Hotuba ya Magufuli saa 6 mchana ina '' implication'' kwa tukio la 7 mchana huo. Key words '' mtu, msaliti, risasi''
Pili, ikiwa Magufuli hakuhusika alitakiwa ajitenge na uovu ule, ironically akawa cheerleader hata kwenye matibabu
Tatu, watu waliokwenda kumuona Lissu Nairobi baadhi walikutana na kadhia, nasikia hata Maza alinuniwa.
Nne, hakuna maelezo yule kijana wake mpendwa DAB alikuwa Dodoma anafanya nini, yeye hajanusha
Tano, wahusika akina slow slow wangeshavalia njuga hasa kipindi hiki wakiwa na mawaa na wana mtandao
Sita, Polisi walioficha Kamera walikuwa chini ya utawala wa Magufuli
Saba. Magufuli alikuwa na nguvu za kuagiza uchunguzi wa haraka na wa kina ikiwa hakujua nani alifanya
Nane, Bunge lililazimisha kuziba nafasi ya Tundu Lissu makusudi kabisa, Magufuli alikuwa na uwezo wa kuzuia
Tisa, baada ya uchaguzi wa 2020 vyombo vya magufuli vilimfuatilia Lissu tena akikimbilia ubalozi wa EU.
JokaKuu