Mwl.Nyerere alifanya jambo hili mbele yangu mwaka 1998

SAGANKA

JF-Expert Member
Jun 9, 2012
313
202
Ilikuwa mida ya saa 9:30 alasiri pale maeneo ya Musoma alliance,wakati huo nikiwa natoka ktk kiwanda cha Mara Oil (nilipokuwa nafanya kibarua ingawaje ilikuwa child labour kwani wakati huo nilikuwa na miaka 16).

Mwalimu alipita na gari yake aina ya Land rover akiwa na dereva wake akamuona mama mmoja pembeni mwa barabara akiwa na ameshikwa na uchungu na hatua za mwisho za kujifungua, mume wake akiwa amesimama pembeni kwani alikuwa akimsindikiza hospitalini kwa baiskeli,hali ilipokuwa mbaya akamshusha ili ijifungue.

Mwalimu akamwamuru dereva kusimamisha gari,akasogea kwa karibu na kumwamuru dereva kumpakia yule mama na kumkimbiza hospitali mara moja. Akampa dereva pesa anunue unga wa ulezi ili utumike kumpikia uji yule mama atakapojifungua.

Mwl yeye akabaki pale barabarani kwenye kona ya Musoma alliance.Magari yakaendelea kupita,yale ya serikali walipokuwa wakimwona mwalimu wanasimama na kutaka kujua kulikoni ikiwezekana aingie kwenye gari.Wote walipewa jibu hili" Nenda,kwani mama aliyekuwa anajifungua hapa hamkumwona?"

Katika siku hii ya leo ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwl.Nyerere,nimeamua kuwaletea ushuhuda huo juu ya moyo wa utu aliokuwa nao mwalimu.Lakini pia hali ya maisha aliyoishi mwl.

Nani leo hii rais mstaafu anaweza kutumia LandRover Pick up?
 
Kama leo hii dhaifu ataweza kufanya huo muujiza kweli au labda afanyie kwenye ndenge daily yupo ulaya
 
Huyu mwingine kila siku kutafuta nchi ya kwenda kuficha alivyotuibia ili siku kikinuka asepe.

Hata "akisepa" ni sawa tu, ana muda gani tena wa kula alivyopora? Ni tamaa tu!!. Tutamkumbuka kwa "USHAROBARO"
 
Jkunayule mwingine mke wake alipewa tenda ya kuja ku-dispose bia zilizo expire, alipiga hela ya kufa mtu.
 
Ilikuwa mida ya saa 9:30 alasiri,pale maeneo ya Musoma alliance,wakati huo nikiwa natoka ktk kiwanda cha Mara Oil(nilipokuwa nafanya kibarua ingawaje ilikuwa child labour kwani wakati huo nilikuwa na miaka 16) mwalimu alipita na gari yake aina ya Land rover akiwa na dereva wake,akamuona mama mmoja pembeni mwa barabara akiwa na ameshikwa na uchungu na hatua za mwisho za kujifungua,mume wake akiwa amesimama pembeni,kwani alikuwa akimsindikiza hospitalini kwa baiskeli,hali ilipokuwa mbaya akamshusha ili ijifungue.Mwalimu akamwamuru dereva kusimamisha gari,akasogea kwa karibu na kumwamuru dereva kumpakia yule mama na kumkimbiza hospitali mara moja. Akampa dereva pesa anunue unga wa ulezi ili utumike kumpikia uji yule mama atakapojifungua,Mwl yeye akabaki pale barabarani kwenye kona ya msm alliance.Magari yakaendelea kupita,yale ya serikali walipokuwa wakimwona mwalimu wanasimama na kutaka kujua kulikoni ikiwezekana aingie kwenye gari.Wote walipewa jibu hili" Nenda,kwani mama aliyekuwa anajifungua hapa hamkumwona?".
Katika siku hii ya leo ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwl.Nyerere,nimeamua kuwaletea ushuhuda huo juu ya moyo wa utu aliokuwa nao mwalimu.Lakini pia hali ya maisha aliyoishi mwl,
nani leo hii rais mstaafu anaweza kutumia LandRover Pick up?

Mwalimu katumia gari aina ya pickup 1998? Nahisi kama umeongeza chumvi.
 
Pale kona Panaitwa Nyarusurya! Dah umenikumbusha mbali sana maeneo hayo.
 
nimesikiliza baadhi ya nyimbo TBC za kile kipindi cha msiba, zile zilikuwa nyimbo nzuri zana hasa kuna nimesikia ya Komba naTOT na ile ya kina Remmy Ongala,
 
69 Reactions
Reply
Back
Top Bottom