Stori zikaenda enda na wewe! Rasheedah yupo vlueless kuwa Kungwi anatembea na mumewe mtalaka, kungwi akaomba ushauri na maujanja kwa Rasheeda.
Kungwi: asee nimechoka ya kijijini huwezi nitaftia kiserengeti kimoja kikaninyooosha?! Kulalia mazee nahisi nazidi kuzeeka hata ma ujanja sina tena yote yameisha. Sisi wanawake tunaakili nyingi ila kwangu naona zinaisha!
Rasheeda: akacheeeeeka sana, Kungwi bwana kungwi wewe unachukuaje ujuzi kwa raia wa kawaida sasa?! Akampa maujuzi na nini pale Kingwi akaomba poo, kweli wajinga ndio walaji sio walwaji! Akajisemea Kungwi kimoyomoyo. Basi nimeshakuelewa ngoja aje mwanangu Maringo nitamwulizia ulizia afu nikuforwadie. Wakabadilishana namba za simu Rasheeda akaondoka zake.
Lunch time Maringo akapigiwa simu akatoka kwenda lunch na Mkuu wa mkoa, mkuu wa mkoa kakodi gari lingine akijua pale ataonwa na Mrembo, kweli mchezo wa karata 3 aliuweza. Maringo akaingia kwenye mchuma V8 gari lote linatikishika, big body kama K.Michelle wa Marekani, chura wa kumwaga! Mkuu wa mkoa anachizika kampeleka Royal Livingstone! Lunch na wewe Patric anamwaga ung'eng'e
Patric: unajua tangu nimekuona nimekupenda ghafla, usiku silali nakuwaza wewee
Maringo: we si umenitamani ndio maana haulali
Patric: hapana mpenzi huku anamshika mkono! Me nimekupenda bure kwa mapenzi yote
Maringo: na mkewako je
Patric: ah mke wangu yupo si tutafanya kwa siri!
Maringo: siri hiyo inakuwaje?! Uchi nakupa kwa siri alafu?! WhaT next?!
Patric: kwani wewe unataka nini?!
Maringo: unauhakika utaniweza?! Si unaniona?! Me najua umeoa na wala staki matatizo na mke wako kabisaa! Na najua umenitamani, ukishanibabua unasepa na sitakuwa na pa kukupata kwahiyo ombi lako nimelikataa! Hata mimi natamani pia kuwa na familia! Sio unitwange weee nizeekee Lusaka bila watoto
Patric: familia hata leo nakupa wala usiwe na wasiwasi ukitaka nyumba, gari, kazi nzuri kama hiyo ya bank anazingua meneja nakuhamisha kokote unakotaka
Maringo: akakumbuka jinsi Joe alivyomtenda kwa Kandi akaona huu ndio muda wa kulipiza! Akamjibu naomba nikufikirie j2 tuonane nikupe jibu akijua kesho anaenda kuongea na mama yake ampe maujanja! Little did she know!
Patric: nashukuru sana mpenz wakala pale akamrudisha ofisini akaondoka moyoni anafuraha kuwa sasa kile chombo anakitendea haki
Weekend ikafika Drogba Oga na Didie wakakutana kwa Oga wakaweka kambi kama kawaida! Stori stori na wewe
Oga akawa anajigamba kapata chuma kipya nyomi ya kufa mtu, wenzake wakamwuliza Selina vipi?!
Oga akawaambia Selina bwana hata simwelewi elewi muds mwingi nipo alone ila kwa huyu demu hapa nimenasa mpaka namdindisha ndotoni namfakamia mashambulizi ya kufa mtu nikiamka hamna kitu naota
Wenzake wakamcheeka oooo abeeeeeg! Oga abeeeeeg! U cray Ooooo! Huku wanaendelea kucheka!
