Mwl.Nyerere alifanya jambo hili mbele yangu mwaka 1998

Mwalimu katumia gari aina ya pickup 1998? Nahisi kama umeongeza chumvi.

tatizo la wabongo ndio hili hawaamini eti unahisi, amini bwana mbona kitu kipo directly wewe bado mbishi tu, haya kesho anakwenda muscati kutafuta nchi ya kukimbilia akiachia uraisi.
 
Ilikuwa mida ya saa 9:30 alasiri,pale maeneo ya Musoma alliance, mwalimu alipita na gari yake aina ya Land rover akiwa na dereva wake,akamuona mama mmoja pembeni mwa barabara akiwa na ameshikwa na uchungu na hatua za mwisho za kujifungua,mume wake akiwa amesimama pembeni,kwani alikuwa akimsindikiza hospitalini kwa baiskeli,hali ilipokuwa mbaya akamshusha ili ijifungue.Mwalimu akamwamuru dereva kusimamisha gari,akasogea kwa karibu na kumwamuru dereva kumpakia yule mama na kumkimbiza hospitali mara moja. Akampa dereva pesa anunue unga wa ulezi ili utumike kumpikia uji yule mama atakapojifungua,Mwl yeye akabaki pale barabarani kwenye kona ya msm alliance.Magari yakaendelea kupita,yale ya serikali walipokuwa wakimwona mwalimu wanasimama na kutaka kujua kulikoni ikiwezekana aingie kwenye gari.Wote walipewa jibu hili" Nenda,kwani mama aliyekuwa anajifungua hapa hamkumwona?".
Lakini pia hali ya maisha aliyoishi mwl,nani leo hii rais mstaafu anaweza kutumia LandRover Pick up?

This is what is called, "leadership by example".
Hii hata wengi wa viongozi wa Dini hawawezi kufanya kama alivyofanya Nyerere.
Ndo maana Kanisa Katoliki liko Kwenye Mchakato wa Kumfanya Nyerere, kuwa MWENYEHERI.
 
Ilikuwa mida ya saa 9:30 alasiri,pale maeneo ya Musoma alliance,wakati huo nikiwa natoka ktk kiwanda cha Mara Oil(nilipokuwa nafanya kibarua ingawaje ilikuwa child labour kwani wakati huo nilikuwa na miaka 16) mwalimu alipita na gari yake aina ya Land rover akiwa na dereva wake,akamuona mama mmoja pembeni mwa barabara akiwa na ameshikwa na uchungu na hatua za mwisho za kujifungua,mume wake akiwa amesimama pembeni,kwani alikuwa akimsindikiza hospitalini kwa baiskeli,hali ilipokuwa mbaya akamshusha ili ijifungue.Mwalimu akamwamuru dereva kusimamisha gari,akasogea kwa karibu na kumwamuru dereva kumpakia yule mama na kumkimbiza hospitali mara moja. Akampa dereva pesa anunue unga wa ulezi ili utumike kumpikia uji yule mama atakapojifungua,Mwl yeye akabaki pale barabarani kwenye kona ya msm alliance.Magari yakaendelea kupita,yale ya serikali walipokuwa wakimwona mwalimu wanasimama na kutaka kujua kulikoni ikiwezekana aingie kwenye gari.Wote walipewa jibu hili" Nenda,kwani mama aliyekuwa anajifungua hapa hamkumwona?".
Katika siku hii ya leo ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwl.Nyerere,nimeamua kuwaletea ushuhuda huo juu ya moyo wa utu aliokuwa nao mwalimu.Lakini pia hali ya maisha aliyoishi mwl,nani leo hii rais mstaafu anaweza kutumia LandRover Pick up?
Ah wapi nani wa sasa wa kusimama!? wanaobserve protacol!! Viazi tupu!
 
nini kimekuliza? alivyomsaidia huyo mama au kuna kingine kinakuliza? Nyerere legacy na wewe mteja pia!

Ni mara chache kama sio hakuna kiongozii wa juu kufanya aliyofanya Mwl. Kilichoniniliza ni kitendo cha kumsaidia huyo mama. What a soul
 
kama kumbu kumbu zangu zipo sawa ilkuwa ni gari aina ya 110 station wagon , alipenda sana kuja na hiyo gari musoma , joseph butiku akiwa ndie RC Mara kabla ya bwana MMoja anitwa Balozi Lugoye, Mwalimu alikuwa simple sana Niliwahi kumuona pale Makoko seminary akiwa na Askofu marehemu Justine Samba, yeye akaingia shambani kuwasaidia wanafunzi kulima kitu ambacho hata askofu alishangaa.
Mkuu naifahamu sana hiyo gari. Ilikuwa petrol engine V8. Mwalimu aliachana nayo muda mrefu kabla ya 1998 alipogundua kuwa inatumia petrol kupita kiasi. Kama sijasahau, katibu wa mwalimu mzee Kasori ndiye alikuwa anaitumia baada ya mwalimu kuachana nayo. Nilisema Saganka ameongeza chumvi alipoandika kuwa ilikuwa pickup.
 
