Money Penny
JF-Expert Member
- Jun 20, 2016
- 17,280
- 16,556
Hii CD ya sasa hivi, Prison break, 24, zitasubiri miaka 1000!
NI MVURUGANO WA KUFA MTU!
MSOMAJI USICHOKE, TWENDE MPAKA MWISHO, UKIFIKA KATIKATI USICHUKIE WALA KUKIMBIA, NDIO MAISHA!
KIJIJINI:
Kashkash letee, natena letee
Kashkashi letee nasema lete,
Leteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
Mdundiko ndani ya nyumba watu wanajimwagaje sasa! Kila mtu kwa sehemu yake, kila mtu na mtu wake, wengine wapenzi humo humo wanadandiana, kiruu, mwenyekiti wa kijiji nae yumoo, anayarudi na mke wake, watoto wa shule ndo kabisaa, wengine wanasaidiana kupiga ngoma na madebe, tobaaaa! Ni vurugu, ni mvurugano, ni vumbiii cha! Sio kwa vurumai lile, kila mtu na upande wake, ingekuwa enzi za mziki Darassa angeimba sio Chui sio Simba sio mamba he!
Ng’ombe mzima keshaliwa, mbwa anatafuta mifupa, sio kwa sherehe lile! Cha! Wanakijiji oyooooooooooooooooooooo, wanakijiji vepeeee! Alikosekana mzee wa sengeli tu maana sio kwa mifuraha ile, kijiji kimeshinda, kimeshinda kabisa, na mwenyekiti wa serikali za mtaa alipewa pongezi na mkuu wa mkoa, akatoa ng’ombe wa 3, soda kreti 30, bia kreti 40 na chibuku, wale wanywe wafurahi, sio kwa ushindi ule!
Mke: Nipe talaka yangu nakwambia, nipe!
Mume: Sikupi hata moja!
Mke: Sitaki kuishi na wewe tena nipe nirudi kwetu
Mume: Nishakwambia sikupi we mama kama unataka kwenda kwenu nenda wasalimie salama
Mke: Yani hapa piga ua talaka utatoa nakwambia, usinichezee ivoo, la sivyo nitakuonyesha wewe nitasahau nimezaa watoto 3 na wewe, mwanaume wa namna gani wewe Malaya mkubwa kabisa, hauna hata maana unatembea na kijiji kizima sa ajabu una ukimwi
Mume: kama mimi nina ukimwi hata wewe unao, mwanamke kukitembeza kama kinalika sasa, haujiheshimu hauheshimu ndoa wala nini! Hata kama watoto hawapo uliambia ufungulie jiko hilo?
Mke: wewe ongea wee ukimaliza andika talaka fasta niende kwangu
Mume: uende kwako au uende kwa huyo mwanaume unaemwona wa maana, hivi mama subira una akili kweli wewe?! Ndoa ya miaka 40 unaipiga teke? Mimi niulivyoozeshwa kwenu nilkiambiwa nisitoe talaka, kama unataka kurudi kwenu nenda mwenyewe nitakauja kuongea na kaka zako, kwanza hata wazazi hawapo
Mke: nakupa dk 10 andika talaka naondoka sina raha na wewe tena mshenzi mkubwa!
Mume: akamwangalia tu anamhurumia, akamjibu nakupa talaka kwa shingo upande, nenda kwa huyo wa maana utaja niambia usishangae ukirudi ukakuta chombo kingine
Mke: fanya haraka kumbe ulishapanga nitoke uingize mwengine aya fanya haraka
Mume: kaandika talaka ndani ya dk 15 kampa, nakutakia maisha mema na huyo bwege wako!
Mke kaingia ndani kafunga virago, ndukiiii, akafika mbele anaona mziki wa kijiji, eh! Leo kwani kuna nini jamani?! Kuangalia burudani na nyama zaliwa kila aina, anajiuliza imekuwaje? Amekuwa buzy sana na kazi za home hata yeye na mumewe hawajui? Katika kuangalia angalia anamwona mshefa wake! Tobaaa na huyu yupo huku tena na mwenyekiti wa kijiji, sasa ntaenda wapi maana huu mguu ndio wake,
Akaona bora ajidibe kwenye mziki, ili aonekane, kabla hajaingia mkuu akamuona, akatoka pale alipokuwa amekaa mke mtu akamfuata kwa nyuma akakuta anaingia kwenye gari nay eye akaingia, wakakaaa weeee huko ndani weeee, bila dereva, mkuu akashuka akaenda kuaga kwa mwenyekiti haooo nduki!
KUNGWI!
"Mapenzi ni kama SWIMMING POOLS usijisumbue kujua NANI aliogelea kabla yako! nani mnaogelea naye kwa wakati huo au nani ataoga ukitoka, WEWE ENJOY KUOGELEA TU MAMA, haina kuremba"
Kungwi akaonekana yupo buzy anaitendea kazi hela yake
Maisha yenyewe ya sasa sheedah tupu, we fanya yako,. Zaa watoto walee, ilimradi bwana anasomesha,a analeta msosi home, we una shida gani? Haya mambo ya kaangalia nani kapita, sijui rosa kapitaaaaaaaaaaaaaaaaa, bwashee kapitaaaaaaaaaaaa, maria kapitaaaaaaaaaaaaaa, Nancy kapitaaaaaaaaaaaaaaaaaaa shogangu ndoa haimalizi mwezi hio utarudi kwenu mwenyewe! We fanya yako, afu tabia za watoto wa dot com mnachungulia simu ya mwanaume sijui mnapokea mtakufa asee!