Baadae Drogba akafunguka juu ya Selina kuna siku nimemwona yupo na mkuu wa mkoa wanaingia hotelini pale mjini me nilitoka kufuatilia vitu vya ofisini kwa hotel meneja alikuwa ananunua hisa za pale ofisini. Basi nikawaona ila wao hawakuniona wameshikana viuno na nini
Mdogowangu utakufa yule mkuu wa mkoa kitombi hatari anatembea na mama na kadada kamoja pale benki kwenu akaanza kukaelezea, Oga akajibu si Mrembo huyo! Dah kumbe mrembo nae anajidai hayumo kumbe yumo! Akajisemea Oga
Drogba akazidi kufunguka pia kampangia nyumba kamama kamoja kametokea kijijini kuna rafkiangu ni jirani wa huo mtaa wa kimada wa mkuu wa mkoa basi ni balaa tupu! Namhurumia mkewake Mary.
Didie akadakie Mary ndo yule nilitembea nae skuile au?!
Oga: eh na Didie nae anatembea na wake za watu!? We Drogba utammaliza mdogowako, i hope ur using protection oooo! My braza i dont want u to die oooo! I don't!
Drogba akampa ramani yooote waliopanga na pacha mwenzie didie, ah me wakati mwengine nakuwa nipo taiti nimefungia mtu sa huyu labda Kandi, Oga akashtuka Kandi tena?! Drogba akamwambia u know Kandi ey my gurl! Oga akachoka tangu lini? Akamwambia a month naaaaaw! Oga akajibu eiiii! Chinekeee i tell you naaaaw Droga you will die ooooo, stop it oooo!
Drogba akaendelea so wakati nipo na Kandi ma mchungaji Neema, Oga akajibu Neema Ooo! Mama Pastor Oooo! You Drogba sikufahamu! Aseee me sio ndugu yako oooo! This is too much oooo, Drogba Please Ooo! Stop this nonsense ooo abeg! Please my bro aaa, Didie talk to your half. He will go to hell Ooo! Didie hana usemi na yeye mgeni kwenye gaMe inabidi awe mpole
Drogba akafunguka unajua me angala nina 3 na natumia protection so nikizidiwa namgaia si unajua Yesu kasema tusiwe wachoyo so namgawia nusu yangu Didie hapa nae afaidi si unajua tunavyofanana hamna anaeweza notice tofauti yetu upo mbali sana, kwenye balls, mmoja ana balls ina kovu la rangi jeupe mwengine balls zake hazina kovu! Eh Oga akachoka! Labda kwasababu yeyr anajua kuwatofautisha kwasababu wamekua pamoja akaona hii kali
Wakaanza kudiscuss mambo ya kazini Drogba akamwambia Didie vipi mzee Masoud naskia ana expand horizon yake to Dubai and Accra Ghana na Lagos Nigeria! Mbona mambo yatakuwa mwake naskia mnasafiri nae pamoja na Joseph Braza hongera sana you being a finance manager Didie lazima upo proud!
Didie akajibu ndio am proud nimeiletea kampuni feza nyingi sema bado ngoja kwanza tutengeneze branch tutapata hela za kuwachapa watu. Kamamwuliza Oga vipi benk haujapata big fishes au upo buzy na Maringo?!
Oga: so far wapo 40 lakini kwa sasa ngoja kwanza wafike 100 ndio itakuwa nzuri kuendelea na plan yetu. We Drogba vepee?!
Drogba: ah me kwangu HR pale hamna kitu si unajua nipo Real estate hamna vitu kiviile ila wakija tutapanga deal. Drogba akaendeleza plan yake ya kuwazungusha michepuko wake. Oga akameuliza lini uta dettle down na uta settle down na nani?!