Usisahau mkuu, alipong'atuka alianza ukulima. Mkulima yeyote aliyekusudia na mwenye uwezo ni rafiki kipenzi cha pick-up kokote duniani.
Kama ni kusomba mazao, alitumia trailer la tractor yake ambayo mpaka leo ukienda Butiama utaikuta na pia alikuwa na Isuzu Lorry tani 7 alilopewa na mkoa wa Iringa kama zawadi baada ya kustaafu urais. Kwenda shambani alitumia Nissan yake station wagon. Hakukuwa na cha pick up pale. Narudia tena, Mwalimu was humble lakini Saganka kaongeza chumvi.
 
Hapo Mwalimu alikosea sana kama nia yake ilikuwa kuwafundisha jambo fulani hao viongozi! Mwalimu pengine aliwaza kuwa hao wanafunzi wake wataelewa dhumuni la huo mwito.

Kwa upande mwingine, hayo yalikuwa matumizi mabaya ya mali za umma; kwa sababu safari za viongozi watatu wakubwa kama hao ziligharimu pesa nyingi za watanzania. Sasa kuwaita na kuwapa mapapai, kisha kuwaacha warudi mwakwao, ilikuwa ufujaji wa mali.

Lazima atakua alikuja kufafanua maana ya huo mwito kwa hao viongozi watatu. Na kwa upande wa matumizi mabaya ya mali za umma, ni vema alitumia hizo gharama kuwafundisha hao viongozi watatu (3), kuliko hayo matumizi mabaya yangeachwa yakaenda kwa viongozi hamsini (50), mia (100), mia tatu (300) nk wasio na wakuwakemea.
 
Kama ni kusomba mazao, alitumia trailer la tractor yake ambayo mpaka leo ukienda Butiama utaikuta na pia alikuwa na Isuzu Lorry tani 7 alilopewa na mkoa wa Iringa kama zawadi baada ya kustaafu urais. Kwenda shambani alitumia Nissan yake station wagon. Hakukuwa na cha pick up pale. Narudia tena, Mwalimu was humble lakini Saganka kaongeza chumvi.
Nilichoona ni pick up,kama zamani ziliitwa Hammer sasa hiyo mi sijui,nitaongea nilichoshuhudia,sina haja ya kumpamba mwl kwa pickup,sifa alizonazo zinatosha kabisa na wala haziihitaji pickup.Nilikuwa na miaka 16 na ubongo wangu ulikuwa fresh.Usipoamini sina namna nyingine.
 
Ilikuwa mida ya saa 9:30 alasiri,pale maeneo ya Musoma alliance,wakati huo nikiwa natoka ktk kiwanda cha Mara Oil(nilipokuwa nafanya kibarua ingawaje ilikuwa child labour kwani wakati huo nilikuwa na miaka 16) mwalimu alipita na gari yake aina ya Land rover akiwa na dereva wake,akamuona mama mmoja pembeni mwa barabara akiwa na ameshikwa na uchungu na hatua za mwisho za kujifungua,mume wake akiwa amesimama pembeni,kwani alikuwa akimsindikiza hospitalini kwa baiskeli,hali ilipokuwa mbaya akamshusha ili ijifungue.Mwalimu akamwamuru dereva kusimamisha gari,akasogea kwa karibu na kumwamuru dereva kumpakia yule mama na kumkimbiza hospitali mara moja. Akampa dereva pesa anunue unga wa ulezi ili utumike kumpikia uji yule mama atakapojifungua,Mwl yeye akabaki pale barabarani kwenye kona ya msm alliance.Magari yakaendelea kupita,yale ya serikali walipokuwa wakimwona mwalimu wanasimama na kutaka kujua kulikoni ikiwezekana aingie kwenye gari.Wote walipewa jibu hili" Nenda,kwani mama aliyekuwa anajifungua hapa hamkumwona?".
Katika siku hii ya leo ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwl.Nyerere,nimeamua kuwaletea ushuhuda huo juu ya moyo wa utu aliokuwa nao mwalimu.Lakini pia hali ya maisha aliyoishi mwl,nani leo hii rais mstaafu anaweza kutumia LandRover Pick up?

Miaka 16 unafanyakazi tena ajira ya watoto kama ambavyo umesema? Shule uliishia darasa la ngapi? na leo hii uko wapi? unajua kutumia Compyuta!! Bado nina maswali mengi ya kujiuliza juu yako!!
 
