Selina akashukuru Mungu, dola 1000 sio ya kitoto hata akinengua wiki nzima hapigi dola 1000. Akasnza kupiga akili atafute nyumba apange maana sio kwa kukaa kule
Akahangaika na nyumba akaipata, akalipa kodi ya miezi 7 huku anajitafuta. Asubuhi anaenda kufundisha usiku stripping! Maisha yakawa yanaenda ivo ivo buzy na mambo yake. Yeye na pendo hawawasiliani hata kidogo!
Pendo yupo engaged! Haaamini wala hajawahi kuota! Kwanza alijua hatoolewa, miaka 37 hana mtoto hana bwana huyo Jose tangu ampate ana mwaka tu. Akachukua simu ampigie mama yake akaona haitanoga mama akapokea akamwambia nakuja huko mchana naona Jose ameenda ofisini! Akajiandaa kwa mama mojaa!
Mama akafika anasubiri aambiwe ubuyu Pendo akamwonyesha kidole mama wooooow jaman mwanangu akamkumbatia eee bora na mie niozeshe uuuuwi jamaani Mungu asaaante jamani nimefunda wengi na mie mwanangu namtoa kimasomaso mara anapanga harusi ifanyike wapi mara hivi mara vile eh mama mbona hata hatujapanga tarehe za harusi afu yule ujue ni mjane sidhani kama atataka mambo makuuuubwa simple tu church watu 10
Kungwi: watu 10?! Hapana labda harusi ila sendoff lazima nitikise kijiji!
Pendo akakosa pozi! Kha! Hapa kazi ipo akamkubalia tu sawa mama hii ni show yako ila kitchen pati wala staki
Kungwi: nini?!hapana asee kpati lazima nifanye kijijini yani ya nguvu kubwaa!
Pendo anazidi kuchooka
Kungwi: kwani unajua kila kitu kuhusu ndoa mwanangu?! Staki aibu mie, unaolewa unarudishwa baada ya siku ya 3! Hapana asee!
Pendo akawa mpole kama jongoo akasema sawa tutakwambia tarehe ya harusi na siku ya mahari sasa hivi siwezi hata kuuliza itakuwa mapema saana. Eh kungwi kafurahije sasa anaozesha anapiga mahesabu nani wa kumfunda mwanangu maana mtoto anauma sio kitoto! Akaona ampeleke kwa Rasheeda kubwa la maadui wake, mkali wake, mjanja wake
Manoa keshakuwa supa wa mjini mjini! Kapendeza Maringo kampendezesha ukimwona utadhania pedeshee. Maringo akaitisha family meeting kwake bila mama yake. Wakaja kaka zake Hachikoko na Luwi! Wakakaa wanne na baba yao!
Maringo akawaambia baba kule kijijini ameshatengana na mama, akikaa kule atakufa lazima tumlete hapa! Lazima apangiwe hapa, atafutiwe kibarua, kodi ya miaka 2 tunailipa sisi, misosi sisi, usafiri sisi, kwa ufupi pocket money ni sisi!
Kaka zake wanamwangalia baba yake kabadilika kawa handsome kweli, wakawa wanashangaa ivi Maringo hii nyumba unamiliki vipi na hilo gari wakauliza kakaz!
Maringo: hayo baadae kwa sasa twamtaka baba apate nyumba awe na uhuru wake sio vizuri mtoto wa kike kuishi na baba yake tuu!
Kakaz wakakubali wakapiga mahesabu yote wakaja kugawa kwa 3, kila mtu akarnda kutafuta hela yake, ndani ya siku 3 baba kapangiwa nyumba Leopard Hills huki mashambani wakamwekea na ng'ombe na mbuzi awe anachunga, wakamtengea kasehemu analima hapo! Akafurahi mwenyewe ingawa sio karibu na home. Kila weekend wanapeana zamu ya kwenda kumwona baba yao, wanaenda na wajukuu wanaenda alone wanaenda kama picnic sikunyingine wanamwalika mama yao Rasheeda aje anakataa ah basi tu maisha yanaenda, Manoa kawa wa mujini, akanunuliwa na gari Rav 4 awe anazinguka zunguka
Manoa akajiongeza akawa anafuga na kuku akazungukia supply hapo mjini mahotelini na kwenye nyumba za watu akapata tenda ya mayai, kuku, ng'ombe akakaa sawa.
Kijijini akaweka mtu mashambani akivuna mavuno anakuja kuuza mjini anapata hela, nyumba ya kijijini akapangisha
Siku moja anatoka kwenye mizunguko yake akakutana na kungwi anatembea barabarani akamfuata na Rav 4 yake, nakuona mrembo umevamia jiji la Lusaka, Kungwi kumwangalia haamini! OMG! Manoa?! Kha! We manoa wewe umekuwaje?! Umekuwa handsome katoto?na gari unaendesha?! Kweli dunia duara!
Manoa: nipo baby naishi Leopard Hills nikupeleke kwangu ukapaone. Wewe unaishi wapi?
Kungwi: naishi hapo mbele nipe lift nikakuonyeshe akapewa lift wakaondoka huku wana catch up ya kijijini mpaka mjini. Kufika kwa Kungwi Manoa anashangaa mbona anaishi pazuri, Kungwi akamwambia hapa kwa mwanangu pendo ameniachia nikae yeye aneshachumbiwa anaishi na bwana wake si unajua tena haya mambo ya mjini me nimemkataza amekataa yani aibu tupu
Manoa: hongera sana Kungwi kwa kupata mkwe
Kungwi: asante hapa nasubiri mahari nirudi zangu kijijini!
Manoa: ok sawa hongera sana nyumba nzuri sana. Wakawa wanaongea pale masaa kibao kushtuka saa 11 jioni manoa akaaga. Me naenda kwangu mbali, Kungwi akamwambia karibu tena si ushapajua hamna neno
Manoa: asante, karibu na wewe kwangu hata leo twaeeza kwenda kesho nikakurudisha
Kungwi kuambiwa hivyo kama amewashwa mota chini! Akapaki fasta fasta utadhani anaenda mkoa wakaondoka wote mpaka kwa manoa anatoa tu macho palivyo pazuri kuliko kwake. Anamwuliza Manoa ivi inafanya shughuli gani?! Manoa anamwambia ufugaji na kilimo kidogo tu
Maringo akaanza kazi UN kila mtu anamshangaa lile body tinga tinga! Maringo nae yupo noma kwenye kazi sio kitoto, anapiga mzigo hatari! She is a very hard working girl, akapata msg kwa Bank manager: bebi umenitupa kabisa! Tangu uniahidi haujatokea!
Maringo: usijali jioni basi ntakucheki love!
Bank manager akajaa midadi kisa kaitwa love
Usiku Patric akatia timu kwa mara ya kwanza kwa Maringo, eh! MAaringo kapiga hot pants patric akachoka zaidi, hamba cha maongezi wala nini akamvamia maringo wa watu, piga miti miti na wewe, du! Patric weeee! MUNGU anakuona! Yani anachanganya mama na mtoto, kweli wanaume wengine ni wagonjwa waliotoroka milembe!
Joe bado yupi Hospital, Kandi akajipa kibarua cha kila siku kwenda kumwona ex wake maana hakuwa na msaada mwengine zaidi ya wazazi na ex wake! Joe akaanza kupata relief, akimwona Kandi na wazazi wake anawatambua wote, akaanza mazoezi ya therapy kidogo kidogo Kandi yupi benet anamsaidia keshamsahau Drogba akipigiwa hapokei simu hajibu sms Drogba akapotezea akawa amebakia na Kungwi tena kungwi mwenyewe mpaka amwite basi taabu tupu! Mary na Neema hawamcheki tena akajiona ana gundu, akawa yupo buzy na kazi basi
Siku moja akafunga safari kwenda kwenye strip club! Akiwa amejaa minyege akamkuta selina, anapiga mipombe huku anamwangalia selina! Eh si akaenda kumlipia! Akalipa dola 500, kweli Nigerians wana mawe hatarious! Selina kuitwa kumbe Drigba akagoma akamwambia meneja mrudishie hela yake huyu shemeji yangu meneja kurudisha hela akakataliwa akaambiwa hapokei aongee na selina mpaka akubali
Selina akamwuliza meneja kwani kalipa ngapu akajibu dola 500 yako 250. Selina akiangalia anaitaka na shida zake kem kem akakubali!
Drogba akambeba mpaka chumba cha ndani akala mzigo! Selina roho inamuuma dah kweli kazi ya uchangudoa tuwaachie wazoefu sie tunaojaribu dhamira zetu hazijafa ni sheedah! Akavumilia ivo ivo mpaka Drogba akamaliza akaondoka zake kurudi home.
Zikapita siku 2 Selina akiwa ofisini anaendelea na shughuli zake kama kawaida akaja kuitwa Selina una mgeni wako, selina akaguna akatoka! Kuangalia ni Drogba! Tobaaa kasahau nini tena huyu mwanaume? Dyu dyu lake au?! Akaenda kumsikiliza kwa aibu reception
Selina: nambie Drogba! Kuna kitu umesahau au umekuja kufuata chenji maana me sikulipwa hela jana niliikataa
Drogba: sahau kuhusu hela, nataka kuongea na wewe!
Selina: nambie lunch yangu inaisha after 1 hr
Drogba: naomba tuongelee kwenye gari, wakatoka kwenda kwenye gari Selina akawa anajua anaenda kuliwa
Drogba: selina unajua sijapenda kaka yangu alivyokufanyia! Me sijafurahi kabisa lakini nimekaa siku 2 hivi nimeshindwa nimeona nije kukwambia kuwa me nakupenda sana naona uwe mpenzi wangu!
Selina: tobaa! Hii ya leo kali sasa napigwa mpira toka kwa kaka mtu mpaka mdogo mtu, we Drogba ni mkichaa au?! Unataka kuniletea aibu me kwenu?! Oga akijua itakuwaje?!