Drogba: this is not the time for settlement, bado sisi vijana wasogo sana, miaka 35 bado kabisa damu inawaka
Musa nae akajiskia mpweke, miaka 2 sasa hana demu, upwiru mwingi, hana pa kumpata demu akaamua atoke zake out angalau apunguze stress! Akaenda kulala Kayube Estate! Usiku amenda Dinner anakutana na mrembo anawaka kapiga bonge la makeup! Akaona uzalendo usimshinde akaenda kumsalimia, wakawa wamekaa pale wanakunywa lakini msichana alikuwa uncomfortable! Musa akawa haelewi kwanini, akamwuliza wewe ni Mzambia?! Akajibu hapana mimi nimetokea Mbuki na Faso! Akiwa katika maongezi akasikia mtu anamwita Evelyne! Njoo huku nimeshafika. Dada wa watu akamuaga Musa akaondoka. Musa akasema dah kweli me sina bahati, nikama nimeshika dhahabu alafu nikapokonywa ndani ya nusu saa! Akawa anamwangalia tu Evelyne anavyoishia.
Selina kama kawaida anamfundisha Caroline mambo yao ya ballett! Caroline amesha catch up na baba yake Jose ametoka, skuhiyo darasa lilipigwa saa 11 jioni mpaka saa 2 usiku ili tu abaki afanye alichoambiwa na mganga. Caroline anashangaa mwalimu aondoke leo?! Selina akaanza kujifanya anaumwa pale na nini! Akaomba alale anajiskia kizunguzungu, Caroline na huruma za kitoto akampeleka kulala guest room, Caroline akaendelea na mambo yake pale na nini akamsahau mwl akaingia kulala, Jose hakurudi sikuoyo alifichwa na Pendo. Usiku saa 6 kasoro kufika akashtuka anaelekea chumbani kwa Joseph anakuta hamna mtu, akakaa mpaka saa 7 usiku mtu hajarudi akazodoka, asubuhi akaamka fasta fasta akaandika kinoti kuwa amepata nafuu anaondoka akaweka mezani akasepa, Caroline kuamka akakuta kinoti, akasoma akacheka tu akakitupa kwenye dust-bin!
Maringo akatua kwa mama yake Rasheeda, wanaongea ongea na wewe, akampa ubuyu wote wa beans wake Joe alivyotembea na office mate akamwambia naona ofisi chungu mama roho yauma kama inataka kunitoka
Rasheeda: anamhurumia kweli lakini hana jinsi akamwambia hayo ndo taliyonifanya niondoke kwa baba yako, keshanipa talaka yangu sasa nimekuja kukaa hapa mjini, nikajapata bwana mzuuuri sana ananipenda hivi nilivyo
Maringo: akakasirika mama hapana asee hii ni ndoa sio relationship haukupaswa kuondoka sio vizuri kabisa! Huki analia maskin! Umefanya vibaya sana kaka Hachikoko na Luwi wakiskia hawatoelewa kwani umewaambia?!
Rasheeda: hata hawajui ndio maana nimekuja kutafuta nyumba nikapanga! Nitulie kwanza baada ya miezi 6 niwaite mje
Maringo: analia hakupenda wazazi waachane lakini atafanyaje sa ndio imetokea! Akawa analia pale anabembelezwa!
Rasheeda: mwanangu nashukuru kwamba umekua na umewaona wanaume walivyo, inabidi u fight for your happiness hata hawa viongozi wa dini na wa serikali hii ndio michezo yao. Wewe komaa kupata amani na furaha yako hizi tv na cartoons na fairy tale stories zinawaharibu watoto sana mnatafuta happily ever after ila hamjui happily ever after inapitia wapi? Inapatikanaje?! Ina fightiwaje?! Ina sacrificiwaje!? Hivyo hawaonyeshi kwasababu movie ni madaa 2 mpaka 3 labda kama sasa hivi naona kuna series ndio wanaeleza ukweli wa maisha!
Maringo: mama kichwa hapa kunaniuma sana wala usiongeze dozi nimeshajaa
Rasheeda: hata bado sijamaliza. Kakako Luwi nae ndo ipo juu ta mawe siku nitamwita naskia amechanganywa huko na kidada kimoja tatizo hamwongei na sisi tuwasaidie ila nashukuru kuwa umekuja na tutayamaliza hapa hapa.
