Mzahamzaha na professional za watu..

Mzahamzaha na professional za watu..

dikembe

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
1,645
Reaction score
1,441
Hallooo ,
subkuch tiike wana jf
Nilikuwa na mahusiano na nurse mmoja katika mji ambako nilizaliwa, baba na mama walikua wanaishi huko.Kipindi hicho nilikuwa field huko home. Baada ya kumaliza field nurse wangu alinipatia vile vipimo vya HIV (kama vikaratasi hivi unaweka tone la damu yako then unasubiri dakika tano kuna mistari itaonekana). Kwa ajili ya kumpima mtu kabla sijamtumia.
Baada ya kurudi DSM ili niendelee na masomo yangu, pale ninapoishi ilikua nyumba ya kupanga nkakuta kuna mdada mpya kahamia kama jirani yangu. Kabla sijafika alishapewa taarifa zangu hivyo hakushangaa aliponiona. Alikua mdada mrembo, mweusi, mrefu, mwembamba ila ana umbo la kuvutia, kiumri alikua kanizidi hivyo heshima ilikuwa juu.
Basi tukaanza urafiki akiinita uncle, akawa anapika na kunikaribisha maramoja moja. Baada ya kama mwezi siku moja alikuja chumbani kwangu kucheki movie, basi katika kupiga story mara ikaingia ya kupima HIV, yeye akasema hajawahi kupima mi nkasema nshapima mara nyingi, na hapa ndani nina vipimo kama ana moyo nimpime. Akasema nimpime, Basi nikatoa vipimo vyangu nikamchukua damu nakumpima, wakati anasubiri vipimo jamaa yake akaja hivyo akaenda kuongea nae, akaaka muda mrefu mpaka jioni jamaa akawa kaondoka, huku upande wangu vipimo vikaonyesha ana maambukizi! nilijuta kumpima kwani nitamwambia nini mdada wa watu? sijui chochote kuhusu ushauri nasaha.....mh...ilikua wakati mgumu sana kwangu, nilimwonea huruma sana.
Basi baadae akaja na kuniuza majibu yake, nkamwambia yuko poa, ila akalazimisha kuona hiyo karatasi nkamwambia nimeitupa...Hakuamini akaanza kutafuta mara akaiona na kugundua ameathirika! Dah, alilia sana kwa uchungu na kutaja jina la boyfriend wake, mama yake pamoja na mwanae( kumbe alikua na mtoto mmoja). Dah, nlishindwa nifanyeje, nkajikuta nambembeleza na kushauri aende hospital kwa ajili ya kuhakiki kwani hivyo vipimo havina uhakika sana. basi baada ya mtanange mrefu alitulia.
Kesho yako alidamka kwenda kupima na kweli akakuta positive, ilikua siku ya huzuni sana kwake alitamani kujiua na kusema jamaa ndio kamletea.
Baada ya kama mwezi alikubaliana na hali na mimi nilimfichia siri na akaanza kupata dozi ya ARV. Maskini nilijuta kumpima, masihara yalinifanya nijione mkosaji... Ila nilimwonya asimwambie jamaa yake kwani itakuwa mwisho wa kupewa misaada na atatelekezwa, hii ni kutokana na kumbe jamaa alikua mume wa mtu, yeye alikua kimada tu....
Ni miaka kumi sasa imepita sijui kama bado yupo hai au alifariki dunia.....
 
Utakuja kufungwa bure. Ww hujui ni kosa?
 
Mkuu nilijuta kujaribu, nkataka ku-undo nikashindwa , nkatamani iwe ndoto tu but nkaona najidanganya....mpaka kesho nakumbuka hili tukio.
 
Aisee, sijui kwa nini sinaga aina hizi za curiosity. Kuna mtoto aliwahi mtahiri mwenzie kwa bati, kidogo aue.
 
Hizo pressure za kupima huwa mnazitafuta za nini?
 
Mkuu, mh..roho za wanasayansi hizo..Ni kuatili wa asili, au pia ni akili za kitoto kutokufikiria in three dimension. Impact ndio inakuzindua.
 
Mkuu jibu sahihi sina, ila haikuwa serious kabisa. mwisho wa siku ikawa very serious and unfortunately sikua na plan B.
 
Dah, kiherehere cha kwenda kumpima mtu mambo makubwa wakati it takes more that 45mins kumuandaa mtu ulianza anzaje kwa mfano. Kwani wakati unampima ulidhani nini kitatokea kwa mfano?
 
Pole, hopevumekua sasa

Mkuu, mh..roho za wanasayansi hizo..Ni kuatili wa asili, au pia ni akili za kitoto kutokufikiria in three dimension. Impact ndio inakuzindua.
 
Dah, kiherehere cha kwenda kumpima mtu mambo makubwa wakati it takes more that 45mins kumuandaa mtu ulianza anzaje kwa mfano. Kwani wakati unampima ulidhani nini kitatokea kwa mfano?
Kuna kitu mimi sina kwenye maisha yangu, NEGATIVE THOUGHT...na hichi ndicho kiliniponza. Ila nilikua bado mdogo sijui vitu vingi hapa duniani, nlikua bado nategemea boom. Bahati mbaya ila ilinifuza na mpaka sasa naikumbuka
 
mkuu huyo nesi ndo asiyependa muvi za cinemax, anapenda mle nyumbani chakula anachopika na sio chakula cha hoteli du hapendi umpe hela ya vocha ndo huyu?
 