Kumsaidia Mama mmoja aliyekuwa anajifungua,kutumia landrover pick up haitoshi kusadikisha kuwa alikuwa kiongozi mzuri sana. kimsingi ungetuambia baada ya kuona tukio lile,aliweka sera endelevu ili kuondoa hali kama hii nchi nzima. Elewa kwamba kama yeye alimwona huyu mmoja,the same day,same time kuna mwanamke mwingine tandahimba,mbinga,kiteto.may be walikuwa na tatizo kama hili,lakini hawakufikiwa na msaada aliotoa Nyerere
Musoma alliance

Unajua hata mwizi anayeiba kwa kutumia silaha,kukatisha maisha ya watu,mwisho wa siku naye anakwenda kutoa msaada,au kutoa sadaka,haimfanyi mtakatifu kwa sababu katoa msaada.
 
Ni kweli nilikuwa na miaka 16,niliacha shule wakati huo kwa ujeuri tu nikiwa form two mwanza sec.Baada ya kusota takribani mwaka mzima huku nikifanya kazi za shuruba katika kiwanda cha mara oil nakulipwa sh.700 kwa siku,nikaamua kumwomba kaka anisamehe na ikiwezekana anisaidie nirudi shule.Kwa kunisema saaana akaamua kunirudisha tena shule mwaka 1999,kidato cha pili.Nikasoma vizuri,nikapata div 1 ya 16 final,nikachaguliwa kujiunga f5 pale nsumba-hgl(High Government Leaders),nikamaliza 2004.Nikapata div.1 ya 9,nikaomba political science udsm,na law KIU(Kampala International University),nikakosa udsm,nikapata KIU.Bahati mbaya the same same year,sponsor wangu akafariki,nikashindwa kwenda KIU.Nikabaki mjasiliamali hadi mwaka 2007 nilipojiunga THE MWALIMU NYERERE MEMORIAL ACADEMY,baada ya kuvutiwa na kozi ya "POLITICS AND MANAGEMENT OF SOCIAL DEVELOPMENT"(Bachelor).
Nikamaliza mwaka 2010.Leo hii nipo mahali fulani nafanya kazi huku kila jioni na-attend course ya Public Relation ngazi ya Master's Degree ,najua kutumia computer,na kama bado una maswali mengine uliza nitafafanua.Je bado una wasiwasi na uelewa wangu?Ninachokuomba ukiweza niunge mkono nichukue jimbo la serengeti mwaka 2015 kupitia cdm.
 
Kumsaidia Mama mmoja aliyekuwa anajifungua,kutumia landrover pick up haitoshi kusadikisha kuwa alikuwa kiongozi mzuri sana. kimsingi ungetuambia baada ya kuona tukio lile,aliweka sera endelevu ili kuondoa hali kama hii nchi nzima. Elewa kwamba kama yeye alimwona huyu mmoja,the same day,same time kuna mwanamke mwingine tandahimba,mbinga,kiteto.may be walikuwa na tatizo kama hili,lakini hawakufikiwa na msaada aliotoa Nyerere

Unajua hata mwizi anayeiba kwa kutumia silaha,kukatisha maisha ya watu,mwisho wa siku naye anakwenda kutoa msaada,au kutoa sadaka,haimfanyi mtakatifu kwa sababu katoa msaada.
Hii kazi uliyochagua ya kuwakashfu marehemu ni hatari kuliko kwenda haja ndogo juu ya quran.Ukweli nakwambia.
 
Kile kilikuwa kichwa bana. Weacha tu. Sio nazi za leo.

Afadhali hawa wa leo wangebakia na vichwa vyao vilivyojaa pumba tu lakini pia wanatuibia maliasili zetu na kuficha ughaibuni huku sisi tukifa na njaa; halafu wanajidai wanasafiri kwenda kututafutia misaada kumbe wanakwenda kuangalia usalama wa mali walizokwiba!! Ole wenu arobaini yenu itakapofika mtalia na kusaga meno!!
 
nini kimekuliza? Alivyomsaidia huyo mama au kuna kingine kinakuliza? Nyerere legacy na wewe mteja pia!
wewe ni wakili wa shetani! Kwani mwenye heri mwl, Julius Nyerere akisifiwa wewe inakuuma nini?? Walimuita 'mtukufu rais, akajibu mwiko kuniita mtukufu, mtukufu ni MUNGU PEKE YAKE, mimi niiteni MWALIMU!' rip mwalimu, pray for us, na wasamehe wote wanaokukashifu!!
 
  • Thanks
Reactions: ral
Back
Top Bottom