Mwl.Nyerere alifanya jambo hili mbele yangu mwaka 1998

Rest in peace baba wa Taifa.

Tupo pa1 na ww ktk philosophy zako japokuwa Radio imaan na ponda wanakulaumu but still we ni baba wa Taifa.
 
Mengine nitakubaliana na wewe, lakini hilo la kusema 'nenda kwani hamkumwona mjamzito hapa?' nitabishana nalo. Palikuwa na jam sana hapo? Ni mzunguko unaojirudia wa barabara? Ulisimama kumsikiliza? Naomba ufafanue hapo ndugu SAGANKA
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini hakwenda na huyo mgonjwa mpaka amfikishe hospitali? akachagua kubaki barabarani? mtoa mada leta jibu[/QUOTE
Ndani ya pickup wangekaaje wote katika seat ya mbele,nahisi alitaka mgonjwa awe comfortable.
 
Siku moja Mwalimu aliagiza waitwe viongozi wakuu wa nchi wakati huo. Rais wa JMT alikuwa ni Ally Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar Salimin Amour na Waziri Mkuu John Samweli Malecela. Kwa kawaida Mwalimu alikuwa ana tabia ya kulala mchana saa 8 na kuamka kati ya saa 10 hadi saa 11 jioni. Siku hiyo saa kumi hivi viongozi hao waliwasili.

Mwalimu ndiyo alikuwa ametoka kuamka na alipoambiwa kwamba aliowahitaji wamefika aliionyesha kufurahi sana. Mwalimu aliwaita bustanini kwake na kuwakabidhi wote watatu kila mmoja Papai kubwa moja na kuwaambia "haya ni matunda toka bustanini kwangu asanteni kwa kuja". wakubwa wale waliondoka Msasani wakiwa na sintofahamu kubwa sana. Inaa maana Mwalimu alituita kuja kutupa mapapai?

Kisa hiki kinawahusu watu watatu ambao wote wako hai. Kama una udadisi nacho kawaulize Mwinyi, Amour na Malecela ili usije sema ni uzushi wakisha ondoka duniani!!
 
Hii inanikumbusha simulizi la Msamaria Mwema. Mwalimu practised heroic virtue.

Nikumbushie vile vile kwamba kwenye miaka ya sitini Mwalimu alikaa vijijini Dodoma kwa siku kadhaa (au wiki au miezi, I am not sure about the length of time) akiwajengea watu fukara nyumba kwa mikono yake mwenyewe. Mwalimu led a holy life.
 
Radio imaana wao wanajadili in a negative way tu
Hakuwatendea waislam mambo mema. Aliwabagua, kuwahujumu miundo mbinu yao (sera ya uchumi ulikuwa ni kuwanyang'anya mali waislamu waliokuwa matajiri wengi, kuwanyang'anya mashule yao, kuua taasisi zao na kuutukuza ukatoliki), na kufanya serikali nzima iwe inafanya kazi kwa interest za viongozi wa kanisa katoliki huku ikiendeleza kuwanyonya waislamu na wakristo wengine walio wakatoliki. Dhambi hii aliyoitendea jamii ya watanzania ndi inafanya tumkumbuke kwa kueleza wasifa wake huu ambao wengine wasiopenda mabadiliko kuyaita "negative". Huu ndo wasifa wa JK Nyerere! sio kama wengi mlivyo aminishwa!
 
Mengine nitakubaliana na wewe, lakini hilo la kusema 'nenda kwani hamkumwona mjamzito hapa?' nitabishana nalo. Palikuwa na jam sana hapo? Ni mzunguko unaojirudia wa barabara? Ulisimama kumsikiliza? Naomba ufafanue hapo ndugu SAGANKA
Hoja yake ni kutaka kuonyesha kwamba ni magari mangapi yamepita na kushuhudia tukio hilo la mama kujifungulia njiani na hawakutoa msaada wowote.Kuhusu kusimama,kwangu mimi ilikuwa ni mara ya kwanza kumwona mwl,na hivyo niliamua kushuhudia tukio zima,kumbuka nilikuwa natoka kazini na hivyo sikuwa na haraka.
 
Kijana mmoja alikuwa amepangwa Lindo kwa Mwalimu na kwa kuwa alishaambiwa na maafisa usalama tabia za Mwalimu Kulala mchana, basi siku hiyo akiwa na bunduki yake akawa anazunguka kwa nyuma kwenye Veranda mwalimu alikuwa anapenda kukaa akisoma vitabu.

