Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,976
- 22,409
- Thread starter
- #41
Aiseee kuna watu wakisoma hii wanaonijua mimi watasema mbona hawa wote kuna vitu kwao sio kipaumbele??Hapana shaka, wanasema sharing is caring ila wengine wasijesema tunajimwambafy na JF kila mtu anapanda ngege, kila mtu ana gari kila mtu ana life nzuri....
Ofcourse hata usiposhea travel experiences hawataacha kusema, ila iwe angalizo tuu. Ukiona mtu amefanya jambo ambalo sio la lazima na limegharimu hela ujue amelipa kipaumbele au kwake lina umuhimu mkubwa kuliko kuchangia harusi za watu mwaka mzima halafu kati ya ndoa 40 ulizochangia kila moja minimum ni laki moja ambayo kwa uchache inakuja milioni 4 kwa mwaka unakuta ndoa 36 zimevunjika kwa sababu ya kuchepuka 3 mmoja wa wana ndoa kauwawa na mwenzie sababu ya wivu wa mapenzi moja ndo iko kwenye mazungumzo na kasisi na familia.
Sisemi watu wasichangie harusi au ndoa si muhimu ila kila mtu ana kipaumbele chake. Ukiona nimewekeza au natupa hela nyingi kwenye safari sio kuwa najitapa au najisifia, ni kuwa nimeipa ari ya kusafiri kipaumbele kuliko kukaa sehemu za starehe na kununulia marafiki pombe ( again mie sio mnywaji na simaanishi wanaofanya hivi wanakosea) bali hela yangu naitumia kwingine sawa na wao wanaotumia kwenye mavazi, urembo, wengine kusoma (elimu) wengine kuhonga, wengine kusaidia wahitaji n.k.
Kwangu kuvaa sio kipaumbele, sivai mitumba ila kuvaa nguo za elf 10 au 20 sio issue mradi niwe smart. Kwanza huwa nanunua nguo wakati wa sale tena 75% sale hehehheee. Na mshiko wangu kwa asilimia kubwa ni kula bata nikiwa likizo sehemu mbali mbali....
Kibibi Mpenda Kusafiri
K' Matata.
Umeongea fact tupu. Qs I said, it's a Matter of priorities. Mimi kuvaa kwangu hakuna umuhimu, out zisizo na msingi hazina umuhimu lakini I have to travel come holiday.
Hongera sana Kasie