1. Kaka naona hatujakutana siku nyingi sana, ok naona ulichotaka hapa ni kuonyesha umeenda Shule lakini hata na wewe analysis hujui maana yake, ungejua usingeandika habari za Description nilichofanya ambacho umeshindwa kukielewa nimechambua analytically credibility za wale wanaomsemea Lowasa kuwa Rais, which has nothing to do Description kama unavyosema inaonyesha na wewe umegundua siku nyingi sana kwamba humu hamna wasomi so ukaamini ukiandika maneno maneno ya English basi utaonekana una shule kumbe hujaandika lolote zaidi ya pumba kaka. Huwezi kutumia Description kwenye ku-analyze credibility za watu kama nilivyofanya.
2. Kaka niligombea Ubunge wa Afrika Mashariki nikashindwa and then nikagombea Ujumbe wa Baraza kuu la Taifa Wazazi nikashinda, and nikashinda nafasi zingine na sasa mimi ni:-1. MJUMBE MKUTANO MKUU CCM TAIFA 2. MJUMBE BARAZA KUU LA TAIFA WAZAZI/CCM 3. MJUMBE BARAZA KUU LA TAIFA UVCCM, unasema all these hazinipi Moral authority ya kuongea na kuchambua kama nilivyofanya? Are u serious au unabahatisha kaka au ulikuwa hujui? Ungeuliza kwanza kaka kuliko kujiabisha kama ulivyofanya mnaandika andika tu hovyo hovyo bila kujua unashindana na nani kaka kweli unafikiri mimi na wewe kisiasa tupo level moja? please!!
3. HA! ha! hili la mwisho ndio kabisaa sasa naamini huna elimu kabisa kaka, maana Full of judgement huwezi kuifanya bila FACTS, kwanza nimewataja wasemaji wake na nikatoa na FACTS kwamba ni kwa nini naamini kwa kutumia zile FACTS kwamba hawawezi kumsaidia kuwa Rais maana hawana credibility,
- I understand kaka una elimu ila ni ndogo sana kulinganisha na niliyonayo pamoja na exposure, nakuona mara nyingi sana ukijifanya CCM kwa kuweka picha umevaa shati la Kijani, binafsi sijawahi kuwa -impressed na anything of you humu maana nilishagundua siku nyingi sana kwamba huna elimu ya kutosha na huna exposure, na wewe ulishagundua kwamba humu wasomi sio wengi so unaweza kuruka na ujinga ujinga kama huu ulioandika na kuonekana una elimu sana hasa ukinadika maneno kwa English kumbe umenandika pumba tupu kaka pole sana, next time ukiona mtu aliyendika kama mimi ameenda shule tuliza boli maana utishia kuaibika kama hapa leo hii aibu kaka!!
Le Mutuz
Naona unafanya personal attacks wakati mimi nilichofanya ni a critical review albeit brief of your so called political analysis; pamoja na maelezo yako hapo juu to defend your so called "analysis", hoja yangu ipo pale pale hivyo nisingependa kupoteza muda kujirudia.