Sasa una mabwana wangapi wamekutamkia wanakupenda?!
Maringo: so far 2 na Joe wa 3
Rasheeda: hapo ndio napopataka, mama Mungu kakupa kiiila kitu, tumia hizi fursa we mwana, embu nipe status za hao dagaa wako
Maringo: kuna baba limoja sijui linani ngoja nikionana nae kesho nitakwambia ila ni Mzambia.
Mwengine anaitwa Oga tunafanya nae kazi bank ni Mnigeria, mama akaguna mmh! Mwengine ni bank manager ila nimeambiwa anaukimwi naogopa hata kumshika
Rasheeda: akacheeeka dah kweli mtoto sinae hapa! Enhe na joe wa 4 sio?!
Maringo: ndio mama
Rasheeda: yani hapo usiache hata kimoja! Kila mmoja mtumie kwa nafasi yake ila usiwagongeshe, ukiwagongesha either watakuua au watauana, na kila mtu kamata maneno yake kisawa sawa! Na usichanganye neno la oga kwa bank manager wala hilo zee nenda nao sawa hakikisha unapewa kiiila kitu roho yako inataka usisahau kutumia condom, habari ya mchezo wa kitandani ajiri kungwi au nenda kwa mama Pendo namba yake hii atakupa somo zuri la kitandani, kesho amkia kwake urudi me mamako siwezi kukupa somo la kitandani ni najisi!
Ila wote wakamate usiache hata moja kitandani ufanye vizuri ukamate ahadi zao na uzidai, ohoo! We shangaa mjini hapa itarudi kwa babako Manoa kijijini ukalime me nishasema sirudi kabisaa! Alafu mambo ya marafiki hata usi entertain kabisaa! Hao ndo wachawi wakubwa kaa mwenyewe kivyako vyako ukishindwa niite mie mamako nitakuja kukupa kampani! Ukijidai unashika moja utakonda roho wewe! Joe akicheat unakonda roho utaporomoka kiafya utachukia wanaume wote kwa selfish ya mtu mmoja, mwanangu me mama yako nakwambia find your happiness kwa akili usije pata magonjwa ya moyo na ma kisukari yasio na sababu kisa unapenda na kuwaza umetendwa acha huo ujinga fight for your happiness narudia fight for your happiness kila mtu anakufa hakuna kinachobaki hata hawa wamama wa dini nao wanakitembeza sana si tunawaona bwanaa ndio ivyo kinga lazima la hasha mkapime mkiwa wote sio mmoja anaenda mwengine anabaki ndio mwanzo wa kunadilishiwa majibu ukauzoa ukimwi shauriako
Maringo: akachoka na ushauri wa mama yake huenda divorce ilimsumbua sana na akili zake haziko sawa. Akaona bora aongee na kungwi huenda yeye ndo kidogo akili zipo sawa
Usiku wamekaa wanaangalia Tv wanaskia mtu anafungua mlango, mama hana wasiwasi anajua ni Patric, Maringo anashangaa mwizi nini?! Kuingia tobaaaa ni Patric! Maringo anashangaa, Patric hakumwona maana alipoingia alienda moja kwa moja kwa Rasheeda akaanza kumshika shika anambusu! Rasheedah kumzuia Patric anashangaa leo vepee akamwambia anataka kukuintroduce kwa mtoto wangu wa kike na wa pekee huyu hapa, Patric kumwona tumbo lilijaa mavi, Maringo kumwona akachoka mara 100, mama mtu hajui hili wala lile, anaendelea tu Maringo huyu ndio mpenzi wangu anaitwa Patric! Patric huyu ni mwanangu anaitwa Maringo, Patric akampa mkono nimefurahi kukufahamu. Maringo akamwangalia akaanza kushikilia tumbo na mdomo anaskia kutapika akatapika matapishi mengine yakaangukia kwenye mkono wa Patric Bwaaaaaaaaaaah!
ITAENDELEA SAA 11 JIONI