Kungwi kaendelea na yake yale ya ndani mabayo ni PG 18+ kama kawa kama dawa mrembo akaelewa somo, mashangazi wapo nje wanasubiria mwali amalizwe shangazi nae achukue zamu yake!
Kungwi alipotoka simu na yeye, haloo mpenzi za kwako?
Mume: salama za kushinda?
Kungwi: mbaya, nimekumiss kweli hapa nimetoka kwenye somo
Mume: karibu kwangu
Kungwi: mh! Huyo mkeo hayupo kweli?
Mume: nimeshamtalaka leo asubuhi alipoenda sippajui labda kaliwa na simba msituni ila najua mguu ule alikuwa anaenda kwa Yule boya wake anaemwona wa maana, me saivi bachelor mzee!
Njoo baby nikufanye malkia wa nguvu kwenye hekalu langu
Kungwi: nakuja nipe nusu saa!
Kungwi kakata mitaa na yale mavumbi ya kijijini Zambia , kufika kama chiriku, mavumbi mpaka usoni, dah ama kweli, wengine wanavikimbia kumbe wenzao wanavikimbilia kwa miguu. Kufika haangalikiki utadhani alikuwa anacheza mpira wa miguu kwenye michanga, ikabidi Yule mume acheke tu maana sio kwa mwendokasi ule! Ahahahaha, akaingia ndani akatoka na kiti na maji ya kunywa, pole best yangu, kungwi akakaa chini akapewa maji ya kunywa, wakawa wanapiga stori pale na nini, Mume anajieleza ujinga wa mwana mke alieacha ndoa akikimbilia kwa mkuu wa mkoa! Tobaaa kungwi akazidi kutega maskio, stori stori na wewe, kungwi kimyaaa!
Haya karibu nyumba sasa ni yako, Kungwi mh! Akaguna, asante ila me leo sio mkaaji, watoto nimewaacha mwenyewe lazima nirudi kwanza nikaangalia vepee wasije unguza nyumba na hivi kupika hawajui sijui itakuwaje usiku
Mume: wote mje make hapa me kukaa pekeyangu kama jinni hata sipendelei
Kungwi: sawa ngoja nijipange basi,
Mume: ujipange nini? Me ntakusaidia kuhama
Kungwi: sawa ngoja niwapange kisaikolojia watoto alafu tunahamia siku si nyingi, wakakubaliana pale wakaingia ndani! Mziki ukaanza, kungwi tenaaa! Sio wa masihara!
MJINI:
Meneja: Dada karibu
Dada: asante sana
Meneja: interview ikaendelea pale na nini, dada akajibu maswali kwa ufasaha, ikaingia interview ya vitendo! Dada akaipiga vizuri, akaishia kuajiriwa
Meneja: keshoa subuhi saa 3 uje usaini mkataba wa muda alafu uanze kazi
Dada: asante sana akaondoka kwa furaha akimshukuru Mungu!
HR Office:
Kandi: shogangu leo watu mdebwedo, kha! Nyomi kama ile balaa nina njaa hatarious!
Mrembo: yani acha tu hii interview mwendo kasi ajabu, eh shoga umeona msembwende ulee! Kha! Yule lazima ataajiriwa sio kwa yale mavi
Kandi: nimeona shostito! Kha! Yule kaongeza kama Kim Kardashiana au? Maana haipatikani nchi nzima au Yule mbongo nini maana ndo zao kama sio mbongo basi msoweto!
Wote wakaishia kucheka! Haya tutajionea ya ahera maana ya duniani mengi!
Kandi: Yule pale boss lazima atamuajiri na akimwajiri tu anakuwa sakramenti yake, ai jamani! Acha tu wakaendelea zao na kazi kama kawaida!
Musa: Oya niaaaje mwana,
Oga: Poa tu shega, wapi iyo?
Musa: Ah mie nimetoka hapo mjini mara moja boss alinituma, vipi za nyumbani? Selina hajambo?
Oga: Ah Selina bwana anazingua kweli ila basi tu
Musa: Kuna nini tena mwenzangu mapema hii mshaanza kubutuana?
Oga: Ah acha tu, ila kuna kinu kimoja nimekiona mitaa ya kati acha kabisa weka mbali na watoto!
Musa: eeeeh! Wachaa, sasa umefanyaje?
Oga: yani nilipomwona tu nikajaa! Kama simtanki, nilikuwa kwenye gari na dereva nikamwomba asimamishe, nikashuka kumsalimia, kapolee kanaona aibu chenyewe!, nikamwomba namba yake, akanipa nikambipu pale pale, akaisave nikamwambia tutawasiliana, tukasepa me na dereva, njiani
dereva: mdogowangu utakufa na nyota yako ya chipsi mayai, acha kuvamia chura hao, shauriako!