Ninalazimika kujadili masuala mengine matatu uliyojadili kwa kunilenga binafsi:
Kwanza ni suala la elimu; hatupo hapa kushindana nani kasoma zaidi; kama umesoma, ni jambo zuri tu, kikubwa ni kurudisha fadhila kwenye jamii iliyokufikisha ulipo kielimu, huo unatakiwa kuwa ndio wajibu namba moja wa mtanzania aliyebahatika kupata elimu;
Nikiwa bado katika suala hili la elimu, nakumbuka nilienda marekani kusoma uchumi miaka ya early to mid 1990s na nikiwa huko, nilikutana na wewe New York (New Rochelle - pengine hukumbuki) ukiwa ni dereva wa malori ya mizigo; kwahiyo kama baadae uliamua kwenda shule, nakupongeza kwa hilo; kilichobakia kwetu sote sasa tutumie elimu yetu kwa kuendeleza jamii yetu ambayo kimsingi ndio imetufikisha tulipo;
Hoja yangu ya pili ni shambulio lako dhidi yangu juu ya matumizi ya kiingereza kwamba nafanya hivyo kuonyesha nimesoma;nadhani hoja hii ni self defeating kwani wewe mwenyewe kichwa cha uzi wako kipo kwa lugha ya kiingereza, suala ambalo kwanza ungeweza tu kusema "uchambuzi wangu wa kisiasa" badala ya "my political analysis"; kwa lugha yako, ina maana hoja za kiingereza zinakaribishwa, au nimekosea? Katika hili nikueleze tu pia kwamba content ya hoja yako ingefaa zaidi kusema "my political opinion or my political observation", sio political analysis kwani kwa bahati mbaya, haipo;
Na mwisho ni juu ya uanachamma wangu wa ccm; umekuwa na mazoea ya kuni criticize sana kwa maneno kwamba mimi sio mwenzenu, mimi msaliti, mimi sio mwanachama wa kweli n.k; mwanachama wa kweli na asiye wa kweli definition zake ni zipi? Ni kitu gani nachofanya ambacho ni kinyume na yale ambayo mwanachama (sio kiongozi) anatakiwa kufanya? Umeusoma mwongozo wa ccm (1982) pale kwenye kanuni inayosema:
kukosoa na kukosolewa ni silaha ya mapinduzi?
Na kwa vile watunzi wa mwongozo huu walijua watajitokeza watu kama wewe, mwongozo ukaweka bayana kwamba ;viongozi na wanachama hawatakiwi kuhamaki pale wanapokosolewa"; kuhamaki kwako kila siku kila napokosoa chama maana yake haupo in touch na kanuni za chama zaidi ya kanuni zile tu zinazo serve your personal interest;
Isitoshe, hoja nyingi sana ambazo huwa najenga humu juu ya kwanini nadhani ccm imepotea, hoja hizo hizo zikijadiliwa na viongozi wako wakuu, tukiwaita tujadili, mnakimbia; kwa mfano, mwenyekiti wa ccm taifa ambae unamsifia humu kama kiongozi bora amewahi tamka kwamba bila ya uangalifu wa viongozi, chama kitaanguka 2015 huku akikejeli maneno ya kawaida midomoni mwa viongozi kama wewe ya "wembe ni ule ule" akisema wembe huo utawakata wenyewe; ni haya haya mimi huwa najadili na wewe unatoka povu lakini akijadili mwenyekiti, mnakaa kimya;huu ni unafiki na ni unafiki wa aina yako ndio unakiua chama;mwenyekiti pia kasema wana ccm wajiandae kisaikolojia na serikali tatu, na wiki ijayo anataka kukutana na vyama vyote kuepuka vurugu zisizo za lazima ndani ya bunge lijalo la katiba;haya ya JK tumeyajadili sana na nyie kuja na topics kutuponda kwamba sio wana ccm wa kweli, lakini yale yale akisema mwenyekiti, tukiwaita mje tujadili, mbio;unafiki!
Na jana, Katibu mkuu wa ccm Kinana amesema anataka kurudisha ccm ya nyerere, hoja ambayo kila wakati tukijadili, mnakuja na kutukebehi huku mkimtukana mwalimu;haya sasa, yale ambayo nikijadili kama mwanachama na wewe kunishambulia, kinana kayasema na najua kwa sababu ya unafiki, hautakuwa na hoja ya maana katika hilo; kwanini kinana anataka ccm ya nyerere irudi?jibu ni pamoja na kwamba iondokane na watu kama nyinyi;
Mwisho, mimi sio tu mwanachama hai wa ccm ambae nilianzia na chipukizi na baadae uvccm tawi la rungwe sekondari, leo hii ni mwanachama hai wa ccm kwa miaka zaidi ya 20 na kadi yangu imelipiwa ccm tawi la kawe mbele ya katibu wa tawi; in addition, mimi ni raia wa Tanzania peke yake hivyo natosha zaidi kihoja juu ya uzalendo unlike you ambae ni nduminakwili kwani una uraia wa zaidi ya moja;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums