Mwl.Nyerere alifanya jambo hili mbele yangu mwaka 1998

Ilikuwa mida ya saa 9:30 alasiri,pale maeneo ya Musoma alliance,wakati huo nikiwa natoka ktk kiwanda cha Mara Oil(nilipokuwa nafanya kibarua ingawaje ilikuwa child labour kwani wakati huo nilikuwa na miaka 16) mwalimu alipita na gari yake aina ya Land rover akiwa na dereva wake,akamuona mama mmoja pembeni mwa barabara akiwa na ameshikwa na uchungu na hatua za mwisho za kujifungua,mume wake akiwa amesimama pembeni,kwani alikuwa akimsindikiza hospitalini kwa baiskeli,hali ilipokuwa mbaya akamshusha ili ijifungue.Mwalimu akamwamuru dereva kusimamisha gari,akasogea kwa karibu na kumwamuru dereva kumpakia yule mama na kumkimbiza hospitali mara moja. Akampa dereva pesa anunue unga wa ulezi ili utumike kumpikia uji yule mama atakapojifungua,Mwl yeye akabaki pale barabarani kwenye kona ya msm alliance.Magari yakaendelea kupita,yale ya serikali walipokuwa wakimwona mwalimu wanasimama na kutaka kujua kulikoni ikiwezekana aingie kwenye gari.Wote walipewa jibu hili" Nenda,kwani mama aliyekuwa anajifungua hapa hamkumwona?".
Katika siku hii ya leo ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwl.Nyerere,nimeamua kuwaletea ushuhuda huo juu ya moyo wa utu aliokuwa nao mwalimu.Lakini pia hali ya maisha aliyoishi mwl,nani leo hii rais mstaafu anaweza kutumia LandRover Pick up?

Mbona huwasifiiwazazi wako waliohangaika kukulea mpaka hapo ulipo? hilo la kumsaidia mtu ni la kawaida yeye kama binadamu. sio hoja ambayo inatufanya tumkumbuke.... wewe naye ni mateka miongonimwa mateka wa Nyerere legacy
 
na wale walio kufa kagera je unakumbuka

Mimi nawakumbuka sana kwa vile nina ndugu waliopoteza maisha yao kwenye vita ya Kagera, walipigana kwa moyo wa utaifa kwa vile walikuwa wanajua kua nchi hii ni yetu sote. Sidhani kama hilo linawezekana leo kwa vile nchi hii si yetu sote tena! Uongozi wetu ndio hutujengea utaifa wetu pia; tunapokuwa na uongozi goigoi basi hata utaifa wetu huyumba. Ukweli ni kuwa iwapo ningempa Nyerere A- kwa uongozi, basi Mwinyi na Mkapa wangepata B- ambapo Kikwete angepata lower marginal D-.
 
Unamkumbuka mwalimu Malalika wa alliance miaka hiyo ya 90?
Sikusoma alliance,ila niliwafahamu baadhi ya walimu akiwemo Wandiba-bookkeeping na commerce pamoja na yule mjaluo aliyekuwa headmaster baadae Afisa elimu mkoa(Otieno)
 
Mwalimu katumia gari aina ya pickup 1998? Nahisi kama umeongeza chumvi.

kama kumbu kumbu zangu zipo sawa ilkuwa ni gari aina ya 110 station wagon , alipenda sana kuja na hiyo gari musoma , joseph butiku akiwa ndie RC Mara kabla ya bwana MMoja anitwa Balozi Lugoye, Mwalimu alikuwa simple sana Niliwahi kumuona pale Makoko seminary akiwa na Askofu marehemu Justine Samba, yeye akaingia shambani kuwasaidia wanafunzi kulima kitu ambacho hata askofu alishangaa.
 
Daima alikuwa anatekeleza yale aliyokuwa anayahubiri.Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi,AMEN. Viongozi wote tuliopo leo hutekeleza kinyume ya tunayo hubiri,aibu kwetu!.
 
Mbona huwasifiiwazazi wako waliohangaika kukulea mpaka hapo ulipo? hilo la kumsaidia mtu ni la kawaida yeye kama binadamu. sio hoja ambayo inatufanya tumkumbuke.... wewe naye ni mateka miongonimwa mateka wa Nyerere legacy
Siwasifii wazazi wangu kwa sababu ni wajibu wao kunitunza,mwl kazi aliyoifanya haikuwa wajibu wake ni msaada na utu tu.Lakini pia nimesema mwl kwa sababu leo ni kumbukumbu yake na si ya wazazi wangu.Unapenda fujo au ulikuwepo juzi mbagala wakati ile text book inakojolewa.
 
kama kumbu kumbu zangu zipo sawa ilkuwa ni gari aina ya 110 station wagon , alipenda sana kuja na hiyo gari musoma , joseph butiku akiwa ndie RC Mara kabla ya bwana MMoja anitwa Balozi Lugoye, Mwalimu alikuwa simple sana Niliwahi kumuona pale Makoko seminary akiwa na Askofu marehemu Justine Samba, yeye akaingia shambani kuwasaidia wanafunzi kulima kitu ambacho hata askofu alishangaa.
Uko sahihi na waweza kuwa shuhuda mzuri,achana na huyu anaesema mwl hakuwahi kutumia landrover ya aina hiyo.
 