Hallooo ,
subkuch tiike wana jf
Nilikuwa na mahusiano na nurse mmoja katika mji ambako nilizaliwa, baba na mama walikua wanaishi huko.Kipindi hicho nilikuwa field huko home. Baada ya kumaliza field nurse wangu alinipatia vile vipimo vya HIV (kama vikaratasi hivi unaweka tone la damu yako then unasubiri dakika tano kuna mistari itaonekana). Kwa ajili ya kumpima mtu kabla sijamtumia.
Baada ya kurudi DSM ili niendelee na masomo yangu, pale ninapoishi ilikua nyumba ya kupanga nkakuta kuna mdada mpya kahamia kama jirani yangu. Kabla sijafika alishapewa taarifa zangu hivyo hakushangaa aliponiona. Alikua mdada mrembo, mweusi, mrefu, mwembamba ila ana umbo la kuvutia, kiumri alikua kanizidi hivyo heshima ilikuwa juu.
Basi tukaanza urafiki akiinita uncle, akawa anapika na kunikaribisha maramoja moja. Baada ya kama mwezi siku moja alikuja chumbani kwangu kucheki movie, basi katika kupiga story mara ikaingia ya kupima HIV, yeye akasema hajawahi kupima mi nkasema nshapima mara nyingi, na hapa ndani nina vipimo kama ana moyo nimpime. Akasema nimpime, Basi nikatoa vipimo vyangu nikamchukua damu nakumpima, wakati anasubiri vipimo jamaa yake akaja hivyo akaenda kuongea nae, akaaka muda mrefu mpaka jioni jamaa akawa kaondoka, huku upande wangu vipimo vikaonyesha ana maambukizi! nilijuta kumpima kwani nitamwambia nini mdada wa watu? sijui chochote kuhusu ushauri nasaha.....mh...ilikua wakati mgumu sana kwangu, nilimwonea huruma sana.
Basi baadae akaja na kuniuza majibu yake, nkamwambia yuko poa, ila akalazimisha kuona hiyo karatasi nkamwambia nimeitupa...Hakuamini akaanza kutafuta mara akaiona na kugundua ameathirika! Dah, alilia sana kwa uchungu na kutaja jina la boyfriend wake, mama yake pamoja na mwanae( kumbe alikua na mtoto mmoja). Dah, nlishindwa nifanyeje, nkajikuta nambembeleza na kushauri aende hospital kwa ajili ya kuhakiki kwani hivyo vipimo havina uhakika sana. basi baada ya mtanange mrefu alitulia.
Kesho yako alidamka kwenda kupima na kweli akakuta positive, ilikua siku ya huzuni sana kwake alitamani kujiua na kusema jamaa ndio kamletea.
Baada ya kama mwezi alikubaliana na hali na mimi nilimfichia siri na akaanza kupata dozi ya ARV. Maskini nilijuta kumpima, masihara yalinifanya nijione mkosaji... Ila nilimwonya asimwambie jamaa yake kwani itakuwa mwisho wa kupewa misaada na atatelekezwa, hii ni kutokana na kumbe jamaa alikua mume wa mtu, yeye alikua kimada tu....
Ni miaka kumi sasa imepita sijui kama bado yupo hai au alifariki dunia.....

mkuu huyo nesi ndo asiyependa muvi za cinemax, anapenda mle nyumbani chakula anachopika na sio chakula cha hoteli du hapendi umpe hela ya vocha ndo huyu
 
Mkuu..kama umenisoma vyema, kwanza ni kitambo, miaka 10 imepita, halafu aliyenipa vipimo ni nurse na hapo nilikua bado nasoma chuo, yule asiyependa cinemax kama ulivyomention nilikutana naye baada ya kumaliza chuo. nadhani tuko pamoja! na huyu niliyempima alikua jirani tu, nlimpima kimasihara...Unakumbukumbu nzuri.
 
sooo sad aisee sipati picha hali uliyokuwa nayo wakati umeona hayo majibu ... its sad jamani usifanye hivyo tena,... pole sana
 
Michango ya watu wengi hapa kwenye thread mnajikanyagakanyaga tu. Mleta thread alimpima nia kuwa kama angekuwa mzima bhasi angejitahidi kufanya fitna nae apige.

Mbaya sasa kamkuta tayari kimesoma unadhani nae mpimaji si alibaki mdomo wazi tu.
Kumbuka alishasema ni mzuri sasa..........
 
Mkuu kiukweli halikuwa lengo kwani alikuwa mkubwa kwangu, halafu nilikuwa sina hela ya kumshawishi kumbuka nlikua nategemea boom tu. So hakuwa level yangu.
 
hivi mkuu wewe unamasihara sana unachukua tu jukumu la kumpima mtu kirahisi bila kusoma sykological yake,bahatimbaya akifa kwa presha hilo ni kosa la kuua kwa kukusudia.na lengo lako hashwa angekua negative ungemuomba mchezo
 
Back
Top Bottom