My upcoming trip to Jordan

My upcoming trip to Jordan

Relief Mirzska, Daah mimi nikitengeneza list nahisi nitafikisha nchi zaidi ya 50 na sitajua ipi niweke ya kwanza ipi niweke ya mwisho maana natamani ningekuwa na uwezo wa kujigawa nitembelee zote kwa wakati mmoja
 
cute b si bado mdogo sasa

By the way nilishawahi kuandika humu kuwa hata mama yangu mzazi anajua kuvaa kuliko mimi yaani yeye na dada yangu wa kwanza pamoja na mdogo wangu anayenifuata wananishinda kwenye kuvaa

Yaani mimi najiona kabisa nitakavyofanikiwa mapema maana sipendi anasa sijui kuvaa, situmii makeup, sivai mawigi wala siweki kucha za bandia (maana hivi ndiyo vitu vinavyomaliza hela zetu wanawake kwa asilimia kubwa)

Yaani hata ndugu zangu wameshalijua hilo kwamba mimi napenda sana kusafiri kuliko kufanya hivyo vitu, nikiwa Mbeya nikienda kutembea milimani huko huwa nawapigia simu kuwaambia leo nimeenda kutembea sehemu fulani na fulani.

Nakumbuka kuna kipindi ajali zilifululiza kule Mbeya milimani huko, sasa kuna siku ilitokea ajali kubwa iliyowashitua watu, nakumbuka siku hiyo mama alinipigia simu kuniuliza kama mzima nikamuambia ndiyo akasema anhaa nimesikia kuna ajali imetokea, nikakupigia kujua kama ni mzima maana hauchelewi kuwa umeenda kuzurura milimani huko ikakukuta nikamuambia sikuenda.

Ninayeona kidogo ana hobby ya kusafiri ni dada yangu wa kwanza japo yeye anapenda sana safari za ndege na basi kidogo, mimi sichagui yaani ndege, basi, meli na treni vyote twende tu tena kama safari za Dar Mbeya nishapanda sana treni za tazara zile yaani vile tunavyokaa siku mbili njiani mie ndiyo napenda na hamna stress sababu mule ndani kuna kila kitu siyo ndege lisaa limoja tu tumefika khaa.
Aiseeeeee.

Kumbe nawe ni msafiri eti
 
Aiseeeeee.

Kumbe nawe ni msafiri eti
Bado sijioni kama msafiri mkuu, bado sana yaani nikianza kuenda nje kama wewe hivi hapo ndiyo naweza kusema mimi ni msafiri.

Sasa mkuu mwaka 2022 hauna mpango wa kuenda kucheck kombe la dunia live kule Qatar??
 
Nimekaa Amman miezi miwili kwa kweli ni mji msafi katika miji yote niliyotembelea
Huwezi kujutia na watu ni wakarimu sana na maisha yao ni juu
Nimependa nyumba zao pia ni kubwa na za kifahari

Kusafiri ni hobby yangu pia na nimejaza passports nne tangu miaka ya 70
Na kila nikiangalia pages za passports hizo ni vitabu tosha kwani zina kumbukumbu nyingi sana
 
Sehemu ambazo ningependa kufika

1-BALI

2- Machu picchu

3-Delhi

4- Egypt

5- Paris

6- Brazil

7 - Iran

8- Liverpool

9- New york na washington

10- Mwezini
 
Oohh mimi sehemu ambazo ningependa kuishi milele ni USA au UK kwengine ningependa kutembelea tu
Sipendi kitu kinachopendwa na wengi.. huko labda kutembea. Kwa afrika laiti Zanzibar kungekua hakuna bahari ningeweka makazi milele.. sasa bahari na jinsi wakristo walivyo wachache huko unakua mpweke fulani hv..
Nimeishi huko 9 months ustaarabu na ukarimu ulinivutia mno. Halafu natunda kama uko peponi yaani
 
Back
Top Bottom