Drogba: ah haijalishi bwana me nimekupenda kikwelii sio kwasababu umenipa mechi kali wala nini hapana ni kwasababu tu nakupenda!
Selina: haya nimekusikia
Drogba: naomba namba yako
Selina: sina simu
Drogba: naomba nije kukuchukua baada ya kazi nikupe lift mpaka kwako
Selina: hapana me sina nyumba nalala tu kule kazini naamkia hapa nikitoka kazini hapa sina nyumba
Drogba: dah! Selina jaman, naomba unieleer
Selina: na wewe naomba unielewe nipo kazini lunch inaisha baada ya nusu saa hata sijala hapa
Drogba: unatoka kazini saa ngapi?!
Selina: saa 10
Drogba: naomba basi niambie muda wako wa kutoka wa kikwelii
Selina: eh na wewe! Saa 11 jioni
Drogba: saa 11 nipo hapa!.
Selina: sawa kwaheri akawa anataka kufungua mlango Drogba akamzuia! Akatoa pochi akampa dola 200 hii utakula leo, Selina akaipokea kama ni last money yake! Akashuka akamwambia asante akaondoka!
Drobga anamwangalia tu anavyoondoka na yeye akaondoka. Saa 10 Drobga yupo getini, Selina hajatoka akakaa kumsubiria mpaka saa 11 akatoka akamfuata, nimekuja mpenzi kukuchukua, walimu wenzake wanamshangaa mpenzi wa Selina hawajawahi ona selina anakuja chukuliwa na mwanaume kwenye gari nzuri kama ile. Drogba uongo dhambi alikuwa na gari kali.
Selina akameza mate akamfuata, yani Drogba hatuelewani mbona unanifanyia vurugu lakini?! Drogba akamshika selina kwa nguvu akambusu mdomoni, walimu wenzake wanachukua selfie na video, Selina akajichomoa kwa Drogba akamchapa kibao, niache akaondoka. Drogba anamfuata nyuma anamkimbilia walimu wenzake wanashangaa hili la leo picha la kihindi! Nehi nehi chori chori acha acha! Kuchi kuchi hotaee!
Wakatembea wee maili moja selina mbele Drogba nyuma Selina anajiuliza kwani leo Drogba kapatwa na nini jamaa! Au ana mapepo?! Akawa haelewi Drogba akamkimbilia selina akampata akamshika akamnyanyua juu akambeba, Selina mwenyewe mwembamba na Drogba kajazia miraba 4 Selina anampigapiga mangumi kwenye mikono Drogba niachieeee! Nakwambia niachiee! Drogba anazidisha mwenda mara akimbie mara atembee wakafika kwenye gari yake akafungua akamtupa nyuma ya seat selina akafunga gari akapumua.
Baada ya dk 10 Drogba akaingia kwenye gari Selina anamwambia Drogba tafadhali naomba niache niende kazini me sina kipato kingine zaidi ya hii kazi yangu tafadhali, niache abeg!
Drogba akanywa maji kwanza, akamwambia nakupeleka kazini kwako under one condition. Iyo kazi unaacha! Kuanzia leo haufanyi iyo kazi! Selika akabakia mdomo wazi kizungu mkuti haelewi!
Selina: Drogba haya ni maisha yangu unataja nikale polisi au?! Huku Drogba anaendesha gari!
Drogba akamwambia hapo nyuma kuna mfuko uchukue ufungue uangalie kuna zawadi yako, selina kuangalia kumbe simu! Akaambiwa aiwashe akaiwasha ina line iliosajiliwa,
Drogba: hio simu na laini vyote ni vyako! Akaambiwa aangalie ndani ya Boxi akakuta risiti ya nyumba imelipiwa kodi miaka 2! Selina alipochoka zaidi eneo alilolipiwa sasa ndio alipochoka, nyumba kapangishiwa Mass Media Lusaka! Kha! Kwa wazungu na wenye hela zao me mbona naona kama naota anajiambia moyoni! Wakawa wanakaribia ofisini kwa Selina, Selina haamini analia tu kwani kuna nini Mungu mbona unanijaribu namna hii anajiongelesha moyoni anashangaa kuna nini simu ya maana iphone sijui hata kama anajua kuitumia!
Kufika Drogba anamwambia unataka kwenda au unaacha kazo hapa hapa nambie mapema nikiondoka sirudi tena!
Ukiacha kazi nitakutaftia kazi ya kufanya sio hii kama unataka kazi 2 sawa kama unataka vinginevyo sawa kafikirie unaifute kwangu, akamuelekeza, hela hizi hapa dola 1000 za kwako za kuanza maisha, kwaheri!
Selina akashuka anashangaa Drogba kawaje ana mapepo au akaenda zake ndani
Baada ta masaa 4 Drogba amekaa nyumbani kwake anaangalia Tv anamuwaza Selina, kampenda kweli kweli, mara anaskia hodi akainuka kwenda kufungua ni Selina!
Selina akamwambia Ok let's give it a try! Drogba akafurahi akamkumbatia
ITAENDELEA SAA 12 JIONI