Oga: sawa kaka, ila si unajua vijana na damu kuchemka!
Dereva: najua ila aste aste we si upon a selina naskia mnakaria kuoana
Oga: ah selina Yule acha kabisa, mambo alionifanyia bora nirudi kwetu tu Nigeria, nikaoe kule ila huyu mdoli wa kibantu ni hatari hii itakuwa namba ya Soweto kama sio Tz! Kha!
Wakacheka pale na dereva wakarudi ofisini.
Musa: eh makubwa we Oga embu tulia na selina kwanza huwezi jua awa vyura wapo tu! Huwezi jua chura ya nani ile
Kufika mtaa wa 3, dada wa watu akapigiwa simu,
SIMU: uko wapi?
Dada: nipo mjini nimetoka interview
SIMU: ok pitia hapa ofisini nataka kuonana na wewe
Dada: sawa
SIMU: ikakatwa
Dada akachukua taxi moja mpaka alipoitwa!
Moja mbili tatu…. Enhe! Moja mbili tatu…. Safiii
Moja mbili tatu…. Enhe endelea ivo ivo, na wewe pia mikono ufanye vizuri unakosea kosea, enhe namna hiyo.
Eh nani we dada, vipi mbona haufanyi mazoezi? Haya njoeni huku upeesi, acheni hayo maongezi, wakaja wakawa wanafanya mazoezi,
Safi sana, leo mmenifurahisha sana kuliko siku zote, kesho tunaendelea na zoezi lingine ambalo litatusaidia stejini kwenye kucheza, sawa? Wakaitikia sawa! Haoo wakaondoka!
Mwalimu Selina nahitaji private class naona siwezi master level hii
Selina: sawa hamna shida, ila itabidi unilipe
Mwanafunzi: ngoja basi niongee na baba atakulipa ni siku gani na gani?
Selina: tufanye jumamosi masaa 4
Mwanafunzi: sawa hamna neno!
Karibuni wageni, karibuni sana,
Wageni: asante, huku wanaangalia bidhaa wanazouza
Hii bei gani, wanatajiwa, hii bei gani wanatajiwa, hii bei gani, wanatajiwa!
Basi wakajaribisha pale wakalipia wakaondoka.
Leo mauzo sio mabaya, afadhali maana sasa sijui ningefanyaje!
Mara simu ikapigwa, Pendo uko wapi shogangu
Pendo: nipo hapa kwenye kibanda change, nambie
Selina: ngoja kwanza nakuja hapo hapo nikupe ubuyu!
Pendo: haya karibu
Mkuu wa mkoa nae alionekana yupo na mke mtalaka, wakafika kwenye nyumba nzuuuri ya chini, mke mtalaka akijia kuwa ndio kwa mkuu wa mkoa, kumbe hamna kitu, kapangiwa fasta fasta kuepusha shari! Akamkaribisha pale na begi lake 1, karibu akamwonyesha vyumba vyote 3, na jiko na sebule, akamwambia kwenye fridge kuna kila kitu, wewe tu ujisevie, mimi natoka nitarudi kesho leo sitaweza si unajua nina shughuli za kiofisi?
Nje kuna mlinzi anakuja saa 12 jioni anaondoka saa 1 jioni, hii nyumba ni yako asikusumbue mtu!
Mke mtalaka akafurahi, akamshumu mkuu wa mkoa, mkuu akampa mil 3 akasepa huyoo, mke mtalaka akasema kweli, nilipomuacha Yule mzee sikuwa nimekosea! Vitu kama hivi ningevipata saa ngapi na uzee huu ningekufa nywele ile nyumba ya miti akhaa! Nimeteseka ujanani na uzeeni pia? Akawa anaiangalia ile nyumba anapanga jinsi atakavyoibadilisha kikwake kwake, ah maisha mazuri.
Mchungaji: Karibu, karibu kiti, karibu sana
Muumini: asante baba mchungaji,
Mchungaji: enhe niambie! Kuna shida gani maana ulisikika vibaya kwenye simu kama kuna dharura
Muumini: yani acha tu baba mchungaji, ndoa inasumbua babaa!, yani nimeshamfuma mume mara 5, nab ado mnaniambia kuhusu kusamehe jamani me ntaweza wapi?
Mchungaji: samehe tu mama dunia hii sio yetu na siku tutarejesha mrejesho kwa Mungu
Muumini: jamani yani sasa ndoa ipo kama kiazi mviringi sasa, hata sina raha ipo ipo tu, watoto ndo hao wadogo basi nakaaga tu mwenyewe!
Mchungaji: vumilia mama haya yanapita
Muumini: yani me siwezi kwa sasa itabidi nitafute furaha zangu tu!
Mchungaji: mama vumilia, tafadhali haya yote ni maisha
Muumini: akainuka fyeee akaondoka bila kuaga analia tu
Mchungaji akabakia anatoa macho tu!
ITAENDELEA