Pale kona Panaitwa Nyarusurya! Dah umenikumbusha mbali sana maeneo hayo.
Kulikuwa kunauzwa samaki wengi sana wakati huo,sijui kwa sasa.Kulikuwa na mwl.mmoja mchina au mkolea,nilikuwa siwezi kutofautisha,sijui kama yupo au la?
 
Ilikuwa mida ya saa 9:30 alasiri,pale maeneo ya Musoma alliance,wakati huo nikiwa natoka ktk kiwanda cha Mara Oil(nilipokuwa nafanya kibarua ingawaje ilikuwa child labour kwani wakati huo nilikuwa na miaka 16) mwalimu alipita na gari yake aina ya Land rover akiwa na dereva wake,akamuona mama mmoja pembeni mwa barabara akiwa na ameshikwa na uchungu na hatua za mwisho za kujifungua,mume wake akiwa amesimama pembeni,kwani alikuwa akimsindikiza hospitalini kwa baiskeli,hali ilipokuwa mbaya akamshusha ili ijifungue.Mwalimu akamwamuru dereva kusimamisha gari,akasogea kwa karibu na kumwamuru dereva kumpakia yule mama na kumkimbiza hospitali mara moja. Akampa dereva pesa anunue unga wa ulezi ili utumike kumpikia uji yule mama atakapojifungua,Mwl yeye akabaki pale barabarani kwenye kona ya msm alliance.Magari yakaendelea kupita,yale ya serikali walipokuwa wakimwona mwalimu wanasimama na kutaka kujua kulikoni ikiwezekana aingie kwenye gari.Wote walipewa jibu hili" Nenda,kwani mama aliyekuwa anajifungua hapa hamkumwona?".
Katika siku hii ya leo ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwl.Nyerere,nimeamua kuwaletea ushuhuda huo juu ya moyo wa utu aliokuwa nao mwalimu.Lakini pia hali ya maisha aliyoishi mwl,nani leo hii rais mstaafu anaweza kutumia LandRover Pick up?

aiseee hongera zako kwa kuwa moja wa mashuhuda wa mambo ya JKN ni vizuri sana..
 
Nimesom na machozi yakanitoka, kuna mabaya ya Mwalimu lakiini ukweli hatujapata kiongozi kama huyo. Mungu amlaze mahali pema.
 
Viongozi wa sasa watafanya ila wakati wa kampeni..(ataandaliwa mtu,atasaidiwa,litapita gari,atavunga na atataka gazeti limuandike) Igizo kama hilo part 2 yake uchaguzi mwingine
 
Ilikuwa mida ya saa 9:30 alasiri,pale maeneo ya Musoma alliance,wakati huo nikiwa natoka ktk kiwanda cha Mara Oil(nilipokuwa nafanya kibarua ingawaje ilikuwa child labour kwani wakati huo nilikuwa na miaka 16) mwalimu alipita na gari yake aina ya Land rover akiwa na dereva wake,akamuona mama mmoja pembeni mwa barabara akiwa na ameshikwa na uchungu na hatua za mwisho za kujifungua,mume wake akiwa amesimama pembeni,kwani alikuwa akimsindikiza hospitalini kwa baiskeli,hali ilipokuwa mbaya akamshusha ili ijifungue.Mwalimu akamwamuru dereva kusimamisha gari,akasogea kwa karibu na kumwamuru dereva kumpakia yule mama na kumkimbiza hospitali mara moja. Akampa dereva pesa anunue unga wa ulezi ili utumike kumpikia uji yule mama atakapojifungua,Mwl yeye akabaki pale barabarani kwenye kona ya msm alliance.Magari yakaendelea kupita,yale ya serikali walipokuwa wakimwona mwalimu wanasimama na kutaka kujua kulikoni ikiwezekana aingie kwenye gari.Wote walipewa jibu hili" Nenda,kwani mama aliyekuwa anajifungua hapa hamkumwona?".
Katika siku hii ya leo ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwl.Nyerere,nimeamua kuwaletea ushuhuda huo juu ya moyo wa utu aliokuwa nao mwalimu.Lakini pia hali ya maisha aliyoishi mwl,nani leo hii rais mstaafu anaweza kutumia LandRover Pick up?

Kwa nini hakwenda na huyo mgonjwa mpaka amfikishe hospitali? akachagua kubaki barabarani? mtoa mada leta jibu
 
Nimesom na machozi yakanitoka, kuna mabaya ya Mwalimu lakiini ukweli hatujapata kiongozi kama huyo. Mungu amlaze mahali pema.
nini kimekuliza? alivyomsaidia huyo mama au kuna kingine kinakuliza? Nyerere legacy na wewe mteja pia!
 
Back
Top Bottom