Mwizi katumia simu ya wizi kuomba hela, aliyetuma anamdai mhanga, je ni sawa?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Inajieleza hapo wakuu, naomba Mawazo ya busara, Mana hili sijui kama limekaa kisheria.

Ni mtu wa karibu Sana, lakini pia suala la kuibiwa simu ni uhakika analijua maana na vitu vingne pia vimeenda kwa kuvunja.

Mwizi Katumia namba ya mhusika kuomba pesa, na jamaa naye akatuma mkwanja mnono tuu kwa Namba ya Mwizi.

Taarifa ikatolewa kwenye ma groups kua wawe makini, jamaa kuona ndio akajua alituma kwa mwizi,
Sasa anadai pesa yake kwa aliyeibiwa,

Ushauri hapo wakuu,
Je ana Anapaswa kulipwa? Kama ndio ni katika muktadha gani? Yaani kwa kuzingantia nini inalazimika kufanya hivyo?

Au asubiri mwizi adakwe(mpaka sasa 95% anakamwatwa),

Au mazingira yoyote hana ulazima wa kulipwa...?

JIBU LOLOTE napokea maana kuna dilema.
Ukizingatia alituma akilenga kukusaidia,
Lakini pia kuna uzembe kiasi wa kutoongea na mhusika,
Achilia mbali hasara nyingne kwa mhanga.
 
Hapo Dili kwa polisi njia nyeupee..
Kuingia kituoni polis ni Bure ila unatoka na mpunga!
 
Siku hizi hatutumi pesa bila kuongea na muhusika especially ukiambiwa utume kwa namba tofauti na ya muhusika. Huyo mtumaji anywe maji mengi tu huku akisubiri mwizi amlipe
 
mwizi alijuaje nywila ya kuingilia ili afanye miamala kupitia simu aloiiba!?
Mkuu umesoma ukaelewa?
Mwizi katumia laini ya Mhanga(watu wengi hawaweki PIN kwenye laini, hivyo anaitoa kwenye simu husika ambayo kwa asilimia kubwa tunaamini ina lock na kuweka kwenye simu nyingne na kutumia) Kuomba pesa kwa watu wake, ambao pengine kuna baadhi ya Majina Aliyosave kwenye Laini au hata namba zinazoingia, lakini akaelekeza pesa atumiwe kwa namba nyingine,
Hiii ndio michezo yao haya majitu.

Kuna uzembe kwa mtumaji, hii michezo sikuhizi ipo sana, unatumaje pesa kwa msg tu? tena namba inayokuomba pesa sio unayoitumia na huifahamu?.

Mimi Pesa situmi bila kusikia sauti, masuala eti Simu imekufa mike, sijui nimebanwa na kifua ni ujanja wa kizamani sana...

Hata kama ni Kweli ulipo unataka kufa ila nitakuambia chagua kufa au kuongea.
 
Back
Top Bottom