisho ni kupatikana kwa na kutambuliwa kwa serikali ya Tanganyika then kama muungano unahitajika basi itapatikane serikali ya shirikisho ya JMT ambayo yenyewe itashughulika na maswala ya muungano tu.
Shida ni watanganyika waliopo ccm ambao hao wananufaika na aina hii na muungano.
NB:Kibwagizo cha Mh Sugu kwa wazanzibari wote
 
Wenye busara na hekima, huzitambua CHANGAMOTO mapema na kuzitatua..huko tuendako ni GIZA zaidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom