Ok... Tusizunguke sana Willy. The point is hoja yako haina mashiko kwa sababu;
Moja, bado haijulikani zaidi ya waliosema ni kina nani wengine ama wanamuunga mkono au wanampinga Lowassa hadi sasa.
Kwa bahati mbaya ni kwamba wote waliomtetea na waliompinga, hadi sasa ni watu wasio na credibility.
Mbili, haijulikani wenye 'credibility' huko CCM (Kama wapo), wana msimamo gani dhidi ya Lowassa maana hawajaongea.
Tatu, haijulikani kama waliompinga wana chaguo jingine au hawana.
Nne, hatujui kama waliompinga Lowassa kama wana chaguo lao, je hilo chaguo ni credible au sio
Tano, hadi sasa Lowassa hajapata mpinzani kwa maana kwamba ya mtangaza nia mwingine. Ni Lowassa peke yake ndiye "aliyeoteshwa" hadi sasa. Upo uwezekano pia kuwa kipenga kitapulizwa kabla mwingine hajajaaliwa ndoto...