Kijana yule akiwa na imani kwamba Mwalimu amekwenda kulala tahamaki uso kwa uso na Mwalimu. Kwa kawaida macho ya Mwalimu yalijaa ukali, akamuuliza "kijana nikusaidie nini" jamaa alipigwa ganzi ya akili asijue la kujibu. Alirudi kwa wenzake akitweta!!
 
Hakuwatendea waislam mambo mema. Aliwabagua, kuwahujumu miundo mbinu yao (sera ya uchumi ulikuwa ni kuwanyang'anya mali waislamu waliokuwa matajiri wengi, kuwanyang'anya mashule yao, kuua taasisi zao na kuutukuza ukatoliki), na kufanya serikali nzima iwe inafanya kazi kwa interest za viongozi wa kanisa katoliki huku ikiendeleza kuwanyonya waislamu na wakristo wengine walio wakatoliki. Dhambi hii aliyoitendea jamii ya watanzania ndi inafanya tumkumbuke kwa kueleza wasifa wake huu ambao wengine wasiopenda mabadiliko kuyaita "negative". Huu ndo wasifa wa JK Nyerere! sio kama wengi mlivyo aminishwa!
Hatu-judge mwl kwa ukatoliki wake,bali kwa weledi,utu na uadilifu.Mwl aliwanyang'anya wakatoliki mashule ili waislamu nao wasome,waulize kina makamba watakwambia.Unaongozwa na hisia tu,ni hatari!
 
JK kafanana sana na mwl katika falsafa. Nilishuhudia akimpa mtoto wa mitaani pipi huku akitabasamu kwa upendo.
 
Uko sahihi na waweza kuwa shuhuda mzuri,achana na huyu anaesema mwl hakuwahi kutumia landrover ya aina hiyo.
Hayo ndo yalikua maisha ya Mwalimu, namshangaa huyo anayeuliza aina ya gari kwamba kuna chumvi imeongezwa. Haya ma-GX hayakua magari yake yeye.
 
naamin kama sifa redio imani wanazompatia mwalimu angekuwa nazo tungekuwa tunaishi kwa aman sana nchin! tungeishi kama zambia vile no idd wala maulid!
 
Mbona huwasifiiwazazi wako waliohangaika kukulea mpaka hapo ulipo? hilo la kumsaidia mtu ni la kawaida yeye kama binadamu. sio hoja ambayo inatufanya tumkumbuke.... wewe naye ni mateka miongonimwa mateka wa Nyerere legacy

UAMSHO.......at work. Hamfikiri mara mbili mnafuata kama siafu... Elimu muhimu
 
Mengine nitakubaliana na wewe, lakini hilo la kusema 'nenda kwani hamkumwona mjamzito hapa?' nitabishana nalo. Palikuwa na jam sana hapo? Ni mzunguko unaojirudia wa barabara? Ulisimama kumsikiliza? Naomba ufafanue hapo ndugu SAGANKA
Kama ulikua unawaza mawazo yangu, ameelezea kirefu kama vile aliendelea kuwepo eneo hilo na kuyafuatilia yote aliyoyasema Mwalimu. Pia hao aliowambia waende eti hawakua wanamuona huyo mama, inamaana yeye mwalimu aliwaona wakiwa wanampita huyo mama bila kutoa msaada???
 
Last edited by a moderator:
Kulikuwa kunauzwa samaki wengi sana wakati huo,sijui kwa sasa.Kulikuwa na mwl.mmoja mchina au mkolea,nilikuwa siwezi kutofautisha,sijui kama yupo au la?

Alikuwa Mjapani alikuja kwa ule mpango wa JICA alikuwa anaitwa Miamoto, alikuwa na mbwa wake anampenda kama nini, alipomaliza muda wake nchini kwa kutambua kuwa Waafrika hatuwapi viumbe hao matunzo bora akamuua ili watakao baki naye huyo mbwa wakamtesa. Hao samaki walikuwa wanakaangwa kwa mafuta machafu yaliyochotwa mtaroni pale Mara Oil yaliyokuwa yameelekezwa kwenda ziwani kama uchafu!...nashukuru hatujafa kwa kula uchafu ule.
 
Back
Top Bottom